Nimekumbuka zamani

Nimekumbuka zamani

Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi mizecho yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Sisi wengine ilikuwa ukienda likizo vijijini ni mwendo wa kuchunga Ng'ombe na mbuzi, Na ukirudi mchana unafikia viazi vilivyochemshwa na Maziwa mgando. Sasa fikilia kuchunga mbuzi walivyo wasumbufu hahahaaa bora nilivyokuwa nabakia mjini tu kwakweli.
 
Mimi mpaka sasa natamani kila disemba niwe bush, ingawa ni mara chache tulikuwa tunakutana pamoja wa mjini lakini kwa babu kulikuwa na wajukuu zaidi ya 15! Yes hao ni wajukuu ukiweka familia nzima ni 20+, hawa wazee wa zamani hela ilikuwepo familia haifi njaa na mboga zinabadilishwa kama kawaida.

Menu ilikuwa inawekwa kwenye sinia wajukuu wa mjini peke yao na wakule bush peke yao. Unashanga nyie mpo tonge la kwanza lakini wenzenu washafuta sinia zima hapo mtoto wa kiume analalamika hajashiba ila wakike anacheka 😀

Nakumbuka nilikuwa napenda sana kwenda kuchunga ng'ombe na mabro, kule babu alikuwa anatufungashia kidumu cha maziwa basi tunapitia kuiba ndizi na mihogo mashambani mwa watu. Huko ni full michezo sio kuogelea na mpira.

Hamna wiki iliyokuwa tamu pia chungu kama ile ya kuanzia tarehe 25-1 jan, ilikuwa leo kipaimara hapa kesho pale kidogo mkesha halafu tarehe 2 mzazi anakuambia wakati wakurudi mjini umefika, bibi anakuaga kwa kilio na wewe unalimwaga chozi. Memories zilikuwa zinanihaunt kwa miezi mpaka kufutika ndio nitulie shuleni.

Kwasasa kwa babu wamebaki watu hata 10 hawafiki, inasikitisha kuona bibi umri umesogea natamani angalau Mungu aendelee kumuweka zaidi kila nikienda nimkute. Disemba yangu ni nzuri sana nikienda bush kuliko nikiwa mjini. Miss those old good days.
 
Sisi pia kila mtu alikua na sahani na kikombe chake, kigoda chake na sebuleni ana mahali pake pa kukaa muda kuangalia tv na ratiba ya vipindi ilijulikana vilivyo.

Utotoni mkiwa machalii wengi home ni raha sana, kuna uncle aliletaga Ps kwakweli sikua naenjoy lile dude kabisa.
 
Lakini mlikuwa mnaaenjoy sanaa,. Ile tu mnakuwa wengi mnafurahia ila sikuizi hamna hii kitu
Mkuu; Hebu fikiria maisha yalivyo sikuizi; halafu inakuja "Kampuni" sukari kg.1 ni siku mbili tu imeisha na kati ya hao walokuja hakuna aliyeleta hata nusu kilo ya sukari. Ni gharama aisee.
 
Hahahh,. Asa kipindi kile mtu atoke Dar bila kubeba mikate na biscuits kwanza tunamshangaa katoka Dar ipi🤣🤣🤣🤣
Utasikia mikate ya Dar mizuri sana. Siku Moja nikaamua sinunui mkate huku Dar nikifika mjini kwao nanunua kama wataspot tofauti.
Nimefika wakail vizuri bila hata kugundua huku wakisifu ya dar mizurii
 
Habari za siku nyingi wanajukwaa….

Leo nimekaa nimejiwazia nikajikuta tu naona watoto wa sikuizi hawaenjoy kama ambavyo sisi zamani tulikuwa tunaenjoy,. Watoto wa saizi hawajui hata raha za kwenda likizo kwa bibi

Kwanza niseme tu kuwa bibi yetu kama wajukuu kabarikiwa nao ,. Mpaka sasa nadhani tunaweza kuwa hata tuko 50 na wengine ambao hatuwajui wanaweza kuwa hata 60 tumefika,. Imagine watoto 13 naa wote wana watoto sio chini ya wanne😄😄 ( ila hiii sio lengo la uzi ) ila mtaelewa kwanini nimesema hivi.

Kipindi kile ilikuwa likizo zote za sikukuu yaani December na ile likizo ya pasaka bibi yangu alikuwa anasisitiza wajukuu wotee tuende kumwona,. Yaani tulikuwa tunakuwa wengii kwa bibi ( kila kona unayopita ina mtu😅😅😅) ,. Na kwa vile tulikuwa wengi uharibifu kila siku kuanzia kwenye vyombo watu wanavunja,. mafundi TV sasa ndio kabisa mpaka bibi alikuwa anafungia ndani Tv zake zote hakuna kuangalia mpaka tuondoke,.

Sasa hapo ndio ile mikakati ilikuwa inaanza,. Ikikaribia likizo simu zinaanza kipigwa basi kila watu tunapangiana vitu vya kubeba,. Mie na dada angu tulikuwa tunabeba zetu TV ,. Binamu zetu wengine wa mwanza walikuwa wanabeba deki,. Wa arusha walikuwa wanabeba CD ( baasi hapo kila mtu ataagiza movie anazozitaka wao kazi yao kuzifatuta zilizotafsiriwa wanakuja na CDs Kibao ),. Wengine wa Dar ilikuwa kazi yao kubeba snacks ,.Wengine mipira midoli yaani Ili mradi tu kila mtu awe na chakubeba ….. Yaani ilikuwa tukifika kwa bibi ni kuangalia tu movie kuanzia asubuhi hadi usiku maana ilikua marufuku mtu kutoka nje ya geti😁😁😁

Usiku sasa kila watu wakishaingia chumbani kwao ni muda wa mastori hadi mida mibovu asubuhi hata hakunaa anayekumbuka alilala saa ngapi,. Kila watu wanasimulia stori za nyumbani shuleni yaani ilikuwa raha kipindi kile….

