Nimeibiwa kiboya kweli, hata sijielewi

Nimeibiwa kiboya kweli, hata sijielewi

asante kwa kunitusi mkuu nakuombea usiibiwe wala kutapelia siku zote uwe mjanja tu

Mkuu sijakutukana, nilichosema shukuru hawajakufanyia kitu kibaya maana kwa maelezo yako ulilala fofofo kwamba mtu au watu wakaingia kwako, wakakata nyavu wakaingia ndani,akachukua funguo akafungua mlango,akawasha taa,akaenda sebuleni akapekua pekua ndani.

Kisha akachukua tv na rimoti yake tu kisha akafunga na kukurushia ufunguo hapo tu bado hujashtuka,hapo ulilala au ulikua umekufa, mwanaume unalalaje hivyo aisee.

Kwa maelezo yako ingewezekana kabisa hao watu kukufanyia ubaya wewe na mke wako maana mlikua hamjitambui.

Ndio maana nikasema shukuru wahajaku- David Cameroon.
 
Wakati mwingine unafunga mlango funguo unatupia mezani mwizi akichungulia anaona ufunguo anauvuta then anafungua mlango na kuingia kama anaingia kwake.

Huyo mwizi wako alikutaimu pale ulipofanya kimoja na kuanza kukoroma akajuwa huwezi kuamka tena hadi asubuhi.

Ila mnalala vibaya nyie wawili, mjitahidi kupunguza huo usingizi wenu, siku ingine watamla mkeo huku unatazama.
 
Pole sana kwa kuibiwa uwa inauma sana.Ila nakushauri uwe unasali kabla ya kulala mkabidhi Mungu kila kitu na kama ni mkristo soma zaburi ya 23 kabla ujalala tubu dhambi zako zote mengine mwachie Mungu akulinde.Samahani kama sio mkristo
 
Aliekuambia kakuibia anakujua ndio jibu lake...
Amini kuna jamaa yangu mmoja alikua anakunywa bar ulipokaribia mda wa kuondoka kumbe alikua anafuatiliwa na mijamaa mitatu mpk kwake nae akaistukia akafika hom akazuga anafunga milango na kujitupa sebuleni kama kazidiwa na ulevi jamaa baada ya nusu saa wakaanza kukata nyavu kumbe alishawastua majirani zamani...wakakamatwa huko huko nje walipokua wanaangaika kuivuta simu katika chaji mmoja alikimbia...kilichofuata ni tairi na petrol vilihusika tena kimya kimya mpk leo huyo aliekimbia kamtumia jamaa wazee wake waje wamuombe msamaha kumbe ni kijana wa mtaa kabisa ila hajakanyaga tena mtaani na maisha kaamishia mkoani...so fuatilia vizuri na vijana wa mtaa hao!!!
 
Wakuu, naleta kwenu hili ili nipate uzoefu na namna ya kujikinga isitokee tena.
Ni hivi, nina nyumba yenye ukuta wa kozi saba kote na geti na ninaishi mimi na wife tu ndani kuna vyumba viwili havikaliwi na mtu. Sasa naamka nakuta flat sceen na remote yake haipo na mlango mkubwa uko wazi wakati kabla ya kulala niliufunga nakumbuka.

Jamaa karuka ukuta, kachana nyavu ya dirisha, kachukua funguo kafungua mlango kaingia sebleni kawasha taa kazunguka room zote manake nimekuta pamepekuliwa na mashuka yametanduliwa kama alikua anatafuta kitu isipokua chumba nilicholala mimi tu na taa kawasha cha ajabu kabeba hiyo tv na remote yake tu pamoja na raba zangu zilizokua mlangoni nje na kuacha vitu kibao vya thamani ambavyo vilikua wazi tu.

Baada ya hapo katoka na funguo kafungua geti then funguo kazitupa mlangoni. Naamka sioni tv, kuchek mlango umerudishiwa tu kuzunguka nje nakuta funguo zangu ziko nje zimetupwa ikanibidi nicheke tu na kushukuru Mungu.

Katika mazingira ya kawaida sio rahisi mimi na wife kulala hivi lazima kuna ujanja wamefanya hebu tupeane uzoefu na namna ya kujikinga na hizi mambo jamani manake ni hatari sana.

Daaah! kumbe mnateseka hivyoo alafu mnatusemaaa kuwa wa mikoani tunawasumbua tukija dar??? hao wezi hawawasumbui?
Huku mikoani kwetu sometime nalala nimerudshia mlango na naamka poouuuwaaa sijaguswaa na hakijaguswa kituuu
 
watu wengi wakifunga mlango wenye kitasa wanachomoa funguo! kumbuka design y kitasa ni kwamba funga mlango zungusha funguo ktk engo ambayo ukivuta funguo haitoki! kasha iache hapo mlangoni. ukiitoa kibaka hua anakuja kufanya tathmini ya mapungufu mlangoni akiiona haipo kwa ndani anacheki mezani n.k. very simple. lakini mbali na kitasa kumbuka kuweka komeo kuongeza ulinzi zamani uswazi ulikua ukifunga mlango unachomeka glasi ya chuma kwenye mkono wa ndani wa kitasa akinyonga tu kwa nje glasi inadondoka hahaha anatoka mbio.
 
Mambo ya bongo watu wanmadawa ya kulevya ya spray wanakupulizia kupitia dirishani baada ya dk kumi hivi waingia kama kwao vile huwezi hata kushtuka unakuwa kama umezimia hivi

chakufanya

ukilala hakikisha una chombo kilicho na maji na kiwe wazi kama jagi hivi pana kiasi

maji huweza kusharabu sumu hiyo na kuipunguza kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba wewe na waliomo ndani si rahisi kusinzirishwa kwa sumu hiyo,

swali zaidi kama unalo

Juzi tupo msibani dodoma tukaibiwa nyumba nzima yaani mwizi kama kwake kaingia chumba hiki kasachi kila mmoja kasomba,kaingia kwingine kasachi imagine watu wanavyolala wengi msibani na kwa kugusana mtu aingie chumba kwa chumba mtu kwa mtu na hakuna hata mmoja aliyeshtuka
 
Duh!! Hiyo hatari ilikuwaje? maana ninavyojua msibani watu hawalali wote pole aisee
 
Umenikumbusha siku naibiwa dish langu (jeusi la nyavu) Nawahi asubuhi kuwasha TV naambiwa No signal!! Naanza kufokea watoto mmeharibu receiver hadi natoka nje kufuatilia waya/cable nakuta dish halipo pamoja na chuma chake!! Nikabaki kudaganywa waloge kwa kuwawekea dawa kwenye nyayo zao😀😀 Niliamua kununua Zuku na kuifunga dirishani kwangu. Sina hamu na wezi,acha wachomwe tu.
 
Watu wengi huamini huibiwa na watu wanaowajua kitu ambacho c kweli saana.ila kwakujilinda style waliyo 2mia hakikisha chumba unacholala kuwe na mabeseni ya maji hata mawili yaliyo na maji na yawache wazi hutalala km walivyo kufanyia yashawatokea wengi hayo ndugu.
 
Wakuu, naleta kwenu hili ili nipate uzoefu na namna ya kujikinga isitokee tena.
Ni hivi, nina nyumba yenye ukuta wa kozi saba kote na geti na ninaishi mimi na wife tu ndani kuna vyumba viwili havikaliwi na mtu. Sasa naamka nakuta flat sceen na remote yake haipo na mlango mkubwa uko wazi wakati kabla ya kulala niliufunga nakumbuka.

Jamaa karuka ukuta, kachana nyavu ya dirisha, kachukua funguo kafungua mlango kaingia sebleni kawasha taa kazunguka room zote manake nimekuta pamepekuliwa na mashuka yametanduliwa kama alikua anatafuta kitu isipokua chumba nilicholala mimi tu na taa kawasha cha ajabu kabeba hiyo tv na remote yake tu pamoja na raba zangu zilizokua mlangoni nje na kuacha vitu kibao vya thamani ambavyo vilikua wazi tu.

Baada ya hapo katoka na funguo kafungua geti then funguo kazitupa mlangoni. Naamka sioni tv, kuchek mlango umerudishiwa tu kuzunguka nje nakuta funguo zangu ziko nje zimetupwa ikanibidi nicheke tu na kushukuru Mungu.

Katika mazingira ya kawaida sio rahisi mimi na wife kulala hivi lazima kuna ujanja wamefanya hebu tupeane uzoefu na namna ya kujikinga na hizi mambo jamani manake ni hatari sana.

