Wewe hujafaidi kitu asee kama Kwa bibi yenu kulikuwa na geti na Tv huko sio vijijini ni mjini huko.
Raha ya kufaidi mwe huru sio kufungiwa kwenye geti. Hizo movie hata kwenu unaweza kuzitafta ukapata tu.
Sisi tulikuwa tunaenda Kwa bibi kijijini Tena miaka hiyo hata CD hazikuwepo
Kwanza wajukuu maximum ni 25 Hivi
Kwa bibi kulikuwa ng'ombe wengi zaidi ya 100!!
Babu alikuwa mkarimu mno na bibi pia.....tukifika tu tunachinja wenyewe mbuzi kubwa la kuchoma tu yaani linaishia juujuu tu kwenye shikome😂
Muda huo Kuna nyama za kubanika zimeshakauka mpaka basi zinaitwa ng'homele kisukuma ni mwendo wa kukata na kuloweka kwenye maji ya chumvi Kisha unakula...
Maziwa sio ya kuuliza ni muda wowote tu unajipimia ....basi wajomba kesho yake mnaenda nao kuchunga pamoja na kuwinda huko mnakutana Watoto shazi mnawinda sungura,digidigi na ndege kama kware ama kanga kama ni masika pamoja na kuchoma uyoga mnakula!!!(Hivi vitu vyote mjini huwezi pata hata ukiwa milionea)
Mkirudi kutoka machungani kulikuwa na bwawa mnaenda kuogelea weee acha tu hapa sio wanawake au wanaume mnaoga mtakavyo maana tulikuwa wadogo wakubwa ndo walikuwa hawaogi...
Mkirudi mtakula mpaka mnakula Tena. Siku ya sikukuu tulikuwa tunaenda kununulia juice cola zile zinaweka kwenye chupa za soda tulikuwa tuna nunua shilingi5 Hadi kumi!!
Michezo ilikuwa mingi sana kuumizwa ilikuwa sehemu ya michezo pia.
Kuna siku hamuendi kuwinda ni Tour ya kusaka matunda pori na kumletea bibi na Babu imagine tulikuwa tunaanza saa3 Hadi saa8 ndo tunarudi na mizigo ya matunda tumechoka mbaya😹😹
Sisi video kipindi chetu huwezi kuikuta Kijiji kiza hata Kwa diwani huikuti wewe ulichoelezea ni miaka ya 2007 hapa tu Kuna CD/DVD!!
Ukweli na miss sana enzi hizo Kuna mto maji tulikuwa tuna yaziba Kisha tunakamata samaki na vidagaa mkimaliza ni kuchoma hapohapo pilipili tulizia huko kula acha kabisa
Kuna matunda mizizi Yale uking'oa linakuwa kama muhoga ila Lina maji tupu matunda Yale hata nyani wanayapenda sana..
Ni vingi vya kuelezea hii ni miaka ya 1995-2002 Hivi acha kabisa
View attachment 3286837