Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Aina za upishi ni nyingi sanaaa unaweza pika kiazi mviringo kwa namna ya kipekee na usichoke kula....ni vile tumezoea mapishi ya mazoea.

Ila tuuuuu mapishi masotojo yanahitaji muda na pesa.
Huyu dada kamaliza kila kitu. Ni mapishi tu.
Cha kukusaidia hapo fanya mpango jitwishe huyu mdada. Utanishukuru kesho
 
Kila siku nimekuwa nikila vitu kwenye mzunguko uleule

Wali
Pilau
Nyama za ng'ombe na kitimoto (za kukaanga, kuchoma & kuungwa na nyanya)
Samaki (kuunga na nyanya & wa kukaanga)
Mayai (kukaanga na kuchemsha)
Tambi
Mboga za majani za kuunga na nyanya
Dagaa (same, kukaanga na kuunga)
Kuku (wa kukaanga & kuunga)
Chapati
Supu ya kuku au ng'ombe
Maandazi
Chips (kavu na zege)
Ndizi za kupikwa
Viazi vitamu & mviringo (style yoyote ile ya kupika. Na kadhalika

Sasa nakula vyakula hivihivi kila siku, hivi karibuni kila nikisikia njaa naanza kuwaza nile nini, vitu vilevile tu kila siku.
Nikaanza kujaribu kusearch vyakula vya Asia huko nianze kupika nijaribu vitu tofauti. Kila nikisearch nikianza kuangalia video za mapishi yao naona wanataja ingredients nyingi ambazo hata sijui pa kuzipata

Hivi ukitoa hivi vyakula common kama nilivyovitaja hapo juu, vyakula gani vingine huwa unapika/kula ukiwa home? Nataka nianze kula vitu vingine hata kwa miezi miwili mfululizo
Njoo Lushoto msimu wa mavuno ukaangiwe ngeda, halafu ule na bada.
 
SI upo mbeya msimu wa viazi vitamu huu, pika kifuge maharage unachanganya na viazi afu pondaponda, pia Kuna kisyesye hiki twanga mahindi mabichi funga kwenye jani la mgomba afu chemsha ni kitamu haswa
 
Wali upo wa aina nyingi, pika pilau la viungo vya kawaida au viungo vizima, pika wali mafua, pika wali wa mbogamboga, pika mandi ya wahindi hii ni ya vitunguu vingi mboga yake mayai ya kuchemsha, pika biriyani kazi kwisha
 
Tuje kwenye ugali badili aina mbalimbali za ugali tengeneza Dona lako weka muhogo mkavu, mahindi ya njano, mtama, au tengeneza unga wa mahindi ya kuloweka
 
Back
Top Bottom