Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Corazon Espinado ,muulize Arsis kama hii biashara ya betting kuna namna hizi biashara za betting zinafanya ili wakamalia tupoteze au huwa wanaenda kuzimu wanapata nguvu za kichawi za kutuvuruga akili wakamalia
Hakuna cha Arsis wala Ramsey...acheni kuendekeza upuuzi, hii ni chai kama chai nyingine na mtunzi katulia na tecno yake anabuni vistory huku akiokoteza mistari na majina kwenye quran. Hebu tumieni akili basi
 
Kwakuwa stori imegusa dini yako (quran) basi umejitia upofu huonu kama ni ya kutunga na bado unajazia nyama! Kila kilichoandikwa humu ni chakufikirika, hakuna ukweli hata 10%. Mtu mzima unaambiwa mtu alifungua chupa akiwa kazungukwa na joka la vichwa vitatu, dragoni anayetoa moto mdomoni sijui na wanyama gani na weww unaamini kisa kaigusa quran!? Huo ni zaidi ya wendawazimu.
Mimi nilipinga sana hicho kisa lakini nilikua nashindwa kumbishia sana marehemu babu yangu, kwa kua najua hana sifa ya uongo. Nikaanza kubishana na arsis kuhusu hilo wa miaka, alichonijibu ni maneno mawili natatu tu. Kisha miaka kama mitano au sita nyuma akanambia kazi kwako.

Alinambia soma kuhusu"vitual reality na augmented rality". Dah kuzisoma nikaogopa na sana, vitu ambavyo vinafanywa na watu hivi sasa.
Simba.
 
Kama nilivyokuahidi, kua Arsis anamfahamu na alishahi kunipa kisa cha Yesu zamani. Nimeipata kumbukumbu yake.

Nilipomuuliza Arsis alinipa majibu ya ajabau sana, ambayo ni kinyume cha mafundisho ya Ukristo na Uislam na yenye utata sana.


Utata wa kwanza; ni kuhusu Maria Bikira ( Bi Mariam kwa Waislam) hakua bikira kabla ya kuzaliwa kwa Yesu na Yesu hakua mtoto wake wa kwanza.

Utata wa pili; Mariam mama wa Yesu ni Mmisri wa ukoo wa wafalme wa Kimisri aitwae Meritaten

Huu utata wa pili, Arsis alisema "tafuta kwenye simu yako 'meritaten" utaiona picha yake iliotengenezwa wakati wake, sio hizo za kuchorwa zilizojaa kila sehemu. Ukweli huo unafichwa sana.

Utata wa tatu; Arsis anaamini Waislam wana kitabu kizuri sana, Qur'an, lakini hawakisomi kwa kukielewa, wanakisoma kwa kuimba tu.

Utata wa nne; Nilipomuuliza kuhusu Biblia akasema, hicho ni kitabu cha wagiriki. Nilipomwambia afafanue zaidi, akanijibu , mimi sikuja kukufundisha Biblia wala Qur'an, hivyo vitabu vipo, visome usichokielewa niulize.
Kwamba Biblia ni kitabu cha wagiriki lkn kitabu hichohicho unachosema cha wagiriki kipo kwenye quran ( Torati, Zaburi, Injili) na mnatuaminisha vilishushwa na Mungu! Kwahiyo Mungu alishusha quran yenye vitabu vya wagiriki!!!??? Yaani alicopy kwa wagiriki then akawashushia waislam!? Tumieni akili
 
hakuna nilipoikataa Qur'an, tafadhali chunga sana kauli yako. Mimi sipo hapa kufundisha Qur'an wala Biblia, wala kukuaminisha chochote kile. Wewe fundisha hapa unalolielewa tutakusoma, haujakatazwa.

Mtu kauliza, Nilipewa majibu na Arsis kama Arsis, siku nyingi sana. Baada ya majibu hayo nikamuuliza sana tena sana nikawa nabishana nae sana, yeye kasisitiza kunielewesha kua "huisomi Qur'an unafata maoni ya watu". Nikawa naisoma Qur'an bila maoni ya watu, neno au maneno nisyoelewa nauliza kila sehemu. Mpaka kwake, Arsis ananipa njia tu na kunipa maana ya baadhi ya maneno nje ya watafsiri wa Qur'an. Ninachoweza kusema, tunahitaji kusoma sana tena sna, bila kua na jazba.

Si unaona umeanza kunihukumu, kwa jazba tu, aya ulioileta haijaonesha ubikira wa Mariam.

hapa sikuja kufundisha Qu'an wala Biblia, nimekuja kuongelea visa vyangu vya kujaaliwa kukutana na viumbe vsiyoonekana, kama majibu yao hayajakupendeza au hayajakuingia, leta swali tuwaulize au subiri wakikusoma wanaweza kukujibu kupitia kwangu. Nina uhakika Arsis anausoma huu uzi.
Weka aya wewe inayoonesha Maria hakuwa bikra.
 
Huyo mwenye jini la kiswezi .

Waswezi ni walevi sana.
Hujaona majini wanaokunywa pombe wewe, kuna majini wa ki comoro hao wanaitwa kibuki, hao wapo comoiro na Japan, hata Japan wanaitwa hivyo hivyo kibuki, nilishangaa sana nilipopewa hio elimu na Arsis, amejuaje majini wa Comoro na Japan wanaitwa ivyo ivyo?. Wote wanapiga pombe kali kali tena za ghali, mapombe ya bei kubwa, wewe mzee wa chai huyawezi bei zake.

Wewe naona ndio jana Arsis alisema "they've opened a can of worms", unaanzisha mabo usiokua na uj)uzi nayo.

Leta vitu, watu wafunguke zaidi. Unajua unanikumbusha mengi sana, mimi na Atrsis ni zaidi ya miaka 30 kujuana nae, mengine nayasahau wewe unakumbusha.
Simba.
 
Upo baina ya Dar na Kilwa. Ni jiji kubwa sio mji tu. Ni katika miji ya wnzi za Mafirauni.

Lamu upo mwingine kwenye himaya hio. bahari kuu ya Mytwara ina mji pia lakini huu maji yake ni kina kirefu sana.
Tunaofanya kazi za ubaharia bila kujiganga huko baharini unaweza usitoboe...yani meli inapita juu kumbe chini kuna mji🙌🙌🙌🙌🙌
 
Kwamba Biblia ni kitabu cga wagiriki lkn kitabu hichohicho unachosema cha wagiriki kipo kwenye quran ( Torati, Zaburi, Injili) na mnatuaminisha vilishushwa na Mungu! Kwahiyo Mungu alishusha quran yenye vitabu vya wagiriki!!!??? Yaani alicopy kwa wagiriki then akawashushia waislam!? Tumienj akili
Arsis anasema hakuna biblia kwenye Qur'an labda umewasoma watafsiri sio Qur'an.
Simba.
 
Inatokea post namba 81.

Nikabeba bakora yangu nikaelekea kwenye uwanja, nikaukuta uwanja mweupe kama umesafishwa, kutazama saa ya simu yangu ilikua saa 9 kasoro dakika 1, nikaona nimefika kwa muda muafaka, nikasima natazam huku na kule nashangaa shangaa, uwanjani, kwa mbali, mwisho wa kiwanja kile kutupu, kina kama miti miwili mitatu na yenyewe sio mikubwa sana, nikaona kama kuna mtu kavaa abaibui kwa mbali, nikatoa salaam kwa sauti hajaitika, nikaanza kusoma dua, ile nasoma dua, yule mtu akapotea mbele ya macho yangu, ingawa ilikuwa kama mita 30 kutoke kwangu lakini kulikua ni mchana kweupe, kupotea kwake ikawa kama kayeyuka kwa kwenda chini ya ardhi na kwa mbali nikaona kama lile baibu limebaki pale nikawa nalisogelea kulitazama huku nasoma dua ndogo ndogo, kufika kama hatua kumi na pale, nikaona ardhi ni nyeupe, hakuna baibi hakuna mtu. Nikacheka nikawa narudi pale kati ya uwanja, ile nafika kati ya uwanja nikajiuliza kwa sauti, yuko wapi aliyenitaka nije, itakua ndoto tu ile, nikawa naondoka, ile naanza kuondoka, nikasikia sauti ikiniita Bwana Mkubwa, nikageuka kutazama pande zote sikuona kitu sauti ikaendelea kunambia, huwezi kuniona, tafuta kitu ukae chini hapom nikajibu wewe nani, mimi staki kukaa, ile kusema sitaki kukaa, kama nguvu fulani ikanivuta chini, nikajikuta nimekaa chini, nikitaka kunyanyuka nashindwa, nikapata kama hofu fulani, Ile sauti kwa upole wa kawaida, ikanambia usiwe na wasi wasi kaa chini, huwezi kunyanyuka hapo, ni mimi nimekuita, mimi naitwa arsis, nikamwambia ramsis? Huyo si firauni, akanijibu akzsema kweli ris.is ni katika mafirauni, mimi sio ramsis, ni arsis. Nilikuwepo pia wakati wa ramsis, namfahamu.

Ikawa wakati tunaongea kama mwili umejiachia na naweza kusima, nikasimaa sauti ikanambia tena, kaa chini tulizana. Uliza chochote unachotaka, naona una maswali mengi sana unajiuliza. We niulize tu, mimi nipo hapa kwa ajili yako. Nikawa nasita kumsemesha. Akanambia nisikilize kwa makini. Mimi nipo hapa kwa ajili yako, babu yako amesikia tu habari zangu hajwahi kuongea na mimi hata siku kama hivyi ninavyoongea na wewe. Hiyo pete ulioivaa ni yangu na mimi nimekuzawadia, hio pete ni ya zamani sana na inawindwa na kila mtu na majinni wajinga wajinga wanitaka sana hiyo. Nikamuuliza, wanaitakia nini? Akasema ukiwa na hiyoi pete ndio unakua u karibu na mimi na ukiivaa hio mimi nakua nipo chini yako, hio pete yangu lakini mimi siruhusiwi kuivaa toka nilipooneshwa, mimi kazi yangu kuilinda na anapokufa anaeivaa mwenye pete hio naichukua namtafuta mwenye vigezo vya kuivaa. Kwa sasa nimekaa nayo miaka 925 bila kupata mtu wa kumpa hio pete aivae, nimeacha salamu nyingi sana, mpaka mwaka juzi, nikatumiwa salamu nije kukuona kama una vigezo, nikawa nakufatilia sana, nikaona vigezo unavyo na vingine utajifunza kadiri siku zinaenda.

Kwa ufupi, hio pete, unaweza kuivaa kidole chochote, mkono wowote, na kila utapoivaa utaiona ipo sawa, haikeri mkononi. Unaweza pia kuivua wakati wowote, lakini kumbuka, ukiivua lazima uiweke kwenye kijaruba chake. Haitakiwi ikae bila ulinzi wangu hata nusu dakika, kukupotea hiyo ikiwa umaivaa ni kitu hakiwezekani, wala haiwezi kuvuka kwa bahati mbaya. Ikikaa kwenye kijaruba chake hakunaambae haimuhusu hio pete akaweza kukinyanyua. Wewe si umekiona kawaida unakibeba inakifungua unakitazama, lakini jaribu kwa wengine uone kama watawea kukibeba. Nikamwabia, nakuamini, sina sababu hya kujaribu. Akaendelea kusema, ukinihitaji wakati ewowote wewe niute gtu. leo namalizia kwa hayo tu, usiku saa tatu uje hapa uniite, tutaongea zaidi na tayarisha maswali yakuniuliza. Uliza chochote utakacho kukijua, nipo hapa kwa kukupa elimu ambayo watu wengi sana hawana. Babu yako amenisikia tu habari zangu kwa mwenye hio bakora, lakini hajawahi kuongea na mimi isipokua huwa kuna vitu tunamuotesha ndani ya hii miaka mitatu, toka nilipokuona wewe. Mwenye hio bakora ni rafiki yangu wa miaka mingfi sana. Hio bakora nayo sio ya mchezo mchezo, lakini yeye mwenyewe atakufahamisha. Nikamwabia nifahamishe tu, kwani kuna ubaya? Akanambia, hakuna ubaya lakini mwenye ndio atakufahamisha vizuri zaidi. Unakumbuka ulivyolala leo mchana uliiweka wapi? Nikamwabia pembeni yangu, akanambia unakumbuka ulivyoamka uliikuta wapi? Nikamwabi nimeikuta imesimama kwenye ukuta wa pango. Ile sauri ikacheka, ikanambia haya kwa heri tutaonaana saa tatu usiku. Uje peke yako, ukija mwengine yeyote hatutoweza kuwasiliana, hautakiwi uje na mtu ukija kuniona. Kwaheri, akaniaga na mimi niawa natabasamu narudi pangoni.

Kufika pangoni nikaingia kwa ndani ya pango, nikaiweka fimbo pale chini kwa kulaza chini. Kuiweka tu, ikaanza kunyayuka yenyewe ikasimama ikasogea pembeni ukutani ikajiweka pale. Nikacheka kimoyomoypo. Huku najisema makubwa haya. Mara nikasikia hodi nje.

Kutoka nje ya pango, nikawakuta vijana wa babu wamekaa, wakanambia ulikua wapi Bana mkubwa, tumekuja muda hatujakukuta, tumekutafuta kote hatujakuona, kumbe upo hapa ndani mapangoni? Kabla sijawajibu, waksema leta pilau lile tuli[pige, bibi huko kasema tuje kula na wewe usile peke yako. Nikatoka na lile kapu la chakula wakaandaa pale tukakaa tukapiga pilau, ilikua pilau ya nguvu kweli, pilau ya kamba.

Mooja wa wale vijana akasema hao kamba bwana wanaitwa taiga, hao ndio kamaba ghali kabisa wakati wa msimu, hao ni lazima msimu ukianza ni lazima apelekewa babu na bibi pale nyumbani, hao wa pilau hiyo ni fresha wa alfajiri hao, hawajaguza friji hao. Hao ni wakubwa kasi sio wa kawaida wana nyama kweli. Tena usiku tutakula hao hao wa kuchoma, baadae tukawavune bwawani kwao. Wapo leo, wengi hawapajui pale.


Tukala pilau tukamaliza, kulikua n chiupa ina juisi ya machungwa, tukaipiga pale. Nikawaambia leo hatuna haja ya kula tena. Wakacheka yule nnae kaa nae pangni akasema usiku baridi huku, bibi kasema tukawavune tuwatengeneze wa kuchoma, yeye atakuletea rojo lake la kulia hawa, atakuja nalo babu usiku. Nikawaa mpbia poa, kweli usiku kuna kibaridi huku.

Tkakaaa kaa wananip story za kamba na namna wanavyotengeneza pesa msimu wa kamba. Wakasema kuanzia miezi miwili mitatu ijayti tutakua hatungji msimu, babu alimleta mtaalam wa ufugaji kama tumeshaanza kuchinga njia ya maji na bwawa upande ule, wakanionesha kwa kidole. Babu kafanya jambo la maana sana, lakini yuke mtaalam akasema huku pa asili tusipaguse kabisatupaache hivi hivi, hawa kamba wa asili huku ni bota mara mia kuliko wale trutakaowafuga, ingawa mbegu tutato hapa hapa, watakua tofauti kasema. Nikawaambia naona itakua kama kuku wa kienyeji na broila, wakacheka, wakasema hata mtaalamu kasem hivyo kwa sababu wale wa kufuga kuna vyakula vya atatufundisha kuvitengezeza ili wawe wanakua haraka. Tutaona jamani, itakuaje.


Itaendelea.
Jumbo Prawns🦐 🦐
Tiger Prawns
.............
 
Hakuna cha Arsis wala Ramsey...acheni kuendekeza upuuzi, hii ni chai kama chai nyingine na mtunzi katulia na tecno yake anabuni vistory huku akiokoteza mistari na majina kwenye quran. Hebu tumieni akili basi
Ramses, huyo aliesema Ramsey mimi simjui, nakubaliana na wewe hakuna.

Arsis kama vile ulivyo wewe Kanali_ haytukuoni. Tunakusoma tu. Mimi Arsis namsikia sauti, kakuzidi hapo tu, ukianza kutuma audio clips humu, utamzidi ata yeye. Leta vitu.

Kanali wa jeshi lipi wewe?
Simba.
 
Arsis muulize Arsis kuhusu lile jina la Mwenyezi Mungu ismullah liadwam jana alinambia nitafute idadi ya sura zinazoanzia na Alif Laam Miim nikamwambia ni 3 ila leo nime research kidogo nimegundua ni sura 8 zenye Alif Lam na mim
Suratul baqara, al Imran,Al Aaraf, Ar Rad, Al Ankabut, Ar Rum, Luqman As Sajda.
Mwambie kingine nini kinafuata ?
 
Vionjo vya Arsis 1 - Pete yake.

Kuna siku nilimuuliza Arsis thamani ya hii pete alionipa. Arsis akacheka sana akanambia haijui thamani yake.

Mimi; Arsis, babu yangu alinambia hii pete ulionipa ni yako binafsi, ile uliompa yeye ni kopi ya hii kwa kutumia vitu vya hapa dunia yetu, nifahamishe zaidi kuhusu hilo.