Bibi kwanza alikuwa ananunua sahani nyingi na vikombe vya plastiki kila mtu anamwandika jina kwenye sahani yake ( maana hataki kero mda wa kula zilikuwaga kelele sio za nchi hii watu wanachagua sahani maara vikombe mwisho wa siku kuvunja ),. Baaasi nguo zetu zote zilikuwa zinaandikwa majina ili akija mtu wa kufua kila mtu kambani anaenda kuanua nguo zilizoandikwa jina lake,. Ila bibi😂😂😂

Bibi alikuwa anatuambia yaani babu yenu wakati anajenga hii nyumba aliweka vyumba vikubwa kwajili yenu,. Yaani dream yake ilikuwa muwe mnakuja mnajaa kama hivi mnacheza mnampigia kelele,. Lakini kwa bahati mbaya alifariki bila kumwona mjuu wake hata mmoja ,. Yaani wote tumezaliwa akiwa kashakufa🥹🥹🥹

Kipindi kile ilikuwa hata kama likizo imekukuta mgonjwa utang’a ng’ania usafiri tu hivyo hivyo maana utajisi unyonge wenzio wote wako kwa bibi,.
Sema ndio hivyo sasa watu wenyewe wotee saizi washakuwa watu wazima ,. Wakuoa wameoa na wakuolewa wameshaolewa wengine toka waliendaga nje kusoma haawajarudi wenginee ndio hivyo yaani kwenda kwa bibi sikuizi laabda litokee tukio na hata mkienda hamui wengi na hata hao wachache kila mtu yuko busy na mambo yake yaani nyumba imepoozaaa😔😔 sio kama zamani…
"mafundi tv!" na wewe unasema wa zamani! Kwani zamani tv zilikuwepo, au unasema zamani ya hivi karibuni ya tsmthilia ya Tausi na akina Cheni na yule mhaya aliyekwepa kwenda kwa madiba kujiunga na tamthilia ya SunSet! Nilidhani zamani ya miembe, mipera, mikorosho na mizambarau haina mwenyewe.
 
Nakumbuka kijijini kwetu huko Tarakea bhn, yaani ilikuwa nyumbani tupo familia yetu na watoto wa ndugu zake baba

Sasa bhn unajua watoto mkiwa wengi jioni tukiwa jikoni kila mtu anawahi sehemu yenye joto, hapo ni full kugombania sehemu yenye joto mpaka mama anatufukuza tukae nje ya jiko mpka chakula kiive,

Au kwenda kukata majani acha kabisa, tunaenda kukata nyasi au matete bhn, afu ukute ni msimu wa mvua au ndo mvua zimekata tuu ynavyokuwa mazito ukiyabeba kichwani, Ila kwakuwa tulikuwa wengi ilikuwa full burudani,

Njoo kwenye chakula kinapikwa kingi na ni marufuku chakula kumwagwa, matunda sasa asubuhii mnaamka kuwah maparachichi kama yamedondoka ni kuyakusanya tuu,

Kulala kulikuwa na vitanda vya 6*6 ni kugombania mm nalala ukutani ukiamini mwizi hatokuona 😂 Ila kwa ujumLa nakumbuka kumbukizi nzuri niliyopata na ndugu zangu kaka, dada na mabinamu zangu!


Hakika siku zinasogea aseeh
 
Sisi pia kila mtu alikua na sahani na kikombe chake, kigoda chake na sebuleni ana mahali pake pa kukaa muda kuangalia tv na ratiba ya vipindi ilijulikana vilivyo.

Utotoni mkiwa machalii wengi home ni raha sana, kuna uncle aliletaga Ps kwakweli sikua naenjoy lile dude kabisa.
Kumbe ww ni wa juzi-juzi tu hapo. Eti mnakaa kuangalia Tv. na Uncle kaleta Ps.
Hebu rudi nyuma kule enzi za redio za mbao National na Hitachi halafu kwa bibi mara nyingi kama sio zote ni huko mashambani - gari ikipita inashangliwa na watoto ...Gaaari; Gaaari. Nyie wa hapo mjini na huko kwa bibi inaonekana ni enzi za juzi hapo umeme ukikatika utawasikia watoto: Haaaaaa! kwa muda halafu ukirudi utawasikia: HUOOOOOO. Hakuna cha mvulana au msichana wote ni kelele mtindo mmoja. Huku mashambani ambako ndo kiuhalisia ndo kwa Bibi; wavulana hushirikishwa kazi za kiume - kuchunga, kuvua samaki, kurina asali, kulima na kukata vichaka kuzunguka nyumba ya bibi n.k n.k. Wasichana hushirikishwa kazi za kupika, kufua nguo, kukamua, kuuza maziwa n.k.nk.
 
Sisi tulikua tumeifunga juu ya mti mkubwa chini kuna maanguko ya maji , nikasukumwa nikaenda juu nikazunguka, Nikabinukia upande wa pili wa kamba, then nikadondokea karibu kabisa na jabali ilikua hatari halafu watoto wengine wakakimbia , bahati nzuri kulikua na wadada wanafua wakanitoa ,nilishakunywa maji ya kutosha.
Aisee,. Pole sana
 
Siku hizi mnaambiwa muende Veta wakati kipindi hichO ilikua wakimaliza Chuo tu wanapangiwa maeneo ya kwenda kufanya kazi yaan ajira mkononi kikubwa uwe umesoma tu mpaka darasa la 7 walikua wanaonekana Shule imejaa kichwani, maisha yamevadirika sana
Maisha yamebadilika sana aisee
 
Back
Top Bottom