Nimechoka kula vyakula vilevile kila siku

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
7,595
Reaction score
15,506
Kila siku nimekuwa nikila vitu kwenye mzunguko uleule

Wali
Pilau
Nyama za ng'ombe na kitimoto (za kukaanga, kuchoma & kuungwa na nyanya)
Samaki (kuunga na nyanya & wa kukaanga)
Mayai (kukaanga na kuchemsha)
Tambi
Mboga za majani za kuunga na nyanya
Dagaa (same, kukaanga na kuunga)
Kuku (wa kukaanga & kuunga)
Chapati
Supu ya kuku au ng'ombe
Maandazi
Chips (kavu na zege)
Ndizi za kupikwa
Viazi vitamu & mviringo (style yoyote ile ya kupika. Na kadhalika

Sasa nakula vyakula hivihivi kila siku, hivi karibuni kila nikisikia njaa naanza kuwaza nile nini, vitu vilevile tu kila siku.
Nikaanza kujaribu kusearch vyakula vya Asia huko nianze kupika nijaribu vitu tofauti. Kila nikisearch nikianza kuangalia video za mapishi yao naona wanataja ingredients nyingi ambazo hata sijui pa kuzipata

Hivi ukitoa hivi vyakula common kama nilivyovitaja hapo juu, vyakula gani vingine huwa unapika/kula ukiwa home? Nataka nianze kula vitu vingine hata kwa miezi miwili mfululizo
 
jaribu Supu ya Nyoka
 
Sijaona.. mashed potatoes, macaroni, oats, cornflex, bokoboko. Hizo ndizi hujasema ni zipi, kuna aina nyingi za ndizi
Kwanza hivi vyakula vya majina ya kizungu ulivyotaja imebidi nikavi google kwanza. Hapo nilielewa tu hiyo mashed potatoes ambayo sijala sana, ngoja nianze kula.
Ila hii corn flakes nimesearch hata sijakielewa binafsi
Pia ndizi nakula za kukaanga, ku roast kawaida na mtori. Katika hizi tatu, ni mtori pekee sijachoka kula
 
Aina za upishi ni nyingi sanaaa unaweza pika kiazi mviringo kwa namna ya kipekee na usichoke kula....ni vile tumezoea mapishi ya mazoea.

Ila tuuuuu mapishi masotojo yanahitaji muda na pesa.
Hapa ni sahihi. Huenda najua aina chache za mapishi ndio maana. Inabidi nispend time kusearch mapishi ya aina tofauti tofauti ni enjoy na mimi
 
Kwanza hivi vyakula vya majina ya kizungu ulivyotaja imebidi nikavi google kwanza. Hapo nilielewa tu hiyo mashed potatoes ambayo sijala sana, ngoja nianze kula.
Ila hii corn flakes nimesearch hata sijakielewa binafsi
Pia ndizi nakula za kukaanga, ku roast kawaida na mtori. Katika hizi tatu, ni mtori pekee sijachoka kula
Corn flakes unanunua.. unachemsha maziwa fresh, unaweka kwa kibakuli afu unaweka vijiko kadhaa vya hiyo cornflakes mlo tayari

Nimemaanisha hizo ndizi ni bukoba, mshale, au mzuzu?
 
Back
Top Bottom