TEAM KATAA NDOA – Ulevi wa Ubinafsi Usio na Maono

TEAM KATAA NDOA – Ulevi wa Ubinafsi Usio na Maono

Friji la mtumba

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
277
Reaction score
434
Ni ajabu sana kuona kizazi kinachojiona "kimeamka" kikikumbatia falsafa ya ubachela kana kwamba ni mafanikio ya juu kabisa ya maisha. Team Kataa Ndoa wamechagua njia rahisi ya kuepuka majukumu, wakijificha nyuma ya visingizio vya uhuru, starehe, na "kupambana kivyao."

Je, kweli wana akili timamu au wamekosa dira ya kweli ya maisha?

1. Kuogopa Jukumu si Ukomavu:
Kukataa ndoa si ishara ya uhuru, bali mara nyingi ni hofu ya uwajibikaji. Wanaume waliokomaa wanajua kwamba maisha si ya kujifurahisha tu bali ni ya kujenga kizazi, kuacha urithi na kushiriki maisha na mwenza.

2. Ubinafsi Uliojaa Uvivu:
Maisha ya kujifikiria mwenyewe kila siku si ustaarabu. Ni ubinafsi wa hali ya juu usio na mchango kwa jamii. Hawa watu wanachangia nini zaidi ya memes na misemo ya kujifariji?

3. Heshima Katika Jamii Inatokana na Kujitolea:
Katika jamii nyingi zenye maadili, mtu anayejenga familia huheshimiwa. Mtu anayekataa ndoa ili aendelee "kula maisha" anajichelewesha kimaendeleo na kijamii.

4. Kuoa si Mateso – Ni Ujenzi:
Ndoa si kifungo kama wanavyodai, bali ni taasisi ya mabadiliko na kujifunza. Waliokimbia ndoa kwa sababu ya mitazamo potofu wamekosa neema ya kukua kiakili na kihisia.

---

Hitimisho:
Team Kataa Ndoa sio wapiganaji wa uhuru, bali ni wakimbizi wa majukumu. Badala ya kujificha kwenye kivuli cha memes, wajitathmini: wanaishi kwa maono au kwa mitikiso ya mtandao?
 
Kataa ndoa waleteni hapa mimi niwachomekee chuma kwa aso 😁😡Ozwo
 
Jibu hoja zao mkuu.

1)mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wengi.

2)kuchapiwa kunakotokana na maadili duni.

3)mgawanyo usio sawia wa mali wakati wa talaka.
 
Ndugu Friji la mtumba kitu usichokijua kuhusu KATAA NDOA ni kuwa sisi hatutaki hiyo taasisi kandamizi inayoitwa ndoa ila mambo mengine yote tupo sambamba na nyie.

Kuzaa tutazaa, kulea tutalea na mahusiano tutakuwa nayo ila ndoa ndio kitu hatukitaki kisikia.

Ubinafsi, uvivu na uoga ni tabia binafsi za mtu awe suria au mwanandoa bado anaweza kuwa hivyo. Sasa usihusishe msimamo wetu na tabia binafsi za mtu.
 
Taasisi kandamizi!!?? Aisee kazi ipo
 
Jibu hoja zao mkuu.

1)mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wengi.

2)kuchapiwa kunakotokana na maadili duni.

3)mgawanyo usio sawia wa mali wakati wa talaka.
Aisee tuna kazi kubwa ya kufanya
 
Taasisi kandamizi!!?? Aisee kazi ipo
Embu fikiria mwanaume akioa tu tayari mwanamke ana nafasi ya kuondoka na 30% ya mali zake.

Embu waza, mke anaweza kuchukua mkopo kwa jina la mumewe hata bila kumwambia wala kupewa ruksa yake. Na mwanaume (mume) lazima alipe.

Wanaume wengi waliooa wanakiri kuuva mkenge, ni vile hawaoni nuru kwenye kutalakiana maana watapoteza mali na nguvu zao kwa migawano isiyowazingatia hata kidogo.

Kifupi sana, sheria ya ndoa ni sheria ya kumlinda mwanamke ndani ya ndoa. Na hicho kitu ndio kitu hatukitaki.
 
Kama unakuja kuja kwa mbaaaali🤔
All in all ndoa ni tamu sana
 
Back
Top Bottom