Nimeanza kuziamini ndoto baada ya kuota nipo na Rais Samia kisha nikapata kazi

Achoki

Senior Member
Mar 27, 2013
151
60
Habari za mchana,

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja. Mimi nilihitimu chuo kimoja maarufu hapa nchini mwaka 2015. Tangu mwaka 2015 nlikuwa naishia tu kupata viajira vya kubangaiza bangaiza. Sasa mwaka huu mwezi wa nne tarehe 3 niliota ndoto ambayo nlivyoamka nikaitafakari sana sikupata jibu.

Ni hivi niliota nipo kwenye gari ya serikali tumekaa watu wanne, mimi nimekaa nyuma na mtu ambaye sijamfahamu ila mbele amekaa dereva na Rais Samia, wakati gari inajiandaa kuondoka basi mama Samia aligeuka nyuma na kunipa begi ambalo lilionekana halikufungwa vizuri akanisisitiza nikamate vizuri.

Basi nikalikamata safari ikaendelea hadi tukafika sehemu ambayo kulikuwa kama kuna mkutano, tukashuka yeye akaenda kukaa jukwaani mimi nikaendelea na majukumu mengine huku nikiwa bado ninalo lile begi. Baada ya hapo nikashtuka kutoka usingizini.

Nikawaza sana hii ndoto ina maana gani sikupata jibu, asubuhi nikamshirikisha ndoto hii mzee mmoja hapohapo jirani yetu akanijibu mwaka huu utapokea habari njema sana basi nkasema sawa na iwe hivyo.

Basi baada ya kupita kama wiki, serikali kupitia OR-TAMISEMI ikatangaza ajira za ualimu na afya, nikatazama nikaona kuna nafasi inayonihusu nikaomba.

Nakumbuka ililkuwa tarehe 4 mwezi juni mwaka huu nikaota ndoto tena! ndoto hii nilikuwa nipo juu ya mnara mrefu sana nimejishikilia, wakati nimejishikilia nikamwona tena Rais Samia halafu kwa msisitizo akaniambia maneno yafuatayo "Jishikilie kwa nguvu usianguke na uutunze huu mnara umesikia" nikaitikia ndiyo, baada ya hapo nikashtuka kutoka usingizini.

Tarehe 5 Juni mwaka huu yakatangazwa majina ya watu waliobahatika kupata ajira, nikatazama nikaona jina langu. Hapo ndipo nlipoona ukamilisho wa ndoto yangu.

Kuanzia siku hiyo nimekuwa mtu kuamini ndoto na kuwa makini na ndoto ninazoota.
 
RAIS DR. SAMIAH SULUHU HASSANI, halafu kwa msisitizo akaniambia maneno yafuatayo "jishikilie kwa nguvu usianguke na uutunze huu mnara umesikia" nikaitikia ndiyo,

baada ya hapo nikashtuka kutoka usingizini.

" Siku nyingine ukiwa unamuitikia mama yeyote aliyekuzidi umri na anayestahili heshima ya umama wake, muitikie kwa kusema, "Ndiyo Mama",
 
Habari za mchana,

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja. Mimi nilihitimu chuo kimoja maarufu hapa nchini mwaka 2015. Tangu mwaka 2015 nlikuwa naishia tu kupata viajira vya kubangaiza bangaiza. Sasa mwaka huu mwezi wa nne tarehe 3 niliota ndoto ambayo nlivyoamka nikaitafakari sana sikupata jibu.

Ni hivi niliota nipo kwenye gari ya serikali tumekaa watu wanne, mimi nimekaa nyuma na mtu ambaye sijamfahamu ila mbele amekaa dereva na Rais Samia, wakati gari inajiandaa kuondoka basi mama Samia aligeuka nyuma na kunipa begi ambalo lilionekana halikufungwa vizuri akanisisitiza nikamate vizuri.

Basi nikalikamata safari ikaendelea hadi tukafika sehemu ambayo kulikuwa kama kuna mkutano, tukashuka yeye akaenda kukaa jukwaani mimi nikaendelea na majukumu mengine huku nikiwa bado ninalo lile begi. Baada ya hapo nikashtuka kutoka usingizini.

Nikawaza sana hii ndoto ina maana gani sikupata jibu, asubuhi nikamshirikisha ndoto hii mzee mmoja hapohapo jirani yetu akanijibu mwaka huu utapokea habari njema sana basi nkasema sawa na iwe hivyo.

Basi baada ya kupita kama wiki, serikali kupitia OR-TAMISEMI ikatangaza ajira za ualimu na afya, nikatazama nikaona kuna nafasi inayonihusu nikaomba.

Nakumbuka ililkuwa tarehe 4 mwezi juni mwaka huu nikaota ndoto tena! ndoto hii nilikuwa nipo juu ya mnara mrefu sana nimejishikilia, wakati nimejishikilia nikamwona tena Rais Samia halafu kwa msisitizo akaniambia maneno yafuatayo "Jishikilie kwa nguvu usianguke na uutunze huu mnara umesikia" nikaitikia ndiyo, baada ya hapo nikashtuka kutoka usingizini.

Tarehe 5 Juni mwaka huu yakatangazwa majina ya watu waliobahatika kupata ajira, nikatazama nikaona jina langu. Hapo ndipo nlipoona ukamilisho wa ndoto yangu.

Kuanzia siku hiyo nimekuwa mtu kuamini ndoto na kuwa makini na ndoto ninazoota.
Duhh shukuru Sana mkuu mm nna ndoto inanisumbua na hio ndoto imeshaonesha dalili zote kua itatimia na ni ndoto mbayaa bas aisee
 
Back
Top Bottom