Kuna dawa huwa wanapulizia chumbani maarufu NUSU KAPUTI , hiyo dawa ikipulizwa ndani ya chumba lazima ulale upitilize isivyo kawaida, mie niliibiwa hadi kitandani huku nimechomeka net. Wakavuta net wakachukua simu zangu. Tukio hilo kamwe sitalisahau ndani ya Tangu. Pole sana. What goes around comes around.
 
Watu wengi huamini huibiwa na watu wanaowajua kitu ambacho c kweli saana.ila kwakujilinda style waliyo 2mia hakikisha chumba unacholala kuwe na mabeseni ya maji hata mawili yaliyo na maji na yawache wazi hutalala km walivyo kufanyia yashawatokea wengi hayo ndugu.

Naunga MKONYO HOJA

👏👏👏👏👏👏👏👏👍
 
Mkuu Pole sana kwa tukio hulo.Na mumshukuru saana mungu kwamba mpo wazima.

Hembu tuambie Weekend yako uliianza vipi na kuimalizia jana kwa style ipi?

Maana kuna Mshkaji wangu yeye alilala nyumba yoote milango wazi,cha ajabu gari aliiacha Bar na yeye akakodi Taxi.
Cha kushangaza kuamka asubuhi akaanza kuitafuta gari na kusema imeibiwa,akaenda vituo vyoote vya Polisi kusema kwamba Gari yake Imeibiwa na nyumba imefunguliwa kwa Master Key.

Sasa alitokea jamaa mmoja mwenzie akamuambia mkuu haujavunjiwa nyumba wala haijafunguliwa,utakuwa ulilala milango wazo,jamaa alimtukana balaa,na kumuambia oyaaa mie ninaakili zangi timamu,siwezi kulala mlango wazi.
Basi jamaa akawa mstaarabu,na kumuambia unajua kwamba gari yajo uliicha Bar?na uzuri Bar yenyewe kwa mlio Zanzibar ni Gymkhana Bar ambapo ulinzi upo mzuri sana.Ikabidi jamaa aliganda akavuta kumbukumbu kwa aibu akasepa wiki nzima mtaani hayupo.

Sasa nakuuliza kujua je weekend yako iliishaje mkuu na mlikuwa nanani siku hiyo
Yep Gymkhana pakosawa kiulinzi shida inakuja usirogwe kumsahau mpenzi pale!kwa hawa wapenzi wetu wasiojitambua itakuwa shida kuu!
 
Mambo ya bongo watu wanmadawa ya kulevya ya spray wanakupulizia kupitia dirishani baada ya dk kumi hivi waingia kama kwao vile huwezi hata kushtuka unakuwa kama umezimia hivi

chakufanya

ukilala hakikisha una chombo kilicho na maji na kiwe wazi kama jagi hivi pana kiasi

maji huweza kusharabu sumu hiyo na kuipunguza kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba wewe na waliomo ndani si rahisi kusinzirishwa kwa sumu hiyo,

swali zaidi kama unalo

Zinaitwaje hzo spray?na zinauzwa bila taratibu maalumu kwamba unaenda fanya nayo matumiz gan???
 
...jiandae maana siku nyingine atavirudia hivyo vya thamani alivyoviacha
 
Mkuu German Shepherd mmoja akiwa na miezi kama 3 hivi unaweza mnunua kuanzia sh 300,000 mpaka 600,000 na ni vizuri ununue mdogo ili apate mafunzo unayotaka wewe, pili mafunzo kwa trainer inaweza cost sh 200,000 au zaidi kutegemeana na aina ya mafunzo unayotaka apewe, tatu Msosi wao mfano mimi huwa nachukua mahindi,dagaa, na calcium au damu kidogo nasaga basi kijana anawapikia wanakula wananenepa balaa.
Asante mkuu.Kumbe sio Ghali kivilee.
Tatizo watu wengi tunaona kwamba German Sherpherd ni ghali saana kuliko hata Maisha yetu.
Maana ukitaka cost isiwe kubwa basi mfanye kama member ndani ya familia,hapo ndio utaona kwamba hana gharama kwenye kulisha.
 
Yep Gymkhana pakosawa kiulinzi shida inakuja usirogwe kumsahau mpenzi pale!kwa hawa wapenzi wetu wasiojitambua itakuwa shida kuu!
Hahahaha,Bora pale Kuliko kwenda nae Dem mzuri mwisho wa mwezi pale Mombassa Mesi(Oposite SOS),wajeda mara wanasepa nade kama hajatulia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom