Nimegundua mchumba wangu kanisaliti baada ya kuona meseji za mapenzi kwenye simu yake

Habari za asubuhi wakuu. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani.

Wakuu bila kupoteza muda ni kwamba leo asubuhi nikiwa tumelala, mpenzi wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa tano aliniomba nimsaidie kutengeneza simu yake kwa sababu ilikuwa na matatizo katika upande wa WHATSAPP.

Katika kuitengeneza nimekutana na meseji mbaya sana ambazo zilisababisha nitetemeke mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kiukweli nimejikaza kama mwanaume ili asigundue chochote.

Nikawa nimepiga picha zile meseji kwa camera ya mbele(screenshot) na kujitumia. Ni meseji ambazo zinaonesha few days ago alikuwa guest House na mwanaume. So yule mwanaume alikuwa anaomba wakutane tena pamoja na anakumbushia walivyofanya siku hiyo na kumsifia shemeji yenu kuwa anajua mambo sana.

Kwa muktadha huo hapo juu wakuu. Nipo nae hapa ndani natamani nimmalize kabisa ila roho inasita ingawa hajui kama nishajua usaliti alioufanya. Kiukweli imefikia muda nafsi yangu haitaki kumuona kabisa. Tangu saa tatu nipo tu nimelala naugulia maumivu wakuu.

Je nimpe taarifa au nisubiri mpaka siku ya send off yake nije nimuwekee zile picha za screenshot kama zawadi yake na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu na uchumba wetu?

Je nimtumie meseji hizi ili ajue kwamba nimegundua uchafu wake au nizitume kwa wazazi wake ili wajue matendo machafu ya mtoto wao?

Naomba tupeane uzoefu na mawazo wakuu. Najua wapo ambao watakuja kunikejeli ila it hurts a lot when you do really love someone halafu ana-cheat.

Ahsanteni na karibuni kwa ushauri pamoja na michango yenu wakuu maana nipo katika njia panda japo bado nipo imara sana.
Pole sana,
Watumie wazazi wake,wazazi wako,yeye na marafiki zake hapo muache sasa..hapo utakuwa umejisafisha kabisa
 
Ila kama unampenda sanaaaa muulize tu?akikiri na kuomba msamaha msamehe na maisha yaendelee
 
Mwenzako Koroe hatumuoni, sijui alipotezwa, anyways subir atangaze sana kuwa anaolewa af mwisho wa siku mbwage siku chache kabla ya sendoff, mfanye ajutie kukusalit maana hawa wanawake, ukimbwaga acha fununu zisambae kwann ulimuacha otherwise yanaweza kukurudia
Anajiua halafu unakamatwa kwa kuua bila kukusudia kesi miaka 20 upo mahabusu ukisubiri msamaha wa rais..mimi naona asifike hiyo stage
 
Pole bro, Unakosajee usingizi kwa sababu ya mtu ambaye muda huo yeye amelala usingizi na wala hana hata wazo Moja kuhsu wewe, Piga chini ibaki story, ni vyema uwe imara na kumruhusu aende lakini usisahau kuwa na busara za kumsubilia yule anayesitahili kuwa naye
 
Hii ni kweli ama ni story tu mkuu,? Pole ila huyo dada si hata angefuta hizo sms jamani na pia kama umeamua kua kwenye serious relationship na mnatarajia ndoa hayo mambo mengine angeachana nayo tu ona sasa kinachoenda kutokea🙄

Nakushauri usiwatumie wazazi jaribu kumuonesha na uone atajitetea vipi? Huenda ni rafiki yake katumia simu yake kuwasiliana na huyo mkaka(kama impossible hivi🤔) ila ongea naye huenda majibu yake yakakutuliza jazba kidogo mkuu
Kwahio akifuta anakuwa sio msaliti 😅 hebu mtulizege hivyo vinena jamani mkiwa katika mahusiano serious!

We mtu anakutunza anakufanyia kila kitu still unagawa tobo mafichoni!? Huu umalaya wa kishamba una gharama sana! Kama unaona hakuridhishi kitandani mwambie apige hata lemba ili shughuli ifane sio kusaliti! Aibu sana kwa mwanamke kuwa malaya 😀😀😀
 
Mchane tu mapema ili harakati zote za mipango ya ndoa zisitishwe maana kuja kutuchangisha halafu siku kadhaa tumeshajiandaa kuja kula bufee tusikie mambo yamebumburuka kwakweli tutalaumu sana michango yetu tuliyotoa.
Wahuni wanachangia mchango wa bufee na MC kutuburudisha huku tukinywa wine taratibu halafu mwamba aharibu shughuli mwishoni? Kwanza atawaumiza sana wazazi wa binti na binti mwenyewe 😂😂😃😃😂
 
Kwahio akifuta anakuwa sio msaliti 😅 hebu mtulizege hivyo vinena jamani mkiwa katika mahusiano serious!

We mtu anakutunza anakufanyia kila kitu still unagawa tobo mafichoni!? Huu umalaya wa kishamba una gharama sana! Kama unaona hakuridhishi kitandani mwambie apige hata lemba ili shughuli ifane sio kusaliti! Aibu sana kwa mwanamke kuwa malaya 😀😀😀
Sawa siyo vizuri kwakweli alichokifanya huyo dada, na wala simtetei ila atleast angefuta inapunguza maumivu kwa mwenzake.
Hivi lemba ni nini?
 
Pole na katusi juu babe wangu😂, i can imagine ungekua ni wewe imekutokea hivo sijui huyo dada angekua na hali gani sahivi🙌
Kama ushashuhudia pambano la Tyson na Holyfield lilimalizika Tyson akiwa na hali gani basi ndio namna ambavyo ningem design huyo bitch 😂😂😂 nankibuti juu!

Angechagua kusuka au kufuga rasta!
 
Kama ushashuhudia pambano la Tyson na Holyfield lilimalizika Tyson akiwa na hali gani basi ndio namna ambavyo ningem design huyo bitch 😂😂😂 nankibuti juu!

Angechagua kusuka au kufuga rasta!
Basi msamehe tu, na huenda ungemsamehe na usingemuacha, usichezee nguvu ya mapenzi mkuu. Ungebaki mdogooo😀😀
 
Khaa unanitisha na nnavoogopa kudundwa, naweza kuomba msamaha usiku kucha babe😀😀
Asa kama unaogopa kudundwa kwanini usaliti! Ukiwa muoga unatulizana tulii unaacha mapepe yote 🤣! Af msamaha hausaidii kama kuna mtu alishakuzama ile picha tayari itabakia kichwani mwangu kuwa jamaa nae ulimfanyia unayonifanyiaga sirini
 
Aisee ila hadi mtu anasaliti nadhani kunakua na sababu hawezi tu akaanza kusaliti na mko vizuri tu, tena mfano wewe unavojidai mkali hivo na labda hujali, aarh akipata mtu mwingine akamuonesha kujali basi hicho tu kinatosha kusaliti. Si nzuri ila kila mtu aplay vizuri part yake kwenye mahusiano masalitiano yatapungua.
 
Hahahahah kwahio mi sijali bebe😂😂😂 hebu acha zako bana!!!
 
Back
Top Bottom