Roho Kuukuu: Watoto Wenye Busara za Wazee

Roho Kuukuu: Watoto Wenye Busara za Wazee

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
778
Reaction score
1,808
Ushawahi kuona mtoto mdogo wa miaka mitano, lakini akiongea, pointi anazotoa ni za mtu mzima wa miaka 60? wakati hata shule hajaanza?

Hawa ndio wale watu wanasema roho zao zilishawahi kuishi duniani zamani, zikafa, zikarudi tena kwenye miili ya watoto.

Wanapenda kukaa na watu wazima kuliko kucheza na watoto wenzao. Hii ndiyo sifa kubwa ya kwanza inayokustua ukikutana na hawa watoto ambao roho zao zimeshapiga round ya kwanza duniani.

Wakati watoto wengine wanagombania vinyago, wanachafuana na udongo, au kupiga kelele za michezo ya kitoto, yeye anawaona kama wanampotezea muda. Kwake yeye, hiyo michezo haina mashiko, Utamkuta yuko bize kwenye mapaja ya watu wazima kusikiliza maongezi yao.

Utamkuta kila wakati amejichomeka katikati ya watu wazima. Anapenda kukaa karibu na babu, bibi, au baba zake akitega sikio. Utadhani anasikiliza siri za serikali, kumbe anafurahia tu busara na stori za maana zinazoongelewa hapo.

Ukipiga nyimbo za diamond, anaweza asionyeshe ushirikiano. Lakini ukidondosha wimbo wa zamani, ule wa miaka ya 70 au 80, utamuona anavyotulia au kuanza kuitikia kichwa kwa staili ya kizamani kabisa. Ni kama ule muziki unagusa memory ya maisha yake ya zamani.

Akifungua kinywa chake kuongea, pointi anazotoa siyo za shule ya vidudu. Anatoa maneno ya hekima, na darasani huwa ana akili kubwa

Hawa ni watoto ambao wanaitwa Old Souls. Yaani, miili ni midogo na mipya, lakini roho zao ndani ni kuukuu, zina uzoefu wa miaka mingi na zimeshaona mengi hapa duniani. Ndio maana hawaoni shida kukaa na watu waliowazidi umri, kwa sababu kule ndiko vaibu lao lilipo.

Kuzaliwa ni kila siku tutazaliwa, maana maisha hayasimami na roho haina mapumziko. Huu ndio ukweli wa mtaani ambao wengi hawauoni, hatuzaliwi mara moja tu pale tunapotoka kufa kwa kuamini nadharia ya reincarnation.
 
Ushawahi kuona mtoto mdogo wa miaka mitano, lakini akiongea, pointi anazotoa ni za mtu mzima wa miaka 60? wakati hata shulroho haina mapumziko. Huu ndio ukweli wa mtaani ambao wengi hawauoni, hatuzaliwi mara moja tu pale tunapotoka kufa kwa kuamini nadharia ya reincarnation.
Akina nani wanaosema?
 
HIyo ni Imani ya dini ya Kihindu kule india reacarnation theory
 
Back
Top Bottom