Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Kupika ni Sanaa ukiiwezea hiyo Sanaa hutokinai.
Simple recipe.
Ndizi chemsha na chumvi tu.
Kuku au nyama yoyote
Mchemshe na vitunguu. Akiiva badala ya kuunga.
Saga kitunguu kimoja
Kata kitunguu kimoja
Kwangua karot moja
Hoho moja nzima
Weka vyote na pilipili acha vichemke mpaka viive.
Mchicha chnganya na Chinese.
Katakata
Hoho
Karoti
Kitunguu
Baada ya hapo kamulia limao au ndimu chnganya vyote pika.
Pakua msosi wako halafu nipe mrejesho.
Sijawahi kujaribu hii. Let me try
 
Shida unafosi kupika wewe ndiyo maana unakinai .
Mimi yule mama wa mgahawa ninapokula uwa haniangushi nikimpigia kuwa mbona leo sina hamu na vyakula kabisa anasema njoo utakuta pishi jipya .

Pishi jipya sasa utakuta wali na maziwa ya mgando alafu mchicha umechemshwa supu bila kuwekewa chochote ,natamani nizile nisile ila ndiyo vile mnyakyusa wa watu anakuwa amebuni pishi jipya mteja wake nisipeperuke
 
Fanya uoe sasa Daktari,awe anakupikia pia. Umekosa mtoto mzuri wa kuoa hapo Mbeya?
 
Nafikiri ni mapishi ndio changamoto, wengi wetu TZ asilimia kubwa vyakula ni hivyo ulivyotaja lakini wengine (wachache) hupika tofauti, nyama ni ya ng'ombe lakini upikaji unaweza ukawa tofauti na ukapata kitu chenye ladha, ukiwa na mke anayejiongeza na mwenye exposure kidogo basi utafurahi, kuna siku unapikiwa vitu hata huvielewi lakini ukila vina make sense na viko healthy.
 
Back
Top Bottom