Kiukweli katika hii audio kaka yako ameniangusha sana,yaan nimesikiliza mpaka dakika ya sita nikaona niache
Kwanza anazungumzia mambo ya kurithishana dhambi wakati katika imani ya kiislamu hakuna mambo hayo kabisa
Qur'an inasema mara baada ya Adam kufanya dhambi na mkewe hawa,wao pamoja na ibilisi walifukuzwa peponi,lkn Allah akawaambia kama ukiwafikia muongozo kutoka kwangu na mkaufuata basi mtaokoka
Adam akapokea maneno kutoka kwa mola wake ya kuomba toba ,nayo ni "hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu lau kama hutanisamehe nitakuwa miongoni mwa walioghafilika au waliopata hasara kitu kama hicho"
Hapo akasamehewa kasoro ibilisi ambaye alikataa kuomba toba kwa kiburi
Kwahiyo hakukuwa tena na dhambi za kurithi wala za asili,istoshe mola wetu anasema yeye ni mwenye haki hawezi kutuhukumu kwa makosa ya watu wengine
Lakini jambo moja ambalo liko wazi ni kwamba,majanga mengi tunayokutana nayo leo ni kutokana na yale tuliyatanguliza kwa mikono yetu wenyewe,kwa maana madhambi yetu ndiyo sababu ya adhabu tunazo pata kutoka kwa Allah
Kwahiyo kusema watu wanarithi dhambi hapana kwa waislamu hakuna hiyo