Nimegundua mchumba wangu kanisaliti baada ya kuona meseji za mapenzi kwenye simu yake

Nakumbuka jamaa angu nae ilokuwa Bado Kam mwez wafunge ndoa akazifuma msg za mke wake alikuwa anachakatwaga na docter ila alivyo washirikisha wazazi wake walimwambia amoue huyo huyo amsamehe ..kwam Ni kosa la Kwanza
Aisee. Ni mtihani sana.
 
Ushauri mbaya usimuinulie mwanamke kisu akitoka Apo ataenda kuwaambia wazaz wake kuwa mligombana kidogo tu unakipilia visuu atakuacha kwa Hilo.....

Wew fany kutafuta namb za yule nchemba alifu muulize kuwa nakuachia huyu demu wee c ndio kipangq
Siku ingine usijaribu kufanya hivyo jamaa yangu. Unaweza kwenda huko kumuuliza njemba. Lazima mtapishana kauli. Bahati mbaya utaumizwa wewe,iwe kwa maneno au hata ngumi,ksbb wewe ndio utakuwa umeenda umepanic,halafu yeye unaemuuliza hana cha kupoteza,anakujibu vyovyote.

Katika maisha yangu ndicho kitu nimejiapia,siwezi kugombana na mwanaume alie kwenye mahusiano na mpenzi,mchumba au mke,ksbb ya mwanamke. Usichokijua unaweza kuta mwanamke huyo ndio anampenda zaidi.

Dunia ya wanawake wa sasa hivi ukiendelea kuweka methali zako za zamani eti usimuinulie kisu mwanamke,utachelewa mkuu. Kile kisu ni cha kumpiga mkwara,na akiona jisu hewani ataropoka yote. Ila tu uwe na kifua kipana cha kujizuia kama mimi
 
Zi print hizo sms halafu siku mko pamoja na wazazi wake fanya kama unataka kuwapa picha za location ambayo ungependa muende siku ya harusi kupiga picha halafu waombe maoni yao

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wazazi wanaweza wakaaga hapo hapo.....

Na kama una hela sasawazazi wake wanaweza kukuomba msamaha mzito ukakugusa kuliko hata muhusika mwenyewe.
 
Hii ni kweli ama ni story tu mkuu,? Pole ila huyo dada si hata angefuta hizo sms jamani na pia kama umeamua kua kwenye serious relationship na mnatarajia ndoa hayo mambo mengine angeachana nayo tu ona sasa kinachoenda kutokea

Nakushauri usiwatumie wazazi jaribu kumuonesha na uone atajitetea vipi? Huenda ni rafiki yake katumia simu yake kuwasiliana na huyo mkaka(kama impossible hivi) ila ongea naye huenda majibu yake yakakutuliza jazba kidogo mkuu
Ndo maana nakupenda
 
Mkuu usaliti huwa hauvumilik ukiendlea kuwa nae jiran moyo wako utakumbuka mazuri yake
Hapo kumuacha tu ndy suluhisho huo mchezo kam akizoea ww utakuw unaumia tu utavumilia ad lin
 
DAH! Pole sana mkuu. Mapenzi yanauma nyiee! Acheni tu. Swala kama lako lilinikuta hapo mwaka jana tu.Ilikuwa niwe mume wa mtu sasa sema tu bidada alipuyanga vibaya.

Ilikuwa kipindi cha mwezi mtukufu mwishoni wakati huo nilishapeleka posa kwao majibu yakarudi fresh ikawa imebakia swala la mahari tu ambalo tulipanga kupeleka baada siku kadhaa.

Basi siku hiyo ilikuwa weekend alikuja kunitembelea home. Kawaida swala la misosi siku hiyo huwa analisimamia mwenyewe. Basi mida flani akatoka kwenda sokoni kununua mazaga simu akaacha kwenye charge. Muda si mrefu tangu atoke simu ikaanza kuita kwa fujo nikaipuuzia baadae zikaanza kuingia meseji nyingi nikaona sio mbaya ngoja nizicheki.

Aisee! nilihisi pumzi zinanibana, moyo ulipiga kwa kasi hadi nikahisi kizunguzungu kikali nikaamua kukaa chini. Nilikuta meseji kali za mapenzi jamaa akimwagia sifa mpenzi wangu kisha akamuomba wakutane tena baada ya Ramadhani yaani katika sherehe za sikukuu ya Eid.

Nakiri katika siku nilizowahi kuumia katika maisha yangu basi hii ilikuwa namba moja. Nikaona sio swala nikajikaza kiume aliporudi nikamuweka chini then nikamuonesha madudu yake yote akajitia kulia palee, akaomba msamaha na kumlaani shetani.

Sikutaka mambo mengi nikamuomba arudi home maana kwa jazba niliyokuwa nayo ningeweza kumjeruhi vibaya.

Inshort alipoondoka nilimpigia simu mshenga nikamueleza kila kitu. Yeye akaniomba nitulize hasira, akanipa siku kadhaa nijifikirie kwanza.

Baada ya kuona msimamo wangu ni ule ule kikaitishwa kikao wazazi wa pande zote mbili wakiwepo baada ya majadiliano ya muda mrefu hatma ikawa ni kuvunja uhusiano kisha nikarudishiwa kishika uchumba changu, kila mtu akachukua hamsini zake.

HIVYO YANI..
 
Ukiwazingatia Sana hawa viumbe .unaweza ukaja kufanya maamuzi mazito .
Mimi kuna demu amenidanganya alikuwa na mimba yangu.kwa kuwa Mimi nipo dar yeye yupo Zanzibar nikawa namuhudimia.

Hapo Kati Kati yakatokea Mambo mengi Sana.
Jana napigiwa simu na jamaa anajitambulisha yeye ndo alikuwa amemuoa huko Zanzibar na Hana mtoto yeyote.alikuwa ananipiga Tu.
Ni Stori ndefu.

Nimeamua kumpotezea ninachoshukuru nimejitoa kwenye matatizo ya KUPIGWA hela Kwa mtoto hewa.
Binafsi nimemsamehe.
Nakubali mwamba
 
Habari za asubuhi wakuu. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani.

Wakuu bila kupoteza muda ni kwamba leo asubuhi nikiwa tumelala, mpenzi wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa tano aliniomba nimsaidie kutengeneza simu yake kwa sababu ilikuwa na matatizo katika upande wa WHATSAPP.

Katika kuitengeneza nimekutana na meseji mbaya sana ambazo zilisababisha nitetemeke mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kiukweli nimejikaza kama mwanaume ili asigundue chochote.

Nikawa nimepiga picha zile meseji kwa camera ya mbele(screenshot) na kujitumia. Ni meseji ambazo zinaonesha few days ago alikuwa guest House na mwanaume. So yule mwanaume alikuwa anaomba wakutane tena pamoja na anakumbushia walivyofanya siku hiyo na kumsifia shemeji yenu kuwa anajua mambo sana.

Kwa muktadha huo hapo juu wakuu. Nipo nae hapa ndani natamani nimmalize kabisa ila roho inasita ingawa hajui kama nishajua usaliti alioufanya. Kiukweli imefikia muda nafsi yangu haitaki kumuona kabisa. Tangu saa tatu nipo tu nimelala naugulia maumivu wakuu.

Je nimpe taarifa au nisubiri mpaka siku ya send off yake nije nimuwekee zile picha za screenshot kama zawadi yake na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu na uchumba wetu?

Je nimtumie meseji hizi ili ajue kwamba nimegundua uchafu wake au nizitume kwa wazazi wake ili wajue matendo machafu ya mtoto wao?

Naomba tupeane uzoefu na mawazo wakuu. Najua wapo ambao watakuja kunikejeli ila it hurts a lot when you do really love someone halafu ana-cheat.

Ahsanteni na karibuni kwa ushauri pamoja na michango yenu wakuu maana nipo katika njia panda japo bado nipo imara sana.
Mshukuru Mungu amekuonesha mapema, achana nae tulia utafute Mwanamke mwingine. Bora usingejua wazi.
 
nakushauri kama umeridhia huwezi endelea nae piga chini bt kama bado unamhitaji piga moyo konde maisha yaendelee

Na wewe acha basi ushauri wa kimama!!!

Unazungumza habari za kujipima kama anahitaji kuishi na huyo malaya,unaona hapo kuna cha maisha kuendelea tena?yaani unamshauri kabisa mdau aishi na malaya anayejua muda wowote ataenda kugongwa ngozi hivi huyu angekuwa ndugu yako ungethubutu kumpa ushauri huu?

Hakuna mke hapo hao ni wale wameumbwa kudanga maisha yao yote hata huyu asingeziona hizo sms na wakafunga ndoa ipo siku karma ingechukua nafasi yake na wakaachana tu hapa ni Mungu ameepusha mapema.

NB:nakushauri next time cha kuandika huna soma post za wajumbe inatosha.
 
Mkuu una utoto mwingi, karibu 85% ya wanandoa wanachapiwa na baadhi wanajua bt wamepiga moyo konde na maisha yanaendelea
 
Mkuu ni hatari sana kuendelea naye.
Huyo bwana mdogo hajayajua maisha anachukulia vitu simple simple sahihi ni sahihi kosa ni kosa hajaweza kutofautisha bado hivi vitu viwil that's why anashauri as if anatoa wazo la kwenda kuchukua mkopo bank.
 
Huenda ni rafiki yake katumia simu yake kuwasiliana na huyo mkaka(kama impossible hivi) ila ongea naye huenda majibu yake yakakutuliza jazba kidogo mkuu

Hivi ninyi wanawake wote inawezekana akili zenu zinafanana eti???

Ulichokiandika hapa unaamini kabisa kwa uelewa wako kinawezekana?Tanzania hii iliyojaa simu za kichina za mafungu kwa 10K unapata leo useme hapa kuna kuazimana simu tena ili wapenzi wawasiliane?
 
Habari za asubuhi wakuu. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani.

Wakuu bila kupoteza muda ni kwamba leo asubuhi nikiwa tumelala, mpenzi wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa tano aliniomba nimsaidie kutengeneza simu yake kwa sababu ilikuwa na matatizo katika upande wa WHATSAPP.

Katika kuitengeneza nimekutana na meseji mbaya sana ambazo zilisababisha nitetemeke mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kiukweli nimejikaza kama mwanaume ili asigundue chochote.

Nikawa nimepiga picha zile meseji kwa camera ya mbele(screenshot) na kujitumia. Ni meseji ambazo zinaonesha few days ago alikuwa guest House na mwanaume. So yule mwanaume alikuwa anaomba wakutane tena pamoja na anakumbushia walivyofanya siku hiyo na kumsifia shemeji yenu kuwa anajua mambo sana.

Kwa muktadha huo hapo juu wakuu. Nipo nae hapa ndani natamani nimmalize kabisa ila roho inasita ingawa hajui kama nishajua usaliti alioufanya. Kiukweli imefikia muda nafsi yangu haitaki kumuona kabisa. Tangu saa tatu nipo tu nimelala naugulia maumivu wakuu.

Je nimpe taarifa au nisubiri mpaka siku ya send off yake nije nimuwekee zile picha za screenshot kama zawadi yake na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu na uchumba wetu?

Je nimtumie meseji hizi ili ajue kwamba nimegundua uchafu wake au nizitume kwa wazazi wake ili wajue matendo machafu ya mtoto wao?

Naomba tupeane uzoefu na mawazo wakuu. Najua wapo ambao watakuja kunikejeli ila it hurts a lot when you do really love someone halafu ana-cheat.

Ahsanteni na karibuni kwa ushauri pamoja na michango yenu wakuu maana nipo katika njia panda japo bado nipo imara sana.
Subiri umuwekee kwenye gift box siku ya send off na umsend off kwa wazazi wake siku hiyo hiyo
 
Hivi ninyi wanawake wote inawezekana akili zenu zinafanana eti???

Ulichokiandika hapa unaamini kabisa kwa uelewa wako kinawezekana?Tanzania hii iliyojaa simu za kichina za mafungu kwa 10K unapata leo useme hapa kuna kuazimana simu tena ili wapenzi wawasiliane?
Hivi umeona nilichoandika kwa hiyo bracket mkuu?(immposible) Afu hizo simu ziko wapi mbona mitaani watu wanaazimana simu sababu hawana ,ama ikiwa hana salio na mabando yalivopanda bei ujue, ila nimesema hizo ni asilimia chache to impossible, inabidi amuulize vizuri tusimuhukumu kabla
 
Back
Top Bottom