Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Huu uzi Kila ukipiga Chabo 30 pipo are hiya.
Watu kumbe tunapenda majini kiasi hiki.

Arsis anavutia sana story zake.

Nasubiri wasomi wamuulize maswali ya kisomi, ya ya chalenji ndio tutastarehe.

Arsis amewahi kusema elimu yake ataeizingatia, kila "topic" ni Phd.

Usiniulize kamaanisha nini. Sielewi.
Simba.
 
Inatokea post namba 64.

Tukala na wnafunzi wa babu, baada yta kumaliza kula mmoja akasema vipi, mshikaji, sisi tunaelekea kijijini kwenye vishughuli vyetu, sisi hatuna mwiko wa kuondoka hapa. Nikawaambia poa. Wakaondoka na vyombo vingine, wakaniwachia chupa ya chai na kahawa na mikate ya sinia.

Nikakaa kaa kidogo pale uvivu ukaanza kunijia, nikaamka nikakimbia kimbia kidogo, leo nilikua sina mwiko wa dawa, nikaenda kujitupa baharini nikaanza kuogelea kwa kasi, mpaka kama dakika kumi hivi nikajisikia kuchoka nikarudi ufukweni, Ile narudi kwa mbali nikaona mtu yuko pale kwenye lango la pango kwa nje, kasimama na bakora moja nzuri. Kufika karibu nikatoa salam, akitikia, akanambia mimi mgeni wako bwana mkubwa. Nikashangaa, hakuna anaenitta bwana mkubwa isipokua babu yangu tu. Nikamwambia karibu, kwema?

Akanambia, kwema sana, nikamwambia subiri nilete kahawa tunywe, hakunijibu kitu, nikaingia kwa ndani ya pango nikatoka na chupa ya kahawa na vikombe viwili. Nikavitia kahawa, akanambia, samahani, mimi sinywi kahawa hiyo. Nikamwambia ngoja nikuletee chai, akanambia hapana, usilete, kaa kunywa nikueleze kilichonileta. Nikakaa nikaanza kunywa kahawa yangu, nikahisi anitazama mimi halafu anaishika fimbo yake anaitazama.

Akaniuliza "umeupata mzigo wako pale unapolala?", nikamwambia ninapolala wapi? Akacheka, akanambia si hapo ulipolala jana? Nikamwambia sijapata mzigo wowote, nikawa napiga dua za sura ndogo ndogo za Qur'an, kimoypomoyo, nikaanza kuhisi huyu sio mtu wa kawaida. Ikawa kama kanielewa kua nimeingiwa na hofu fulani, akanambia usiwe na hofu, mimi ni rafiki wa babu yako, nenda pale ulipolala kwenye mto wako tazama vizuri utakuta mzigo wako, njoo nao.

Nikaingia ndani kwenye mto wangu wa rundo la mchanga niliojitengenezea, hikaona kuna kama kimkebe cha bati hivi, nikakibeba, kukitazama kilikua na nakshi nzuri sana, na kilikua sio bati, nilipotoka nacho nje nikaona ni chuma kinang'aa nikawa nakishangalia, kinaonesha cha zamani kweli kweli. Yule mzee alikua anitazama tu, huku antabasamu. Kumtazama sana akasema fungua hicho kimkebe uone kina nini ndani, kukifungua nikakuta kina pete moja ina jiwe jekundu lakini limekooza sana linakwenda kwenye weusi. Akanambia "ivae hiyo kidole chochote utachopenda, nikaiva ile pete kwenye kidole cha shahada. Ikawa imenikaa sawaswa kama imepimwa.

Akanambia huo mzigo wako na huu mzigo wako, akanipa ile bakora aliokua amishoika. Akanambia hii bakora ni yangu, ukiwa nayo hii ujue na mimi sipo mbali, usiniulize kwanini. Ukitaka kujua zaidi muulize babu yako. Hiyo pete ni ya kiumbe mwingine . na yenyewe muulize babu yako mambo take, mmi nakueleza kitu kimoja tu kuhusu hio pete. Hio pete usiivue ukaiacha nje, ukiivua hakikisha unaitia kwenye huo mkebe na unauweka vizuri. Hawezi kuufungua mtu huo isipokua wewe na mwenye hio pete, ukiiweka nje ya huo mkebe kama hujaiva, inaweza kuibiwa au inaweza ikapotea usiione tena. Ikiibiwa, huyo akatakaeiiba atapata madhara makubwa sana na itakua ni kwa uzembe wako. Umeelewa? Kabla sijamjibu akanambia, mambo mengine muulize babu yako, kwa heri. Mimi njia yangu napitia humu ndani ndio inakua karibu na kwangu, akaingia pangponi na mimi nikamfata nyuma, lakini alikua anakwenda ndani zaidi pangoni ile natazama pembeni kumtazama tena sikumuona, nikarudi zangu nje ya pango. Nikakaa nakunywa kahawa huku naitazama ile pete, nikaona ina michoro pete yote na hata lile jiwe kwa ndani lilikua kama lina muhuri ambao sijauelewa maana yake. Nikaitazama fimbo, nikakuta na yenyewe ina alama fulani kabla ya pale ilipopinda kushikiwa na chini kabisa huko kama vidole vinne kutoka chini kabisa ilikua na kama alama za nyaya zilizoingizwa kwa ndani lakini zipo sawa sawa na ile fimbo. Ilikua ni nzuri sana kwa uchache. Nikawa nawaza ya kumuuliza babu kuhsu pete na fimbo.

Itaendelea.
Simba.
.

Freshii mwanetu, we tupige marungu.
1. Yan umeachwa mwenyew pangon hujaogopa?
2. Umeona mtu kaja kiajabuajabu lakin hata hujaonesha uoga?
3. Hili ndilo nimekuta naogopa mim, mtu anapotelea pangoni afu unaendelea kumfuata mkuuu?? Na kasema n njia ya mkato kwenda kwao ila ukamfuata??

Anyway sijui ujasiri wako, ila mim hata pasingelalika hapo 😄
 
1724769432521.png


Wajuzi tambueni nini hicho na wapi hapo. Nimescreen shot video clip ya zamani sana.
Simba.
 
Arsis; Yesu ana baba, hakuna muujiza hapo, hata Adam ana baba.


JMimi; amani mimi Muislam, huo utata wa Arsis, mimi mpaka leo anani[pa aya za Qur'an kuhusu hilo lakini mimi sio msomi sana wa dini, mimi najua kuisoma Qur'an kama watu wengi wengine, sijaend deep, Arsis ananipeleka huko taratibu sana.
Simba.
Anaposema Yesu na Adam wana baba ana maanisha baba halisi wa kimwili au baba wa kiroho?

Pia muulize je, anaamini katika kitabu cha biblia?
 
Arsis: wacha watu waongee dini, ndio ubongo unakua na maadili yanapatikana. Huyu simba alikua zamani anaongea ushetani tu wa upnade wa pili. Siku hizi anaanza kujua dini kwa sababu watu wanaongea dini. Usiogope wala usichukie kuongea dini, hakuna maadili bila dini. Zote.
Simba.
Sawa simba, Haya wale wadini ruksa jimwageni na mimi kama kuna mtu anaswali kuhusu uislamu uliza be Free but maintain respect.
 
Hapa km ni makaburini na huyo ni jinni bakora.
Sio makaburini. Hicho ni kituo chamgu cha kukutana na Srsis kulikua kuna majengo mapya yanajengwa na ya zamani yanabomolewa, lakini hio sehemu ya hio miti hawajaigusa kabisa katika ujenzi wao. Kwanini d-sifahamu.
Huyo sio Jini bakora lakini ni jini ambae Arsis alisema :ni jemedari wa vita unayoenda kupigana Unguja".

Kisa cha Unguja kitakua kifupi lakini kitamu.
Simba.
 
Arsis; Yesu ana baba, hakuna muujiza hapo, hata Adam ana baba.


JMimi; amani mimi Muislam, huo utata wa Arsis, mimi mpaka leo anani[pa aya za Qur'an kuhusu hilo lakini mimi sio msomi sana wa dini, mimi najua kuisoma Qur'an kama watu wengi wengine, sijaend deep, Arsis ananipeleka huko taratibu sana.
Simba.
Sawa kaka.. Samahani Arsis ni nani? Sijasoma threads zote..
 
Sawa simba, Haya wale wadini ruksa jimwageni na mimi kama kuna mtu anaswali kuhusu uislamu uliza be Free but maintain respect.
Dini zote ruksa. Arsis mwenyewe ananichanganya, ananambia yeye ni Muislam lakini ni mkrsto, myahudi mbudha. Pia ni mason na hapo tunapokutana ni lango la masons wa Mashariki ya Afrika kuendea dunia ingine. Ipo screeshot juu kidogo hapo nimeiweka.
Simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom