Wakuu,
Hii sio Chit Chat wala Jokes bali ni The Most painful Day of my life.
Nimechapiwa mke wangu.
Hii ni baada ya kusafiri, mshikaji kapita na mke wangu Usiku wa Mei Mosi.
Wife katoka job, kaenda kumegwa kwa mwana akarudishwa saa nne usiku.
Picha la kwanza simu ilizimwa mda wote nikaja kuambiwa battery inasumbua baada ya show kuisha.
Nilitulia nikajiridhisha kwa 100% ni tukio la kweli, leo nimemwagia ushahidi mezani kabaki kumsingizia shetani.
Kichwa kinauma ila hatimaye nimekubali ndoa ni wizi wa mchana kweupe. Maana hela nilimpa, haki yake alipata, ila itoshe kusema huwezi kumridhisha kiumbe aliezaliwa na mwanadamu.
Imagine mpaka walipanga kununua simu mpya ambayo wangetumia wakiwa kazini tu na ibaki hukohuko.
Hapa sijamtimua bado maana nafikiria namna ya ku transition na mtoto huyu wa kindergarten.
Mama yetu Mlezi Mh.
Dkt. Gwajima D sitakuangusha tumeaswa sana humu ndani sitanyanyua hata mkono wangu aende tu salama kama alivyokuja salama.