Mchumba wangu hataki nishike simu yake kusoma meseji, kanikwapua simu yake na kunipigia kelele mbele za watu

kabwinyola

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
560
678
Kumekucha salama

Kama ninavyosema, nina mchumba wangu ambaye tumekuwa wote kwenye uchumba Kwa miaka 4 sasa lakini pamoja na kwamba tumepanga tuoane baadae lakini tuneshakuwa kama mke na mme japo anakaa kwao nani nakaa kwetu,

Juzi nimeenda dukani kwake biashara nimemfungulia mimi, kwa ziara ya kushtukiza nikashika simu yake niliyomnunilia mimi na kuanza kuikagua hakupenda eti naomba simu yangu akakasirika saana mpaka ikabidi nimpe simu nikakaa kimya akaanza kujiongelesha ooo unajua kusamehe kama nimekuudhi.

Maana we una wivu najua ukikuta hata meseji ya kawaida uta kasirika, nikakaaa kimya sikuongea, akaendelea oooo unajua ngoja nikununulie zawadi nikakausha, akasema ooo nikuagizie chakula nikagoma.

Baada ya kuwaza sana tukio hilo najiuliza kuna nini hasa maana alivoruka na kuchukua simu ?
 
Ukanuna ukishika simu ya mpenzio hata kama huna minajili yakuikagua akaanza kuikwapua kwa nguvu shtuka
 
Sasa mkuu mpaka hapo unahitaji msaada gani? manake wewe ndio ulie ona reaction yake ulipo chukua simu,wewe ndio umenunaa,wewe ndio ulie bembelezwa mpaka unataka kununuliwa zawadi,bado unauliza kuna nini? hakuna kitu nna imani ni mke wako mtarajiwa since mko wote 4yrs inatosha kujua unaishi na kiumbe wa aina gani,sasabasi kama bado unampenda msamehe na mwambie asikufanyie hivyo weye moyo wako hauchukui tafran,na jengine mkuu kwani ulikua unatafuta nini kwenye simu yake? utakuja kujikuta Hospital bure kuna vitu vyengine achana navyo kabisaaaa...
 
Back
Top Bottom