Nimegundua mchumba wangu kanisaliti baada ya kuona meseji za mapenzi kwenye simu yake

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,070
2,000
Habari za asubuhi wakuu. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani.

Wakuu bila kupoteza muda ni kwamba leo asubuhi nikiwa tumelala, mpenzi wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa tano aliniomba nimsaidie kutengeneza simu yake kwa sababu ilikuwa na matatizo katika upande wa WHATSAPP.

Katika kuitengeneza nimekutana na meseji mbaya sana ambazo zilisababisha nitetemeke mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kiukweli nimejikaza kama mwanaume ili asigundue chochote.

Nikawa nimepiga picha zile meseji kwa camera ya mbele(screenshot) na kujitumia. Ni meseji ambazo zinaonesha few days ago alikuwa guest House na mwanaume. So yule mwanaume alikuwa anaomba wakutane tena pamoja na anakumbushia walivyofanya siku hiyo na kumsifia shemeji yenu kuwa anajua mambo sana.

Kwa muktadha huo hapo juu wakuu. Nipo nae hapa ndani natamani nimmalize kabisa ila roho inasita ingawa hajui kama nishajua usaliti alioufanya. Kiukweli imefikia muda nafsi yangu haitaki kumuona kabisa. Tangu saa tatu nipo tu nimelala naugulia maumivu wakuu.

Je nimpe taarifa au nisubiri mpaka siku ya send off yake nije nimuwekee zile picha za screenshot kama zawadi yake na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu na uchumba wetu?

Je nimtumie meseji hizi ili ajue kwamba nimegundua uchafu wake au nizitume kwa wazazi wake ili wajue matendo machafu ya mtoto wao?

Naomba tupeane uzoefu na mawazo wakuu. Najua wapo ambao watakuja kunikejeli ila it hurts a lot when you do really love someone halafu ana-cheat.

Ahsanteni na karibuni kwa ushauri pamoja na michango yenu wakuu maana nipo katika njia panda japo bado nipo imara sana.
 

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,416
2,000
Sasa hayo yote ya nini mara kumpa zawadi ya send off mara kutumia wazazi wake utajiongezea maumivi na vikao visio kua na tija bure, achana nae kwasababu unako elekea nikubaya kuliko hata hayo.

Mme ukiamua kuoa nikama kujilipua tu, hao wa Dudu ni hatari sanaa kwanza ukiamua kumuoa anakuona kama falaa, anathamini wele wanao mhoja na kukimbia kama wajanja wake kuliko wewe anae jitoa kumuoa. watakutesa tu mbeleni wengi wako hivo.
 

Kwisense

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
375
1,000
Ushauri wangu, naomba umtumie screen shot hizo kwanza usikie reaction yake, usitume kwa wazazi wake. Mtumie yeye mwenyewe kwanza, baadae shirikisha wazazi wa pande if possible ili kumaliza urafiki kwa amani na bila kinyongo cha wazazi wako/wake.

Kwa kweli Mungu asimame kati ili utoke salama mkuu, maana hayo ni maumivu makali sana na unahitaji busara na akili zaidi kuepuka kwenda rumande. Jitahidi sana kuendelea na uvumilivu uliouonesha maana "Hasira Hasara", unaweza kutumia nguvu kubwa ukavuruga maisha yako yote duniani, vuta subira, tumia hekima, busara na utu kutatua hiyo changamoto.
 

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,070
2,000
Ushauri wangu, naomba umtumie screen shot hizo kwanza usikie reaction yake, usitume kwa wazazi wake. Mtumie yeye mwenyewe kwanza, baadae shirikisha wazazi wa pande if possible ili kumaliza urafiki kwa amani na bila kinyongo cha wazazi wako/wake.
Kwa kweli Mungu asimame kati ili utoke salama mkuu, maana hayo ni maumivu makali sana na unahitaji busara na akili zaidi kuepuka kwenda rumande. Jitahidi sana kuendelea na uvumilivu uliouonesha maana "Hasira Hasara", unaweza kutumia nguvu kubwa ukavuruga maisha yako yote duniani, vuta subira, tumia hekima, busara na utu kutatua hiyo changamoto.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Ahsante sana mkuu.
 

Watery

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
1,877
2,000
Mwenzako Koroe hatumuoni, sijui alipotezwa, anyways subir atangaze sana kuwa anaolewa af mwisho wa siku mbwage siku chache kabla ya sendoff, mfanye ajutie kukusalit maana hawa wanawake, ukimbwaga acha fununu zisambae kwann ulimuacha otherwise yanaweza kukurudia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom