Nimeamini uchawi upo,na nina support kuua wachawi

Nimeamini uchawi upo,na nina support kuua wachawi

kwani binadamu ameacha kuzeeka?shy ukizeeka tuu ushakua mchawi,mimi nililima mpunga kwa misimu 3 maeneo ya Mwamalili,Bubale na Mwankinga,huko hawana tofautiti na Gamboshi,kuna uchawi balaa yaani kila kitu back up yake ni uchawi

kilichonipata nalijuta kuwa mkulima mkubwa???!!!

Mkuu ulipatwa na nini? Hembu funguka basi hata kidogo tupate experience yako!! Au ulivuna gunia 2 kwa hekari 10?
 
Mkuu ulipatwa na nini? Hembu funguka basi hata kidogo tupate experience yako!! Au ulivuna gunia 2 kwa hekari 10?

ha ha ha acha kabisa,kiherehere cha kilimo kwanza kilinitokea puani,nilikua nimejipanga vilivyo life cycle ya project was 3 yrs then nijue what next,mwaka pili kuingia watatu nilikua nahemea machine kiuchumi,option A TO Z zilikwisha,

Mashamba yamestawi kama miwa,mpunga umebeba mpaka umejikunja vuna sasa?

ushasahau nyumbani kwako hata siku moja?shamba nakwenda mara 3 kwa wiki ila kuna kipindi nilishapotea zaidi ya mara 3 mchana peupe,

kwakifupi shamba limezaa njo kwenye kuvuna ndio utasoma habari yako,baadhi ya wenyeji walikua wananiambia kabla ya kuanza msimu natakiwa kufanya yale mambo yao ila hilo lisinipate kwa kusimamia imani yangu kamwe sikufanya hivyo,ina maana kila mtu alikua amezindika shamba lake vilivyo kasoro mimi.so wachawi wote wa hivyo vijiji wakahamia kwangu,

nadhani umepata picha kidogo kwa uchache,mengine ya ajabu ajabu nilikua nayashuhudia kwa macho,ndio maana usukumani mtu ana ngo'mbe 500,gunia 400 cha mpunga ila hana nyumba ya bati ni full tembe,jiulize anaogopa nini?

mtu akiwa mchawi sana wakashindwa kumzibiti kwa aina nyingine ya uchawi ndio wanamfanyia timing ya kumuu mchana peupe,nimejifunza mengi ila fursa zipo sana nitarudi kivingine
 
Ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi tu wanaishi maisha ya wasiwasi wakati wote kwa kudhania wanadhuriwa na wachawi. Nimeshuhudia wengi wenye imani hizo - wanaenda kwa mafundi/waganga ambako wanazidishiwa hofu na pia kuchonganishwa na ndugu/majirani. Ukweli ni kwamba hao mafundi/waganga ulaji wao unategemea hofu hizo za jamii, hivyo lazima wazichochee ili waumini warudi kutafuta mazindiko mara kwa mara!
 
Huo ni mfano tu dogo inaweza kuwa kilo mia sita kwa mia saba sio lazima sita aiseee; nilitaka kuonyesha tu kuwa lazima imani yako iwe juu vya kutosha na ushahidi uwe nao sio iwe imani kuhusu wachawi tu lakini haionekani ikitenda kazi zingine katika maisha yako km. unalala njaa, unaandamwa na magonjwa, migogoro kibao, faraka kwa wingi, nk. imani ni upana wa maisha haisimamii jambo moja

Imani ni mfumo wako wote wa maisha unayoishi, kifupi uwe mcha Mungu kweli na sio mnafiki.. Mtu kama huyu anakwambia yeye ana imani wakati anazini kila siku, anadhulumu watu, anasema uongo ila uchawi tu ndio haamini..

Nashukuru umejitahidi kumuelewesha labda anaweza kuelewa na kubadili mfumo wake wa maisha..
 
Ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi tu wanaishi maisha ya wasiwasi wakati wote kwa kudhania wanadhuriwa na wachawi. Nimeshuhudia wengi wenye imani hizo - wanaenda kwa mafundi/waganga ambako wanazidishiwa hofu na pia kuchonganishwa na ndugu/majirani. Ukweli ni kwamba hao mafundi/waganga ulaji wao unategemea hofu hizo za jamii, hivyo lazima wazichochee ili waumini warudi kutafuta mazindiko mara kwa mara!

Wafanyanyeje sasa? maana hata wachungaji na masheikh huwaambia watu juu ya mapepo/majini yatesayo watu kila siku.
Wachungaji/Masheikh kwenye maombi tunawasikia pia wakikemea roho chafu aka mapepo/majini - TUFANYEJE SASA TOA SULUHU MKUU..
 
Wafanyanyeje sasa? maana hata wachungaji na masheikh huwaambia watu juu ya mapepo/majini yatesayo watu kila siku.
Wachungaji/Masheikh kwenye maombi tunawasikia pia wakikemea roho chafu aka mapepo/majini - TUFANYEJE SASA TOA SULUHU MKUU..
Kuna viongozi wa dini ambao kimsingi hawatofautiani na waganga wa kienyeji katika kuwatisha waamini kuhusu mapepo (mara nyingi ya kufikirika tu) ili wawakamue.

Utaambiwa ulete sadaka zaidi ili wajikite kukuombea! Yatapigwa makelele utadhani Mungu ni kiziwi! Wana ushawishi mkubwa - hivyo wengi huwaamini na kutoa pesa a.k.a sadaka kubwa na mara nyingi.

Hakuna njia rahisi ya kuepukana na mambo haya iwapo umeshatumbukia tayari katika imani hizo potofu.

Kinga ni bora zaidi kwa mfumo wa wazazi (iwapo hawajaathirika) kuwalea vema watoto katika mambo haya. Watoto waelezwe kuhusu utapeli wa waganga/mafundi wa kienyeji na pia wa wachungaji feki. Wakue wakiaminishwa kwamba mapepo mengi ni ya kufikirika tu, na kwamba inatosha kumwomba Mungu wewe mwenyewe kwa imani ukapata ulinzi tosha. Waone kwamba ninyi wazazi hamjihangaishi kamwe na mabaazazi hawa na bado mnadunda vema.
 
Jibu pekee watalipata Kwa Yesu yeye ndio kiboko ya wachawi. Kwa jina lake Yesu, wachawi hukimbia kama wafilisti walivyowakimbia waisraeli baada ya Goliath kuuawa.
 
Hiyo tunaita Traditional Means of Solving Disputes..
 
Kwani ao wasukuma awawez kuishi bila kulogana? Mbona wanatesana wakati wao still ni ndugu na maisha ni mafupi sana duniani?
 
wakati niko kidato cha sita kuna mganga wake akanifata akaniambia maneno flan indirect ambayo nimechukua muda sana kuja kumwelewa alikua na maana gani, jamaa yule ilikua njaa tu inamsumbua bt nadhani hakupenda kabisa yule mama anachawafanyia ndugu zake, na pia hutumii akili nyingi kumtambua mchawi as long as uwe na akili timamu.
Alikwambia Maneno gani?
 
Yaani kama kuna sehemu wa -Afrika tunafeli, basi ni kwenye kuamini ushirikina.

Masikini mimi, sio kwa ndugu upande wa Baba wala upande wa mama, kuna wachawi wa wazi wazi, lkn kitaeleweka tu.
 
sijakuelewa
...hata mimi sijamuelewa. Nafikiri alikuwa na haraka ya kutujulisha kuhusu siri ya Biblia hadi akachanganya mambo!
Rudia tena Mkuu, kwa taratiibu...ili watu wakuelewe...!
 
Kuna familia moja huku vijiji vyetu vya Shinyanga,Bukombe imepata tatizo.Alianza mama wa familia kuugua vitu visivyojulikana kila akifanya medical checkups hapatwi na kitu,akapewa rufaa tu Bugando,kule hali ikawa vilevile but mum is serious sick,amekaa Bugando kama mwezi hv,madaktari kupima tena wakamkuta na uvimbe tumboni,issue inakuja kuwa ngumu,kila wakitaka kufanya operation,vpmo vinaonesha hana damu na maji,saiv ni mwezi wa tatu yuko serious kitandan,Kuna ukweli pia huyu mama alikorofishana na kufokeana na dada wa mumewe yaani wifi ake.

Sasa kuna mtoto wa huyu mama mgonjwa ambae anasoma kidato cha nne aliumizwa sana na mateso anayopata mama ake akachukua uamuzi wa kuandika kama barua kwa wale amewataja kwenye hiyo barua kuwa ni wachawi na wamemroga mama ake, yaan anamshutumu shangazi ake sasa,aliandika pia kuwapa onyo kuwa mama ake apone la sivyo kibaya kitatokea,akabandika hyo barua sehemu kama nne hv humo kijijin,basi ikawa gumzo,zile barua zikatolewa na kupelekwa ofis ya mtendaj kwa sababu zilikua na vitisho.

Huyo dogo akakamatwa baada ya wale walioshutumiwa kumshtak ofis ya kata,lakin kwa vile hao watu ni kweli wanajulikana kuwa ni wachaw mtendaji aliendesha kesi kisela na kumwachia dogo.Baada ya kuachiwa wale watu pa1 na shangaz yake walmuibukia nyumban na kumuonya kuwa atakoma,yeye atatangulia kabla ya mama ake, kesho yake dogo anaenda shule alipokaribia xul akaanguka akafa.

Na baada ya mazishi dogo amekua akija kwao usiku akiwa amejifunika sanda aliyozikiwa,Jamani nimeamini uchawi upo,saiv imepita kama siku 5 toka azikwe na leo ilikua graduu yake na huku mama pia haongei leo siku ya pili,ndo alikua mvulana pekee home.
.....
.....Mwana Shybush Mkuu za masiku
 
mwasyoke ndg yangu, uchawi ulioko kwa ndugu hata useme huamini au usiamini unaweza kukudhuru, hasa kama hufaham chochote kua huyo ndugu yako anaweza kukufanyia ubaya wa kiwango hicho. Ila jina la yesu litabaki kusimama, mungu huwa ana revenge na wachawi kabla hawajafa. namshukuru mungu kwa hilo.
Hawezi mtu kuniloga - anaweza kunifanyia mabaya kivingine mfano kunipiga, nk, sio kuniloga. Silogeki kwa vile sina imani wala sitishiki kabisa na mambo ya kulogana.
 
Back
Top Bottom