Inatokea post namba 1341
Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 F.
Kufika Inn by the sea, tukawakuta wengi wengi wapo nje pale garden, tukasalimiana na yule mama.Mee Ali akawamwambia huyu ndio ulikua unaongea nae kwa simu.
Mama: Kumbe kijana kabisa nilifikiri mtu mzima kama mimi.
Mzee Ali: basi hata sauti huisikii?
Mama: Simu baba, sikujua kabisa kama kijana kabisa.
Tukasalimiana na wengine. tukamaliza kusalimiana.
Mzee Ali kwenye gari nilimwabia hatukai, akasema hata mkewe kamwabia tusikae wala tusile kitu. Basi tukaagana nao baada ya kuwaeleza kuhusu chakula cha mchna kesho, mzee Ali akasisitiza wasikose kuja kwa muda, chakula kitakua tayari watu wakishuka kusali tu mchana. Tukaondoka.
Siku ya pili, kweli babu alikua kachinjisha ng'ombe, wapishi hukohuko alikoagiza apikiwe biriani wakaja na masufuria ao, kila kitu tayari, mapema kabisa. Wakaja na masamaki kibao, ya kuchoma ya kuoka. makachumbari, mapilipili ya kusaga. wakatayarisha msosi, Tuliporudi kusali tu, watu kibao, Mzee Ali aksema kuna vijana wametokea msikitini watapiga dua kidogo halauy tutakula, Ikawa hivyo. Baada ya kula maongezi kidogo, wengi wanaona mbona kazi tulioitiwa haifanyiki, lakini wanashindwa kuuliza, mwenye kahawa anapiga, mwenye chai ya rangi, mwenye chai ya maziwa, mwenye anjari ya Tanga nyeusi , nyeupe, wanapiga pale kwa raha zao huku wanadhangaa shangaa.
Wakati vyombo vichafu vinakusanywa, bwana mmoja mtu mzima, anaonesha mtu anaenukia noti, akasema mimi ndio kaka yao mkubwa, hawa wote ni wadogo zangu, wanangu, wajukuu, wake zangu. Hajabaki mtu wa ukoo labda waliopo nje ya Tanzania na mtoto wetu alietuleta hapa. Sasa nini kinaendelea hapa?
Babu: Tumemaliza kazi, hapana kinachoendelea kwa sasa tuagane lakini naomba wewe bwana mkubwa na mama mwenye mwanae na vijana wawili mmoja wa kike na mmoja wa kiume mbaki mwisho kuondoka. Wengine waende tu wakapumzike nje kwenye magari, wasiondoke wawasuniri, nyie mnaobaki mtaenda kuwaelekeza cha kufanya. Yule mzee akasema kama ni hivyo nipeni kahawa, wakakaa na babu wanakunywa kahawa, ikawa watu wanatoka wanakwenda kwenye basi lao kubwa lililowaleta na wengine kwenye coaster, ikawa kuna mama moja sio mzee sana, kavaa vizuri kipesa pesa, mashabu manene manene, vidolenoi, mabangili mahereni anakwenda mlangoni hatoki na wenzake anarudi ndani anawafata wengine wakitoka, anatoka akifika mlangoni anarudi mpaka wote wakaisha akabaki yeye na wale walioambiwa wabaki, wengine washaingia kwenye mabasi huko nje.
Babu: basi jamani ruksa nendeni tu, maagizo yenu ya nini cha kufanya mtaondoka hapa na bwana aAli atawaelekeza huko.
Tukaagana nao, wakaanza kuondoka, cha ajabu, yule mama alievaa kitajiri, na madhahabu kibao, ikawa anakuja mpaka mlangoni anarudi ndani, anakaa ananyayuka anaenda mlangoni anarudi. Mimi nikashangaa kwanza, Mzee Ali akawa anacheka tu kichinichini. Babu anakunywa kahawa yake kama hajui kinachoendelea. Wenzake wote wakatoka. Mara yule mama mlangoni akaanza kusema...
Yule Mama; Jamani nipisheni niende wenzangu wataniacha na magari.
Babu; Mwacheni mgeni aondoke, anasema kuelekea mlangoni.
Mama Yule; Ahsanteni , ile anatoka akarudi ndani. sasa nitatokaje, wamejaza maji namna hii, nini hiki, ziwa au bahari? kumbe mpo baharini kabisa?
Babu; Njoo mama, pita huku mlango mwingine, akamuonesha mlango, akamwambia mjukuu wake mmoja msindikize mbele lakini usimshike mkono, mwache aende kama ataondoka, wakaenda, sisi tunawaona, mara wakarudi.
Mama yule; Huko ndio siendi kabisa, watu wangu wanachomwa moto mnataka kunichoma na mimi?
Babu; Ali kawaite yule mzee na yule mama wapo nje wanamsubiri.
Mzee Ali akaenda akawaita wakarudi.
Yule mama; Jamani bora mlivyokuja, nyie mmepirta hapa hapa? Na maji yote haya?
Wale wakawa wanashangaa, hakuna maji hata tobne, Sisi wote tuliopo pale hatuoni maji anayaona peke yake.
Babu; Njooni mkae hapa. wakakaa.
Babu; Haya nenda mama hawa watakuja,
Mama Yule: Baba hapatokeki hapa, mie nakufa leo jamani.
Babu; Bwana na mama na Sheikh Ali, huyu ndio mtu wenu aliewaleta mpaka huku, anajua huyu mtoto wenu yuko wapi, ongeeni nae vizuri.
Yule Mzee; kwanza hebu niongezeni kahawa.
Akapewa kahawa, yule mama mwenye mtoto kama kapigwa bumbuazi anatazama lakini haamini anachokisikia.
Yule Mzee; Akamwita kwa jina yule mwanamke,
Mama yule: Ndio baba, huku anapiga magoti.
Yule mzee; simama, haya sema unajuwa "fulani" yuko wapi?
Mama Yule: Aaah baba, mambo makubwa sana haya.
Babu: Sema moja , usitupotezee muda, unajua hujui?
Mama Yule: Najua baba.
Babu: haya waambie hawa yuko wapi na wanampata vipi?
Mama Yule; Yupo Bunju Huko Dar, kwani hapa tuko wapi?
Babu: Wewe wacha kuuliza maswali, wewe jibu unachoulizwa.
Babu: Muulixeni, mimi atanitia hasira.
Mama; Sharifu ongea nae wewe baba.
Mzee Ali: Sema mama yuko wapi fulani?
Mama yul: YUpo bunju baba.
Mee Ali: kwa nani?
mama Yule: kwa washirika wetu baba.
Mzee SAli: Washirika wenu wangapi?
Mama yule: Huko Bunju mimi nawafahamu wawili.
Mzee Ali: Mlimchukuwa wapi?
Mama Yule; mwanza mabatini baba.
Mzee Ali: Kwa nani?
Mama Yule: kwa washirika wetu baba.
Mzee; Ngoja Sheikh, napomba wakaitwe nje kwenye gari akaanza kutaja majina, akamwambia mama wa yule mtoto.
Babu: Huyu hawezi kwenda sasa hivi, Simba nenda wewe kawaite.
Mimi: Nipe mjina mzee.
Mzee akanza kutaja majina kama watu sita hivi, akasema hao watatu wanawe wa kuwazaa mwenyewe huyu, hao wengine ndugu zake wote.
Babu; Simba waite hao waambie waje na vijana wote wa karibu waliokuja nao.
Nikaenda kuwaita, wakaja watu kama kumi hivi.
Itaendelea.