Léo tuko hapa
Léo tupo hapa

Sukari iko nyingi
Sukari ipo nyingi

Léo TUKO hapa,tutakunywa sana chai kwa vile Sukari IKO nyingi.
Léo TUPO hapa,tutalewa tutakavyo Sababu Pesa IPO nyingi.

Nadhani IPO na TUPO Ina Sound POA
Tumia IPO na TUPO,ukiwa hapa Tanzania
Tumia TUPO na IKO ukiwa kwa majirani zetu Wakenya.
 
Viambishi vya mahali (locative suffix) "ko, po, mo"

Ko - general (ujumla)
Kiaambishi hiki hutumika unapoongelea mahali kitu/mtu alipo kwa ujumla (general).
Mfano: Niko Dar es salaam (Dar es salaam ni kubwa na haifafanui upo Dar es salaam sehemu gani)
Pia kiambishi -ko kinatumika unapouliza kujua kitu/mtu mahali aliko.
Mfano: Mwanafunzi yuko wapi.?

Po - Specific (bayana)
Kiambishi hiki hutumika kuelezea bayana kitu/mtu alipo.
Mfano: Nipo Kinondoni
Yupo Makumbusho

Mo - Inside (ndani ya..)
Kiambishi hiki hutumika kuelezea kitu/mtu akiwa ndani ya (mahali)
Mfano: Nimo chumbani
Nyoka yumo shimoni.

Zingatia: Viambishi hivi kwa watumiaji wa lugha (Kiswahili) huwa wanavichanganya katika matumizi lakini sentensi huleta maana japo inakuwa na makosa kisarufi.

##Nimejaribu kuelezea japo si mzuri sana kwenye kuandika, wengine wanaweza kuongezea.
Asante.##
 
Léo tuko hapa
Léo tupo hapa

Sukari iko nyingi
Sukari ipo nyingi

Léo TUKO hapa,tutakunywa sana chai kwa vile Sukari IKO nyingi.
Léo TUPO hapa,tutalewa tutakavyo Sababu Pesa IPO nyingi.

Nadhani IPO na TUPO Ina Sound POA
Tumia IPO na TUPO,ukiwa hapa Tanzania
Tumia TUPO na IKO ukiwa kwa majirani zetu Wakenya.
Sawa sasa ni wakati gani wa kutumia iko na ipo?
 
Ipo maana yake ni hapa hapa, yaani ukisema sukari ipo ni kwamba ipo hapa hapa na
Iko ni kwamba sehemu nyingine yaani sukari iko, ila ni mpaka godown au store
Upo?
Sasa tujaribu hapa chini

"Upo hapo ulipo upo"? Atakaeweza kutafsiri
hapa nampa maua yake
Nimekuelewa kuwa iko ni kwa vitu vilivyo mbali na ipo vilivyopo karibu

Vipi kuhusu tuko na tupo?
 
Ko - general (ujumla)
Kiaambishi hiki hutumika unapoongelea mahali kitu/mtu alipo kwa ujumla (general).
Mfano: Niko Dar es salaam (Dar es salaam ni kubwa na haifafanui upo Dar es salaam sehemu gani)
Pia kiambishi -ko kinatumika unapouliza kujua kitu/mtu mahali aliko.
Mfano: Mwanafunzi yuko wapi.?

Po - Specific (bayana)
Kiambishi hiki hutumika kuelezea bayana kitu/mtu alipo.
Mfano: Nipo Kinondoni
Yupo Makumbusho
Nimekusoma

Kwa hiyo nitakuwa sahihi kusema kwa mfano: kwa sasa niko Dar es Salaam ila nipo Tegeta kimakazi
 
Ipo maana yake ni hapa hapa, yaani ukisema sukari ipo ni kwamba ipo hapa hapa na
Iko ni kwamba sehemu nyingine yaani sukari iko, ila ni mpaka godown au store
Upo?
Sasa tujaribu hapa chini

"Upo hapo ulipo upo"? Atakaeweza kutafsiri
hapa nampa maua yake
Ni kama jamaa yako Tu unamuuliza vipi upo shop hapo na je huo mchele upo
 
gari iko poa....ndani gari ipo poa..njee
nyumba ipo poa.... njee nyumba iko poa ndani
hivi ni viambishi vya mahali vikielezea ndani ama nnje....
 
Back
Top Bottom