Mkuu
Step by step huu wizi ni common sana wala usihuzunike.
Ilishawahi kutokea kwetu, siku hiyo tulilala ndani tena vyumba vyote zaidi ya watu7 na wamwisho alilala saa7 usiku lakini tulilizwa siku hiyo.
Alitugutusha dada yetu saa2 asbuhi baada ya kuamka na kukuta mabadiliko makubwa sebureni!
Siku hiyo walibeba screen,music system na fridge. Tulilala usingizi wa kifo asikwambie mtu.
Tulifunga milango yote na kuiacha funguo mezani. Jamaa walipiga tochi wakaiona funguo, wakachana nyavu,wakachukua mti na kuupaka superglue then kiulaiini wakainasa funguo na kwenda kufungua mlango. Mlango ulikuwa na komeo kwa ndani ikabidi wachane nyavu tena dirisha ambalo bahati mbaya sana lilikuwa karibu sana na mlango.. so ikawa rahisi sana kupitisha mkono na kufungua komeo!!
Walikusanya vyao wakajiondokea kiulaiiini!!
Ikabidi nianze msako chini kwa chini kwenye vijiwe vyote vya wahuni na wavuta ganja pale mtaani angalau nijue jamaa huwa wanafanikisha vipi oparetions zao.
Simlizi zao ni ndefu sana ila moja ya zana na nyenzo nyepesi kabisa ambayo wakiiapply lazima usinzie ni MOSHI WA CD ni sumu hatari sana hii ikipuliziwa kisha ukavuta moshi wake au hata hewa/harufu ikikufikia nyakati ambazo kuna upungufu wa circulation ya oxygen.
Kinga kuu ya zoezi hili ni kuacha wazi chombo kilichojazwa maji nyakati za usiku na mara zote hakikisha unalala na funguo zako kitandani mwako uzilinde zikulinde!!
Pia ufugaji wa mbwa nao ni ulinzi tosha ila lazima wawe fully trained japo nao kuna namna wanakamatika kilahisi sana.