Arsis; Kweli, zipo pete zangu tano mpaka sasa. Hio yako ilikua yangu binafsi, ni ya kipekee, imetenezwa kiustadi mkubwa sana, nilitengezewa na rafiki zangu wa dunia ya tano Ramadiyin, lakini walikataa kabisa kunambia hicho kito chake kinaitwa nini au wamekitoa wapi. Nikawuliza na na hiy pete yenyewe ni ya dhahabu au ya material ipi.? Walinambia wewe chukua hii na wakanielekeza namna ya kutengeza pete nyingine na kuzipa nguvu ya mawasiliano kwa kutumia hii yako. Nimetengeza moja nyingine kama hio lakini ya kito sio cha hapa kwenye dunia hii na nimechanganya chuma aina nyingi, ina mawasiano ya moja kwa moja na hio pete yako na zingine tatu ndio maana naweza kujua wewe unafanya nini wakati wowote, ukiivaa au usiivae, mradi ipo kwako nafahamu.

Mimi; Na zingine?

Arsis: Moja ile ya babu yako, siku hizi anavaa dada yake. Mbili za wale wasaidizi wangu alionipa Jini Bakora. Ndio hizo tu.

Mimi; Thamani yake si lazima ijulikane, hakuna kitu kisichokua na thamani.
Arsis; Sikiliza Smba, hapa kwenu wapo masonara na watu wa madini, wapelekee wakakupe thamani yake, hata mimi natamani kujua hilo.

Mimi; Ile ya babu?

Arsis: ile hata wewe unaweza kujua thamni yake, ile na ile ya wale majini wawili wanawake, ni vito vya ruby, na dhahabu imechanganywa na fedha kidogo na shaba. Huwezi kutengeza dhabu tuu ikawa ngumu.

Mimi; Ile ya babu lakini ni rangi ya silver ila kito cha damu ya mzee, zile za wanawake wa kijini kito kinafanana na cha babu lakini yake mraba kama yangu a)za wanawake wa kijini za duara. Na pete zao rangi ya dhahabu.

Arsis; Ya babu yako ni dhahabu nyeupe za wanawake ni dhahabu ya njano. Sikiliza simba, kesho nenda na wale wanawake wa kijini duka la sonara ujue thamani yake hio pete, na mimi nitakua na nyinyi. Leo atakuja yule jini mwanamke kukufundisha kitu kuhusu hio pete yako, mimi nitamfundisha atakuelekeza kuivua na kuivisha kito chake, hakuna anaeweza hata jini, bila kupata ruksa yangu au yako.

basi kweli, muda kidogo yule jini wa kike akaja akanambia ivue hio pete yako nikuoneshe namna ya kulivua hilo jiwe lake na kulirudishia. Nikaiuvua akanionesha. Ile pete yangu ilikua jiwe la mraba lakini kwa juu limetuna kiaina. kwa hini ni jiwe lenyewe lakini limefata mzunguko kwa mbali kama wa pete. Akanambia tazama nikatazama, akaiminya juu lile jiwe, kuelekea chini kwa mkono wa kulia kwa kidole gumba huku kaizuwia na mkono wa kushoto, niasikia kup, jiwe likatoka, akanambia kuirudishia ni hivi, akaliweka jiwe lini kwa ndani, akaliminya mkwa mkono wa kuliai kutokea kwa ndani kwenda nje, ikalia tena kup, akanambia tayari. Fanya wewe sasa.

Nikaiminya mara mojambili, ya tatu ikakubali, nikairudishia. Ikawa sawa.
jini1; Kama hukuusikia huo mlio ujue jiwe halijatoka kwenye pete na ukilirudishia kama hukusikia mlio ujue jiwe halijaingia.
Haya, tutaonana kesho twende kwa sonara, tumeagizwa na Arsis. nikamwambia poa. Akasema saa nne asubuhi tuwe tumeshafika kwa sonara, unapajua?
Mimi; Napajua, maduka yamejipanga mtaa wa Mkunguni pale.
Jini1; basi tukutane pale saa nne kamili, usinisahau tu nitavaa abaya.
Mimi; Poa.


Siku iliofata nikaenda nikawakuta wawili yeye na mamake, tiukasalimiana wakanambia haya sonara yoyote unaependa wewe. Tukaingia moja ya duka kubwa kubwa hivi pale Mkunguni, mlinzi akatufungulia, kuingia ndani wale wanawake mmoja akaanza, tuna pete zetu tunataka uzithaminishe, kama bei nzuri tujue. Jamaa wa dukani akawatazama mkononi, wakamwabia hizi hapa, wakamtolea pete kama nne hivi za dhahabu na moja ya kito, sio zile zao lakini moja ina kito cha Rubi, sonara akazipima zile tatu. Ile ya nne akaitazama na kidude kimoja cha machoni akawaambia hii mpaka niitoe hili jiwe kwenye pete. ruksa?
Jini 1 itoe tu.

Yule jamaa, alikua muhindi, akaichukua kifaa chake akakitoa kile kito akakitazama tena akasema hii ruby nzuri imechongwa kitaalam kabisa. Akaichungulia kama mara mbili tatu akaiweka pembeni, aksema hii pete peke yake bila jiwe, laki moja na elfu 60, hizi zingine pete ni nzito zaidi, hii moja laki tatu nahii nyingine laki mbili sitini. Hii Ruby peke yake million moja laki mbili kwa ajili yenu. mtaziuza?
Jini1; Bado hatujamaliza, mpe na hio, wakanambia mimi.

Nikaivua nikampa. Hapo ndio kasheshe likaanza, akaanza kuitazama, akasema hii inaonesha dhahabu imechanganywa kizamani sana hii. Hii ruby pia lakini sina uhakika, huku anaitazama sana ianaigeuza, akasema na hii inabidi niitoe, nikamwabia sawa.akahangaika kulitoa jiwe kwenye pete, aakatia vifaa vyake akashindwa, nikamwambia nipe nikusaidie. Akanipa nikaitoa nikampa akaipokea akaitazama pete kwanza, akaitazama mara mbili mbili, akatia kama zile koleo (pliers) zenye pua ndefu, ikawa kama anaisugua hivi, nikaona anashangaa inateleza, haisuguliki. akatoa kipande cha msasa wa chuma, akasema kidogo naisugua, haiharibiki,, nkamwabia poa, msasa ukawa

Akamwita mwenzake akamwambia hii dhahabu imechanganywa na nini? Yule aakishika akaitazama akasema sina uhakika lakini nzito sana, hii sijui wamechanganywa na chuma gani, hii bwana mpaka itiwe kwenye moto na sisi hatuna fundi hapa, tukiipima hivihivi tuanweza kula hasara, Hii lakini inaonesha ya zamani sana, hakuna mchongo huu siku hizi, sijui sonara gani huyu, umenunua wapi hii? Nikamwabia hio nimerithi.

Akaongea na mwenzake kihindi , yule akaanza kulitazama jiwe, akalitazama akasema hii ruby lakini na yenyewe ya zamani sana, hii cutting yake sijawahi kuiona na sijui inashikaje kwenye pete haitoki. Hili jiwe bwana siwezi kulithaminisha mimi ntakupa bei kama ya riby kwa uzito wake, nikamwabia sawa, akaiweka kwenye mzani wake wa vito, akalitoa akarudia mara ya pili, akamwita mwenzake, akaliweka na yeye kwenye mizani wakaongea tena kihindi.

Muhindi: Sikilizeniu jamani, hii inabidi itiwe moto au acid ili kujua dhahabu peke yake ni kiasi gani tuithaminishe. Na hili jiwe zito sana kuliko ruby ya size hiyo mara tatu, hii itakua sio ruby, sijui jiwe gani, Nawashauri nendeni Zanzibar Jewellers kule India street pale wana moto, wana acid watawapimia na hili jiwe. Akawa analiingiza jiwe haliingi, akacheka, sasa hii pete imekua ndogo au jiwe limekua kubwa? mbona haipiti kabisa? Nikamwambia nipe. aliponipa nikaweka kama nilivyofundishwa likaingia. Akanambia jamani hii pelekeni kule, haya vipi tumalizane dada?
Jini 1 akamwambia tunataka tujue thamani ya zote kwa pamoja, uli tujue tugnagawana vipi.
Muhindi: Nendeni basi kule mkijua thamani yake mnaweza kurudi hapa tutanunua.
Mimi; Poa, twendeni.

Tukaondoka mpaka Zanzibar Jewellers, mambo yakawa yale yale. wakasema hii tuipige moto, mnatupa tuksa? halafu tunaitia kwenye acid, hili jiwe ngoja niwashauri kitu. Nitawaelekeza mahali, hapa hapa karibu mwende pale wale wana mshine na kazi yao ni mawe tu, watasema thamani yake, mnaweza kuwauzia wao, lakini msiitie moto hii kabla hamjajua thamani ya hili jiwe, maana mnaweza kuiyayusha dhahabu ikawa mpaka mtengezee pete nyingine.

Tukaamua twende kwa watu wa mwawe kwa kua wapo karibu, ni pale mbele ya jamatini clock tower Dar.

Kuingia ndani bahati nikamkuta mtu wa mawe namjua siku nyingi, anaitwa Husseni Baniani,nikalitoa kabisa lile jiwe nikampa jiwe na pete, yeye alikua interested na jiwe tu, akachukua vitu vyake kama kuna kipimo kinatumia maji hivi, akanambia hiki kipimo ahakidanganyi, kinapima specific gravity, kitu kama hivo. Akaanza kupima akanipa chart moja ina uzani kwa kila aina ya germ stone na poicha picha za kila jiwe. Chart inaonesha kila jiwe na maelezo yake.


Akahangaika mwisho akanambia hii sio ruby, akasema hii labda red diamond. Akacheki, akalisugua na tupa inateleza, akanambia hili jiwe umepata wapi? hapa umelamba dume, lakini sijui jiwe gani. Hili bwana tuwachie tulipime taratibu, mie nikacheka. Akamleta sonara mmoja akampa ile pete, sonara akasema njooni muone tunachofanya, si mmeamua kuuza hili? mMaaana hii itayeyuka tutaibakisha dhahabu tu. Yule Jini akasema sawa hakuna shida, sonara akawasha gas akaiweka pete kwenye bakuli fulani la kigae akawa inaipiga moto, piga moto kweli kweli, ipo vile vile, akasema haiwezakanai, akaongeza moto, akamwita jamaa mwingine akamwita na yule Husseni, wakaipiga moto mambo yako vile vile. Yule sonara akasema tuitie kwenye acid, nikasema swa, wakafungua acid akaitia, ipo vile vile, haina hata kutoa moshi wala nini, wakamwita mzee mmoja wa kihindi, anaonesha boss wao, wakamweleza.

Akalitazama jiwe, pete ikatolewa walipokua wanajaribu kuichoma kwa acid, wakaitia kwenye maji, akawaambia pengine acid imekufa? Wakatoa kibati fulani wakakiingiza kwenye acid, haijachukua hata dakika kikayeyuka chite.Sonara akasema, hii acid mpya kabisa ndio nimeimimina sasa hivi. Wakatazamana wakaongeaongea pale. Boss wao akaelezwa kuhusu jiwe, akalitazama akamuuliza Huseni umepima weight yake. Akamwambia nimepima mpaka nahisi mizani yangu mbovu, haiwezekani jiwe hili liwe gram zaidi ya 250, muhindi akasema wewe umepima vibaya labda 2.50 sio 250. Husseni akacheka, akamwabia twende ukaone, tukaenda wote, wakapima, mhindi akasema hii mizani inataka ifanyiw calibration, ngoja nileta yangu, kaingia ofisini kwake akatoka na mizani yake ya digital, mambo yale yale, haamini macho yake. Akasema hii pelekeni kwenye mashine kubwa kule TGC, akatuelekeza, nikasema poa. akasema na hio pete wapeni waitest, pale mtapata jibu kitaalam lakini watawa charge gharazama za kupima kwa sababu biashra yao ni vipimo tu.


Husseni akasema sikiliza, mimi nachukua risk, hilo jiwe lamba million mbili mimi nikafe nalo, hio pete baki nayo mwenyewe utaweka jiwe lingine. Nikamwambia hapana, zinaenda pamoja, Nikalirudishia jiwe lamngu tukaondoka. Kutoka nje tukaagana na majini wale wa kike, wakaondoka zao, nafika nyumbani, kalba sija paki vizuri gari nikamsikia Arsis, umeona mambo? Utahangaika dunia nzima, una kitu ambacho hakina thamani yaani "priceless".


Hicho ndio kisa cha pete ya Arsis kwa uchache.

Itaendelea kwa kionjo kingine cha Arsis.
Unatuchanganya, kipande hiki ulikuwa Tanga kwa Babu akawa anakupa story za yeye kufahamiana na Arsis, ghafla kwenye kupima pete ushafika Dar!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom