SoC03 Kisa cha Funguo na Muuza duka

Stories of Change - 2023 Competition

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Taifa linaweza kupiga hatua ikiwa kila mmoja wetu atakipenda kile cha halali akifanyacho.
Kwa juhudi, maarifa mengi na kujitoa.

Nakumbuka mama Theresa alipata kusema: "It is not what we do, it is how much love we put in the doing."

Nakukaribisha kusoma andiko hili ewe mwanajamiiforums.

Andiko hili limegusia maswala ya maana utawala bora na uwajibikaji na misingi yake katika njia ya fasihi andishi.


Naamka asubuhi, nimepitiliza mda niliopanga kuamka na yote yametokea baada ya kusikia kengele ya saa na kuipuuza huku akili yangu ikisema nilale kiduchu.

nitaamka baada ya dakika 5 sasa nimepitiliza makisio ya dakika 5 yamesonga hadi lisaa limoja.

Picsart_23-05-11_19-45-35-261.jpg


Lakini pia mfukoni hali si shwari na natakiwa kwenda kazini kwangu ambapo ndio kuna kila kitu na hata nauli ya kunisogeza huko sina, naona sio kesi.

natoka nimeshaoga na kujipiga utwuli, nalivaa jua na kutembea kilometa kadhaa na begi mgongoni kwenda kazini kwangu ambapo ni hatua kidogo, mwendo wake kwa miguu sio chini ya dakika 40 hadi saa zima, sina namna, naamua kuliingia hivyo hivyo.

Nafika kazi ambapo ni dukani.

nasalimia wateja niliowakuta wakinisubiri kwa sababu nimechelewa, nawaswabahi, hakuna hanae hitikia wala kufurahi kuniona kwani inaonesha nimewakwazwa kwa kuchelewa kwangu. na bila shaka walikuwa dukani kwangu mda mrefu wakisubiri huduma.

Picsart_23-05-11_19-39-03-958.jpg


Sasa mmoja wapo ambae kwangu kiumri anaonekana ni mdogo, yeye anajitolea kufungua mlango wangu wa duka na nazama mfukoni ili kutoa funguo. najipekua kwa muda mfupi tu nagundua kwamba funguo za dukani nimezisahau nyumbani.
ambapo ni mbali kama nilivyokueleza awali.

Naamua kuacha begi mlangoni pa dukani ili niwahi kwenda nyumbani na kurudi kwa haraka.narudi nyumbani nikiwa na hasira.

Picsart_23-05-11_19-41-35-068.jpg


Napofika nyumbani, kwa haraka naukimbilia mlango na kukuta niliufunga kama ambavyo inastahili, nazamisha mkono kwenye mfuko wa suruali na kutaka kutoa funguo, nagundua kuwa sina funguo za mlango wa nyumba yangu.

Natafakari kwa sekunde kadhaa, akili inanijuza kabisa kuwa baada ya kufunga mlango wakati naondoka asubuhi, niliuweka mfukoni huo ufunguo, najiuliza sasa upo wapi ?.

naendelea kujipekua pekua kila sehemu hadi ambazo siwezi kuweka funguo.

Kwa haraka haraka tu hisia za kudondosha zinanijia, sasa najiuliza, nimedondoshea hapa nilipo ama njiani?

natazama tazama huku na kule, lakini ghafla kumbukumbu inakuja, nakumbuka wakati nimefika dukani kwangu, Nikijitafuta kuhusu funguo za duka, zenyewe zilikuwa mfukoni na nilizishika, na baada ya hapo sikuzirudisha mfukoni bali niliziweka kwenye begi.

Kifupi ni kuwa, funguo zipo ndani ya begi langu nililoliacha kule kwenye mlango wa duka.

Jasho linanitoka, hasira inanipanda, lakini najiuliza namkasirikia nani sasa na ilihali muda unazidi kutafunwa taratibu kama vile nimesimama.

Kwa ghadhabu naanza tena kukanyaga mwendo kuelekea dukani nikiwa nimenuna na sijui nimemnunia nani. Mwendo wa sasa unakuwa wa haraka zaidi kwani akili na nafsi huko vinasemezana ilhali moyo umechoshwa na mizigo ya kusukuma damu kutokana na mwendo kasi nilionao.

Nafika dukani wateja wananilaki kwa kuniuliza kama nimeuona, natikisa kichwa nikitabasamu kwa huzuni na nikijishika kiuno, nawatazama kwa zamu na kuwaambia kwamba sijafanikiwa kuupata, naona wanahoji kwa wahka, kama umepoteza.

"Hapana sijapoteza, funguo nahisi niliiacha ndani, sasa tena nimerejea nyumbani, funguo ya nyumbani nimeiacha kwenye begi hili," nasema huku nikilishika begi na kufanya baadhi ya wananchi wacheke na huku wengine wakinipa pole.

nawaambia wasijali, nanyanyua begi lenye funguo na kulitupia begani na kuwaaga tena jamaa kuwa narejea nyumbani na sasa sijui kama nitarejea tena.

Sasa nimeshakuwa sina haraka tena, maana jua lishakuwa kali, begi langu mgongoni, narudi nalo nyumbani.

Nikiwa njiani simu yangu inaita na kuna mtu ananiomba nionane nae dukani kwangu.

Picsart_23-05-11_19-43-31-942.jpg


ili tupange kuna swala la dharula linahitajika kufanyika jioni.
namwambia sawa anipe kama saa moja hivi nitakuwa nimerejea. Sasa naamua kukaza mwendo ili nikachukue funguo na kuwahi hilo swala.


Nafika nyumbani na kulitua begi chini, ili kutoa funguo za mlango wa chumba changu. Simu yangu nayo inaita, naitazama na kukuta ni yuleyule mtu ananipigia tena, nadhani atakuwa anataka kunikumbusha tu nisikawie nilipo.

naipotezea na kuamua kwanza kuchukua funguo nifungue na kujitoma ndani, nikiwa huko ndio napokee simu.

nashika funguo ndani ya begi na kutoa, natoa funguo za ofisini, narudia tena kuzamisha mkono ndani ya begi na kuchakura chakura, lakini funguo nayoitafuta siipati, napigwa na mshangao, na sasa naamua kumwaga vitu vyote palepale nje ya mlango wangu.

Pamoja na kufanya hivyo, lakini naikosa funguo na simu yangu nayo inakata baada ya kuita kwa muda mrefu na sikuipokea. Nakaa chini nikiwa hoi.

Simu yangu inaita tena, naipotezea kwa sababu nahisi ni kero tu, inaita tena hadi inakata wakati huo hata cha kufanya sijui na sifahamu ni wapi ilipo funguo.

Mara unaingia Ujumbe wa maandishi kwenye simu yangu.

Unaniomba nipokee simu, nafungua na kuusoma kivivu, kabla hata ya kuamua ni kipi cha kufanya, simu inaita tena na sasa napokea kiunyonge tu.

Mpigaji anachofanya ni kuniuliza ni wapi nimefika? Nami namjibu kiufupi tu kuwa nimefika nyumbani, ananiuliza tena nitarejea baada ya muda gani? namwambia muda huu huu, nataka kurejea huko dukani.

"Vipi funguo umeipata?"

"Jamaa yangu, hata nisiongee mengi, funguo nimeipata, lakini sasa.., ngoja tu nije huko tutaongea zaidi."

"Anhaa, sawa nilidhani haujauona, maana hapa kwenye geti la dukani kwako tumeokota funguo moja tukadhani huenda ni ya kwako."

"Ipoje hiyo funguo?"
nauliza huku nikinyanyuka kwa kasi kutoka pale nilipokuwa nimeketi.

Jamaa anielezea, lakini hata kabla hajamaliza, namwambia kuwa hiyo funguo ni ya kwangu, aendelee kukaa nayo hadi nifike.

Kwa haraka tena nachukua begi langu na kwa uhakika kabisa naiweka funguo kwenye mfuko wa suruali na kuanza tena mwendo kuelekea ofisini kwako.

Nawakuta wateja wachache wananisubiri, natoa funguo na kufungua duka, najiuliza niwahadithie kilichonipata ama nipotezee?

Lakini kwanza namuuliza jamaa aliyeokota funguo kama anayo, nae bila hiyana anaitoa na kunipatia, ninapoiona tu na kujua papohapo ni yangu , najisonya mwenyewe.

"Kulikoni Tanzania ?"

"Ndugu yangu ningekuwa nimefanya tukio lolote la ajabu, ningesema itakuwa ni nuksi, lakini ndio kwanza nimeamka, najiuliza ni nini hiki ? ".

"lakini kama ungepokea simu yangu hauoni kama ungefidia mda uliopoteza awali"

nacheka na kuwahadithia mwanzo mwisho, wanacheka kwa sauti na kunipa pole huku wakinisaidia kufungua geti la duka , wengine wakishika fagio na kufagia.

Nawasilisha Ally Nassor Px
 
Mangi alikosa umakini ila juhudi labda tuseme sikuhiyo alikuwa mchovu. Siku hiyo mangii hakuwa makini ila hakuwa mzembe
Tunaweza tukakosea na kuwakwaza wengi ila wapo watakao tuvumilia na kutaka kuona tukisahihisha tulipokosea
 
Mangi alikosa umakini ila juhudi labda tuseme sikuhiyo alikuwa mchovu. Siku hiyo mangii hakuwa makini ila hakuwa mzembe
Tunaweza tukakosea na kuwakwaza wengi ila wapo watakao tuvumilia na kutaka kuona tukisahihisha tulipokosea
Upo sahihi kabisa kiongozi .

Asante sana kwa kusoma andiko langu lakini pia naomba ukipata mda ulipigie kura andiko langu.

Kura yako ni muhimu sana kwangu 🤝🤝
 
Mangi alikosa umakini ila juhudi labda tuseme sikuhiyo alikuwa mchovu. Siku hiyo mangii hakuwa makini ila hakuwa mzembe
Tunaweza tukakosea na kuwakwaza wengi ila wapo watakao tuvumilia na kutaka kuona tukisahihisha tulipokosea

Huyo siyo Mangi, Mangi hawezi kuzembea hivyo!
Labda ni Muhha!!
 

Asante sana kwa kusoma andiko langu lakini pia naomba ukipata mda ulipigie kura andiko langu.

Kura yako ni muhimu sana kwangu

Kumbe ni ishu ya kura mkuu?
Ila sasa mbona kama kisa umecopy, na kufanya editing kiaina...!
 
Back
Top Bottom