Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Mungu amponye. Very sad. Moja yabkitu kinaniumiza ni kuona mtu ana matatizo na halafu sina uwezo wa kumsaidia atike kwenye hiyo shida..na hasa shida zisizohusu pesa maana matatizo yanayohusisha ujitaji wa pesa binafsi huwa naona kama sio issue critical
 
Labda unifundishe kuhusu ndugu zenu katika imaan (majini)
 
Nigawie vijiti vya sumu mkuu. Nitupie hata kimoja. Ilivyo navyo ni vingi huwezi kumaliza.
 
Arsis Tungependa kupata ufafanuzi kuwa hapa unajibu maswali yanayohusu kujua tu jambo (Elimu/Kujifunza)

Lakini kwa wenye shida/matatizo kama mimi na wengine ambao tumeuliza hapa namna ya kupata msaada sijaona yoyote akijibiwa.

Ufafanuzi tafadhali.
 
Bado unatolea mifano kwenye dini hizohizo za kuletewa! Umeambiwa kabla ya kuja hizo dini hakukuwa na habari za majini ila mizimu ya wazee tu na mambo yalienda...hizo dini zenu ndo zimetuletea majini.
Hivi unajua kwamba majini walikiwepo kabla ya ujio wa mwanadamu?

Ujue mwanadamu ndio kiumbe wa mwisho kabisa hapa duniani,yaan hata sisimizi ni wenyeji kuliko sisi

Kwenye hiyo mizimu yenu huko kwenye miti mikubwa na mapango ndio na majini yanapatikana huko huko
 
Imebidi nicheke. Mbona naona wengi sana wanaokwenda kutoa mapepo ni kwenye mikusanyiko ya Wakrsto kuliko misikitini? Sijaona misikiti ikatoa mapepo au majini. labda naingia misikiti sio?
Simba.
Hii comment nimeipenda sana,kama kukiri Yesu ni mwokozi na kumuamini,ingetosha kwa majini kutowaingia wakristo kabisa kwakuwa wanalimdwa na damu ya yesu,ila kinyume chake wao ndio wana majini balaa
 
Nimekuelewa sana, utapata majibu. Usiwe na shaka,
Simba.
Simba nami nimeuliza huko awali sijapata majibu. Nina changamoto ya mke wangu kutopata ujauzito. Kwa maelezo yake hajawahi kubeba mimba na anakimbilia miaka 38. Kitabibu wanasema kuzaa/kubeba mimba ni afya. Mifumo yake kwa mujibu wa vipimo iko sawa kabisa na hedhi anapata kawaida. Binafsi nina mtoto (ni wangu).
Sasa nauliza tiba ya hii changamoto. Tiba ambayo ni ya kibinadamu ili hata mtoto akakayezaliwa awe na ubinadamu %100. Najua ni changamoto ya wanawake wengi na ndoa nyingi
Majawabu tafadhali
 
Elezea ulivyofundishwa na Arsis kuhusu aina za binadam
 
Arsis anasema hakuna chalenji humu, kunapooza.
Simba.
Hakuna challenge wapi? Yeye haoni au hana macho.. mbona kuna watu wanauliza hawajibiwi. Kuna member kauliza ili apate usaidizi, jambo lake linahusu baba yake ambaye ni mgonjwa.

Mwingine kaweka na picha ya mmea kakuuliza wewe ili na wewe umuulize Arsis lakini wote wewe na huyo Arsis hamtoi majibu.. namna hii huu uzi unakuwa wa hovyo.

Sawa wewe huwezi kujibu and what about Arsis. Kingine jaribu kuwa na mtiririko mzuri, hujatolea ufafanuzi hili mara umerukia lingine hujamaliza hili umeenda kwingine. Uzi unakosa flow nzuri, endelea kuboresha uandishi makosa ya herufi ni mengi hadi mantiki inapotea.
 
hoja yako nzuri sana lakini sio salama maana usisahau kuna watumia fursa humu bila shaka wataanzisha biashara ya kuuza hizo dawa au hata kufungua ofisi za uganga kisa kajua mitishamba miwili mitatu..wabongo noma unawajua
 
Labda unifundishe kuhusu ndugu zenu katika imaan (majini)
Sawa ngoja nikufundishe kuhusu majini, Hawa ni viumbe wa mungu katika quran wameitwa majini na katika biblia wameitwa mapepo wanaweza kuwa wabaya au wazuri kama tulivyo binadamu wakiwa wabaya sisi waislamu tunawaitwa mashayatwin kama vile binadamu akiwa mbaya ataitwa shetani kwa hiyo shetani ni sifa ya kiumbe kibaya aweza kuwa binadamu au jinn ndio maana katika biblia Imeeleza katika MARKO 1:23 Inasema "Na mara palikuwa ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu akapaza sauti"
Sasa swali kwako biblia inavyosema pepo mchafu kwani kuna pepo msafi? jibu baki nalo, Ngoja niendelee kukupa elimu bwana kanali mjivuni usiependa ukweli au wewe ni mwanga nini?
Unamjua Mariam magdalena ? huenda humjui maana wewe ata biblia inaonekana husomi, Mariam magdalena huyu alikuwa ni mmoja wa wanawake wa karibu na yesu na alikuwa mfuasi wake mwaminifu sasa kivipi mfuasi mwaminifu na yesu aingiwe na pepo kama ilivyoandikwa katika MARKO 16:9
inasema "Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu magdalena , ambaye kwamba alimtoa pepo saba"
Hapo utaona ata watu wa karibu na yesu walikumbwa na pepo je kipindi hicho muhammad alikuwa kaja duniani mpaka useme uislamu na majini ni ndugu? jibu ni hapana sasa kama hapana hawa pepo walikuwa wanaushirika na kina nani hali ya kuwa uislamu haukuwepo jibu baki nalo pia.
Mwisho nikurudishe katika Mambo ya Nyakati wa pili hapo kuna kisa cha Mikaya mwana wa imla na Yehoshafati mfalme wa yuda kuwa makini hapa uchote elimu bure bwana kanali sawa?
Katika kisa hiki Mfalme Ahad wa israeli alitaka kujua kama atashinda vita dhidi ya Remoth-gileadi hivyo akataka manabii wamwambie kama ataweza shinda manabii wakasema ndio atashinda, Lakini Yehoshafati akasema yupo nabii wa kweli ambaye ndie Mikaya tumsikilize nayeye mikaya atasemaje.
Sikiliza majibu ya mikaya sasa, Katika nyakati wa pili yaani 2 Mambo ya nyakati 18:20-22 Inasema"
Akatoka pepo akasimama mbele za bwana, akasema mimi nitamdanganya, bwana akamwambia jinsi gani?akasema nitaondoka nakuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote,bwana akasema ondoka ukafanye hivyo, Basi sasa angalia bwana pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa, naye bwana amenena mabaya juu yako"

Sasa bwana kanali huyo pepo aliesema ataenda kuwa pepo wa uongo kwani kuna pepo wa ukweli? alafu ujue huyo pepo alikuwa mbele za BWANA yaani mungu alikusanya mapepo akayatuma ili wakamdangaje mfalme wa izraeli kupitia kinywa cha manabii wake huyo mFalme sijui unaelewa au mada imeanza kuwa ngumu kwako.?
Kwakifupi ni kuwa huyo pepo alienda kwenye kinywa cha manabii kwa amri ya mungu hiyo inaonesha pepo ni viumbe wa mungu wanaweza kuwa wabaya au wazuri ndio maana huyo pepo apo anasema yeye ataenda kuwa pepo wa uongo that means wapo wakweli. Are we travelling in the same boat?
 
Boss, umenifurahisha sana kwa masomo mazuri sana

Wakristo wengi huwa hamsomi biblia kabisa,au huwa mnapenda vifungu vyenu pendwa lkn mengi hamyajui kuhusu ukristo wenu,ona sasa mnavyoumbuka

Kutwa kushadadia waislamu wana majini mara majini na waislamu ni damu damu,haya aibu yenu hiyo

Kabla ya kuzungumza fanya utafiti kwanza
 
Dah hatari Sana, kwa hiyo huwez kufafanua kwa faida ya wengi.
 
Asante mkuu
kuna maswali niliuliza kuhusu utatu mtakatifu hapa sijapata aliyejibu hata mmoja yaani wakristo wanapenda mambo mepesi mepesi tu ukienda deep kidogo tu juu ya imani yao wanakwepa.
ety wakristo Mbona sisi waislamu mnatusimanga tunafuga majini lakini tupo hapa na tunawajibu tu, Muda mwingine Arsis anaongea mambo yanyopingana na quran lakini tunamsikiliza huenda katika maneno yake ukapata faida.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…