Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Mimi ninachojiuliza Sasa kwa Nini huyo arsis na hao maviumbe sijui majini, mashetani,mapepo nk
Hawataki kujionyesha live tukapiga nao story wakatupa hata michongo mpaka wakutane sijui na waganga,wachawi,manabii,mashehe nk
Ina maana wanatuogopa sisi watu wa kawaida ama?
Maana mara umesema sijui wanatembea uchi hatuwaoni kwa sababu wanatumia kipindi macho,kwanini wasije live maisha yaendee maana umesema tumeumbwa na MUNGU mmoja?
 
Niweke aya ipi? na haipo hio? Mimi sina ujuzi lakini wewe kama unasema ipo, tuwekee tumuoneshe Arsis na FaizaFoxy aliekubaliana na hilo.
Simba
Hawataipata aya hiyo. Watakuja na maneno ya watafsiri tu.

Niliandika. Mada kuhusu hilo.

Wanaiogopa kwa kuwa hawataki ilm, wanapenda kudanganywa tu na watu kama anayejiita Hance Mtanashati.
Mwambie Arsis aisome hii mada yangu:

 
Ujumbe mwingine wa Arsis nimeupata sasa hivi wakati naanza kuandika. Usijibu mtu "private, this is an educative thread, simba, you are not mganga or mchawi" akaongea Kiswahili, kua yeye Arsis atajibu linaloulizwa hapa, private ni baina yangu na anaeuliza, yeye hahusiki.

Kwa hio mnaokuja private msitegemee kujibiwa na Arsis maswali yenu ya Private, anasema anaeta yeye ili ajibu muulize hapa wazi, watu wengi wapate faida, kwa sababu tatizo la mtu mmoja wanalo watu millioni moja wengine. Anassema wabadilishe jina kama hawataki kujulikana halafu waulizze. Anataka kutoa elimu yake kwa watu wengi.

Du, leo tumemkorofisha nini Arsis?
Acha mboyoyo leta story, habari za Arsis kukutumia ujumbe ni chai tupu na unazidi kufanya watu waitilie shaka story. Umewaandikia huu uzi watu wazima so mengine kausha tu.
 
Swali langu Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.
Kwanini uliuza vyeti!? Kama uliamua kumuuzia basi tulia usifukue usivyoweza kufukia.
 
Clip ya dada yetu Nourhan kuna sehemu ilisemwa Malaika hawana ombile maalumu,kama ntakuwa nimesikia vizur,ni kwamba Malaika wameumbwa kwa mbawa kwa mujibu wa qur'an tukufu,tena ikasemwa wengine wana mbawa mbili na wengi tatu na wengine zaidi,mfano huyo malaika mkuu gabriel/jibril ana mbawa mpaka mia sita (600)

Kwahiyo hapa source ya uwakika ni qur'an kwasababu hakuna jini ambaye anaweza kumuona malaika,kama ambavyo binadamu hawezi kumwona jini.katika umbo lake halisi
Arsis nasema mkizitaja aya za Qur'an jaribuni kuzieweka, isije kua mnasoma maneno ya watu ya tafsiri mnasema ni Qur'an.
Simba.
 
Wetu sisi ni Yesu Kristo (masihi) maana hata enzi za Yesu katika bible walukuepo akina yesu wengine mfano baar-yesu.
Ila aliye pekee mwana wa Mungu aliye hai anaitwa Yesu Kristo
Hilo la "Yesu" ukipitia vizuri uzi #Arsis kaongelea.
Simba.
 
Kwenye Theology, kuna doctrine inayo husu mambo haya. Inafahamika kama ANGELOLOGY AND DEMONOLOGY.
katika imani ya kikristo tuna uwanda mpana sana wa elimu zema tu ndio vile haya mambo huwez kuta wanafunzwa waumini makanisani. Na hii ni kwakua wachungaji wengi hawajakwiva katika Theology makini wengi wanaishia kukwepa mambo magumu kama haya
Mwaga elimu.
Simba.
 
Swali zuri sana.

Mimi Simba, Corazon Espinadp lilikataliwa na Arsis, amesema kama yeye anakuja kujibu maswali iwe simba, nikamuuliza kwanini isiwe Arsis? Akasema sawa weka Arsis lakini usiweke Corazon Espinado.

Nikamuuliza kwanini? Akanambia wewe unasikiliza wanaimba lakini hujui maana ya hao mashetani wanaoimba. Akanipa bonge la story la ushetani wa mwanamziki Carlos Santana. Halafu ndio akanambia maana ya corazon ni. mapenzi ndani ya roho na espinado ni miiba mikali. Roho nzuri ilioingiwa na miiba ndio maana yake kwa ufupi.
Mkitaka kisa chake nitawapa, hii kanijulisha juzi, kuelewa tu, mwenyewe nikabadili ID.

Ukiona signature chini ya Simba, ujue sio Arsis.
Simba.
Shukrani kwa ufafanuzi. Tunangoja kisa cha Santana. Pia huu uzi ungewekwa sticky
 
Hotelini kwetu jumbo prawns 4pcs na vegetable kidogo na starch yoyote na sauce yoyote ni dollars 25.
Nimewaambia mimi siku hizi wakati wa msimu wajukuu na watoto wa babu wote tunawahi mahandakini,tunauza kamba kwa dollars. wanunuzi kibao kutoka Kenya wakati wa msimu. Msimu wenyewe haukai, sana sana siku tatu tu.
Simba.
 
Hii kazi nitaacha maana inaogopesha sana
Usiiogope bahari, haina madhara. Bora huko baharini kuliko binaadam wa nchi kavu.

Mimi naamini sisi tuna nguvu kubwa sana kuliko viumbe wasioonekana na wanatuheshimu sana, Wale waovu wanatuogopa sana. Ni kama mwizi wa kibindam anvyoogopa asishikwe akiwa anaiba. Au mchawi anavyojificha ficha akifanya mambo yake, ni uoga ule. Au Kama nyoka ni hatari lakini anaogopa binadam ndio maana anajificha ficha sana.
Simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom