Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Unajua 'Akili Mnemba' inavyofanya kazi?

Ndiyo, ninawakilisha mawaidha kwa sifa na hadhi ya algorathimu za 'Akili Bandia'...

Kiswahili Fasaha--OKAY, muktadha akilifu wa fasaha kwangu ni kile kwa kiingereza hutajwa ni sifa na hadhi ya 'Clarity':

noun: clarity

1. the quality of being coherent and intelligible.
"for the sake of clarity, each of these strategies is dealt with separately"

Yanayolingana:
lucidity

lucidness
clearness
perspicuity
intelligibility
comprehensibility
coherence
simplicity
plainness
explicitness
lack of ambiguity
precision

Kinyume:
obscurity
vagueness

the quality of being certain or definite.
"it was clarity of purpose that he needed"

2. "the crystal clarity of water"

Yanayolingana:
limpidity
limpidness
clearness
transparency
translucence
pellucidity
glassiness
purity
transpicuousness

Kinyume:
opacity
murkiness

the quality of being easy to see or hear; sharpness of image or sound.
"the clarity of the picture"

na tena 'Concise'...

Nashauri, Usichukulie lugha 'Kimazoea' ama ile tabia ya 'Usahihi wa Kisiasa'... Ndiyo asili ya jamii na wasomi na kuogelea kwenye vidimbwi vya 'self inflicted mediocrity'...

Hmmm
mose funguka kiasi kuhusu "lucid dream" jukwaa lipate faida. Wataalam wa saikolijia wanasema ni ndoto ndani ya ndoto. Watu wa roho tunasema ni maekezo ya viumbe visivyoonekana.
Simba.
 
sasa mkuu hio dizeli unamaanisha mafuta ya gari anunue mapya kabisa sheli au aliyotumika atoe kidogo kwenye gari na hiyo dizeli anampakaje je,kichwani tu,usoni au mwili mzima.? na kama aliyepandisha ni mwanamke baadhi wana misitu ya nywele kichwani inakuwaje.?
Dizeli mpya au iliotumika haina neno, mradi ni dizeli. Lakini mara nyingi dizeli iliotumika huwa ni kuoshea oshea vifaa vichafu vya magari tu, hua ni chafu.

Huhitaji diseli nyingo, kidogo tu, iroweshe kwenye kitambaa kidogo tu cha kumpakia.

Dizeli ikitumika kuendeshewa injini za kwenye gari au mashine zingine huchomeka na kua moshi (carbon) na mvuke (carbon monoxide), huipati.
Simba.
 
Kuna kitu kinachoweza kufahamika kama 'kufungika/kufungiwa ya kunasibika kuyajua kwa wakati'; kwa kiingereza ni mambo ya 'compartmentalization'...

Katika majukwaa kama haya, 'mada' ni jambo lenye asili ya kujiwekea mpaka wa kuyasikia na kuyajua kwa wakati; lakini vipi ikiwa 'asili ya mipaka katika kutaka/kupenda kuyafahamu kuyajua mambo' husigana na nasibu ya Ujumuifu wa 'Maarifa na Maarifu'(?)

Kwa mfano, huu uzi unajina: "niliyoyashuhudia-nilipofunguliwa macho"

Je, unatambua jambo la 'Kufunguliwa macho' lina asili ya 'Nuru ya Ufahamu, Maajabu na Mastaajabu' yake?

Ipi inaweza kuwa 'mada' katika 'Nuru ya Ufahamu, Maajabu na Mastaajabu yake' khasa?

Kiufundi, sisi sote ikiwa ni watu wa 'akili' na basi nasibu ya 'dini', adui mkubwa wa kupambana naye ni 'Kasumba' ya 'Mafungu Elimu'...

Labda iwe sisi watu hatuna mpango na 'Maarifa na Maarifu' ila 'kujifurahisha na hili ama lile kwa wakati'; haya ni mambo ya kujichagulia...

ALRIGHT, Simba, 'Ninachangamsha Jamvi'--Ukiona nazidisha sana kupilitiliza mipaka, sema!
Unavoongea umenikumbusha Profesa Palamagamba.

Kufunguliwa mcho ni zaidi ya macho haya tunayotazamia.

Kilichokusudiwa zzaidi na nilichokigundua baadae ni kuongezewa ufahamu ili kua na muono mpana usio na mipaka ya kufikiri.

Siku moja Babu yangu aliniuliza, unaona ukuta huo mbele yako? Nikamjibu, babu si huu hapa, nauona. Akanambia, macho yako yakifunguka utaweza kuona mpaka vilivyo nje na mbali sana ya huo ukuta.

Nakiri nilkua sikumuelewa mpaka miaka mingi sana baadae. Sasa nafahamu kua upeo wa muono wa binadam, mipaka yake anajiwekea mwenyewe.

Au ni Palamagamba kwa ID za JF?
Simba.
 
Hapana huyu mose sio robot wala sio binadamu ni kiumbe mwingine kabisa.
Lugha yake inadhihirisha hivyo
Ni mtu mwenye muono mpana tu. Kutokueleweka ni jambo alilolizoea mpaka kaelewa kua wapo wanaomuelewa.
Simba.
 
Yaani napitia posts mpaka nacheka peke yangu. We bi FF ni mtata sana.

Punguza ukali, kua mpole. Arsis na wewe anakusifu sana, sio Sheikh Mittoga tu. Lakini mimi nakwambia poa (cool down) bi FF.
Simba.
Kwa mujibu wa Wakristo.

Wakristo habari za Majini sio rafiki kwetu.
Tunazisoma tu ili kupata elimu mpya ya viumbe tusiowaona ambao kwa asilimia 100 ni maadui zetu.

Hatuwezi kuchukua habari inayosemwa na Jini kuwa ni habari Njema kwakuwa imetokana na tendo la dhambi.
Jini anaweza akaagua na kusema jambo sahihi lakini kuagua ni dhambi katika imani ya Kikristo.

Ila habari zote zinazo mhusu Binadamu ni habari Njema ziwe mbaya au nzuri, kwakuwa tumeambiwa mpende jirani yako kama nafsi yako.
Kwetu Jini hawezi kuwa Jirani wa kumpenda na kumwamini, kwanza hatumwoni.

Wengi wanasema Kuna Majini wa Kikristo.
Hiyo habari sio ya Ukweli na hakuna ushahidi wowote popote wa kimaandiko kuthibitisha hiyo habari.

Katika vyanzo vya Wakristo hakuna Nabii aliye wahubiria wala kuwashirikisha Majini katika maswala ya Dini na Ibada.
Kama Majini Wana Dini basi tunaamini Wana Manabii wao wa Kijini, na Nyumba zao za Ibada za Kijini.

Hivyo kwa mujibu wa sisi Wakristo wenyewe na kwa kuambiwa na Manabii wetu,
Majini wote ni maadui zetu na Binadamu wote ni Marafiki zetu bila kujali matendo yao kwetu.
 
Kwa mujibu wa Wakristo.

Wakristo habari za Majini sio rafiki kwetu.
Tunazisoma tu ili kupata elimu mpya ya viumbe tusiowaona ambao kwa asilimia 100 ni maadui zetu.

Hatuwezi kuchukua habari inayosemwa na Jini kuwa ni habari Njema kwakuwa imetokana na tendo la dhambi.
Jini anaweza akaagua na kusema jambo sahihi lakini kuagua ni dhambi katika imani ya Kikristo.

Ila habari zote zinazo mhusu Binadamu ni habari Njema ziwe mbaya au nzuri, kwakuwa tumeambiwa mpende jirani yako kama nafsi yako.
Kwetu Jini hawezi kuwa Jirani wa kumpenda na kumwamini, kwanza hatumwoni.

Wengi wanasema Kuna Majini wa Kikristo.
Hiyo habari sio ya Ukweli na hakuna ushahidi wowote popote wa kimaandiko kuthibitisha hiyo habari.

Katika vyanzo vya Wakristo hakuna Nabii aliye wahubiria wala kuwashirikisha Majini katika maswala ya Dini na Ibada.
Kama Majini Wana Dini basi tunaamini Wana Nabii wao wa Kijini na Nyumba zao za Ibada za Kijini.

Hivyo kwa mujibu wa sisi Wakristo wenyewe na kwa kuambiwa na Manabii wetu,
Majini wote ni maadui zetu na Binadamu wote ni Marafiki zetu bila kujali matendo yao kwetu.
Sheikh Mittoga nimekuelwa sana. Lakini nadiriki kusema hujaielewa maana ya jini au majini.

majini ni vumbe visovyoonekana mpaka imefikia kuna baadhi ya watu wanagfikiri jini alikua malaika.

Kuna viumbe vymba na viovu visivyoonekana. Mfano. unasikia mtu anaitwa "genius" kwa kufanaya mambo yake kiutalaamu wa kipekee, hio :geni" ni jini. Yaani genius ni mtu mwenye msaada wa kiumbe kisivchoonekana. Katika Uislam tunasoma sifa za Qareen, Rouhan, Khadim na mengineyo, yote nimkatika jamii ya visivyoonekana, inaweza kua hivyo ndi o majini wazuri.

Pia tunasoma mashetani wapo katika majini na watu.

Usichanganye na mashetani majini, utakua huitendei haki elimu yako.

Ni somo pana sana, lakini kioa tunavyoendelea kusomeshana hapa, tutaelewana kidog kidogo. Elimu ni bahari.
Simba.
 
ni kweli mose yeye anacopy na kupest na kiswahili chake cha google inaonyesha hata yeye hana hajualo mfano hata ukimuuliza swali hajibu yeye bali anauliza AI akijibiwa huko ndo anacopy na kupest hilo jibu la AI maana kiswahili hakieleweki hadi mtu unajua AI ndo imejibu sio yeye..bora aache kucopy tu hiyo AI au afanye summary haoni kina Arsis na Lidafo wanavyoandika.!
Hio ni aina moja ya kujipatia elimu, mimi naamini anaelewa anachpkifanya na anachokiandika, iwe kimetoka AI au poopote. AI si progamu iliofanywa na watu ijiendeshe yenyewe?

Kama vile zamani kuna saa za automatic, na nyenzo nyingi tu za aotomation, za enzi na enzi, hayajaanza leo hayo. Chukulia AI ni nyenzo tu ya kutusaidia kufanya mambo yetu, vipi tutaitumia ni tatizo letu sio wa wanaofanya hizo programu.

Mfano simu zetu za mkononi leo hii, yupo anaeitumia kwa betting, yupo anaeitumia kwa kutazama maasi, misambwanda, yupo anaeitumia kujisomea. Tupo sisi muda mrefu tunatumia kuingia JF.
Simba.
 
Sheikh Mittoga nimekuelwa sana. Lakini nadiriki kusema hujaielewa maana ya jini au majini.

majini ni vumbe visovyoonekana mpaka imefikia kuna baadhi ya watu wanagfikiri jini alikua malaika.

Kuna viumbe vymba na viovu visivyoonekana. Mfano. unasikia mtu anaitwa "genius" kwa kufanaya mambo yake kiutalaamu wa kipekee, hio :geni" ni jini. Yaani genius ni mtu mwenye msaada wa kiumbe kisivchoonekana. Katika Uislam tunasoma sifa za Qareen, Rouhan, Khadim na mengineyo, yote nimkatika jamii ya visivyoonekana, inaweza kua hivyo ndi o majini wazuri.

Pia tunasoma mashetani wapo katika majini na watu.

Usichanganye na mashetani majini, utakua huitendei haki elimu yako.

Ni somo pana sana, lakini kioa tunavyoendelea kusomeshana hapa, tutaelewana kidog kidogo. Elimu ni bahari.
Simba.
Mimi sijachanganya na kusema Majini ni Mashetani.
Nimesema Wakristo hawana Ushirika na Majini katika mambo yao ya Ibada na Imani na Dini kwakuwa hawajaambiwa popote na Manabii wao wawaone Majini kama viumbe wa kuwaamini kuhusu habari na matendo yao.

Kiumbe pekee asiyeonekana anayeaminiwa na Wakristo kama akileta habari fulani ni Malaika.
Malaika walimtokea Lutu kule Gomora na kumpa habari pia
Malaika Gabrieli alimtokea Bikira Mariamu, na wengine na kuwapa habari toka kwa Mungu.
Ila hakuna mahali katika Ukristo Jini alimtokea mtu na kumwambia jambo lolote la maana kwa idhini ya Mungu.

Wakristo habari za Majini wema na wabaya tunazisikia kwa Waislamu tu basi.
Majini kama viumbe wa Mungu tunaamini Wana Dini yao na Mitume wao wa Kijini na hatuna habari nyingine kwenye vyanzo vyetu.
Nadhani hapa nimeeleweka vyema kabisa.
 
Kwa mujibu wa Wakristo.

Wakristo habari za Majini sio rafiki kwetu.
Tunazisoma tu ili kupata elimu mpya ya viumbe tusiowaona ambao kwa asilimia 100 ni maadui zetu.

Hatuwezi kuchukua habari inayosemwa na Jini kuwa ni habari Njema kwakuwa imetokana na tendo la dhambi.
Jini anaweza akaagua na kusema jambo sahihi lakini kuagua ni dhambi katika imani ya Kikristo.

Ila habari zote zinazo mhusu Binadamu ni habari Njema ziwe mbaya au nzuri, kwakuwa tumeambiwa mpende jirani yako kama nafsi yako.
Kwetu Jini hawezi kuwa Jirani wa kumpenda na kumwamini, kwanza hatumwoni.

Wengi wanasema Kuna Majini wa Kikristo.
Hiyo habari sio ya Ukweli na hakuna ushahidi wowote popote wa kimaandiko kuthibitisha hiyo habari.

Katika vyanzo vya Wakristo hakuna Nabii aliye wahubiria wala kuwashirikisha Majini katika maswala ya Dini na Ibada.
Kama Majini Wana Dini basi tunaamini Wana Manabii wao wa Kijini, na Nyumba zao za Ibada za Kijini.

Hivyo kwa mujibu wa sisi Wakristo wenyewe na kwa kuambiwa na Manabii wetu,
Majini wote ni maadui zetu na Binadamu wote ni Marafiki zetu bila kujali matendo yao kwetu.
Nadhani aliyekwambia kuna majini wa wakristo alimaanisha malaika wa Mungu! Nimejifunza kuamini kuwa majini ni malaika waasi yaani ile theruthi moja ya malaika waliodanganywa na shetani kisha kumuasi Mungu. Nalazimika kuamini aliposema wakristo wana majini yao yawezekana alaanisha malaika waaminifu wa Mungu! Ni mawazo yangu!
 
Unavoongea umenikumbusha Profesa Palamagamba.

Kufunguliwa mcho ni zaidi ya macho haya tunayotazamia.

Kilichokusudiwa zzaidi na nilichokigundua baadae ni kuongezewa ufahamu ili kua na muono mpana usio na mipaka ya kufikiri.

Siku moja Babu yangu aliniuliza, unaona ukuta huo mbele yako? Nikamjibu, babu si huu hapa, nauona. Akanambia, macho yako yakifunguka utaweza kuona mpaka vilivyo nje na mbali sana ya huo ukuta.

Nakiri nilkua sikumuelewa mpaka miaka mingi sana baadae. Sasa nafahamu kua upeo wa muono wa binadam, mipaka yake anajiwekea mwenyewe.

Au ni Palamagamba kwa ID za JF?
Simba.
NKNS

Hakika--kila kitu, 'dhahiri-macho' na hata pia 'Dhahiri-Kiini macho' ni 'fikara na uono' !

NOPE--si prof miye!

Unayemuona kwenye kitambulishi cha tundiko hili, kwa jina na sura, ni mimi.

Hmmm
 
Nadhani aliyekwambia kuna majini wa wakristo alimaanisha malaika wa Mungu! Nimejifunza kuamini kuwa majini ni malaika waasi yaani ile theruthi moja ya malaika waliodanganywa na shetani kisha kumuasi Mungu. Nalazimika kuamini aliposema wakristo wana majini yao yawezekana alaanisha malaika waaminifu wa Mungu! Ni mawazo yangu!
Katika maandiko ya Kibiblia hakuna kumaanisha.

Jini ni Jini na Malaika ni Malaika na ni viumbe tofauti kabisa.
Biblia inamtambua Jini kuwa ni Jini na vile vile kwa Malaika.
Hakuna Habari katika Ukristo inayoitaja Dini ya Malaika.
Usichanganye habari.

Kama Kuna Majini wamebahatika kuwa Waislamu hizo ni habari za kwenye Qurani na Waislamu.
Mimi kama mimi sina cha kuongeza.
 
Katika post za nyuma au comments nilisikia habar za moto wa jahannam,,huu moto wetu wa duniani uwe mara saba zaidi ndio ukali wa huo moto wa jahannam

Na huo moto unaambiwa unasaza na hauchi kitu,sifa yake nyingine kutokana na ukali wake ni mweusi kwa mwonekano
 
mose funguka kiasi kuhusu "lucid dream" jukwaa lipate faida. Wataalam wa saikolijia wanasema ni ndoto ndani ya ndoto. Watu wa roho tunasema ni maekezo ya viumbe visivyoonekana.
Simba.
NIMELICHUKUA SHAURI

Ahsante,

Kubwa kuliko yote na tena 'Mpango Mzima' ni wanajamii ya Watanzania kufahamu, kuliishi na kulidhihiri kusudi la 'Mwenge wa Uhuru'--hili kusudi lililo kubwa kupita yote.

Mengine yatafuatia; kwa kuwa haya yote yanayoendelea, hata katika huu uzi, ni 'Sehemu ya Mchakato' wa 'Kuwaotesha watu ndoto Hai'...

Siku za mbele, hili likifaulu kwa idadi fulani ya wanajamii kuwa ni 'Wenye Kujitambua ilivyobora', tutakuwa na taasisi zitakazoitwa 'Vituo vya Utamaduni'; humo ndiyo haya yote yatafundishwa kwa watu wote wanaopenda na kutaka kuyafahamu mambo yaliyositirika ya 'Nuru ya Ufahamu'...

Hmmm
 
Kitu kingine cha kujifunza hapa wasomaji wa huu uzi,tukubaliane kutokukubaliana kwa baadhi ya mambo tu na wala haipunguzi ukweli wa mambo,yaani ukweli utabakia kuwa ukweli tu,ila kwa kuondoa ubishani tukubaliane kutokukubaliana

Mfano mtu anasema malaika waliasi,mtu kama huyu ni kumkubalia tu lkn ukweli unajulikana,mtu anasema imani fulani haitambui uwepo wa viumbe fulani ni kumwacha tu aamini kwa yale ambayo yanafurahisha nafsi yake ingawa ukweli ni tofauti na matamanio yake

Tuendelee kujifunza zaidi

Asante
 


Umenikumbusha;

Q 26:88. Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.88
89. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.89

Simba.
LITAFAKARI KWA KINA HILO TUNDIKO SIMBA...

Lina ufunguo fulani ya kheri kwako wewe kama 'mtu'...

Hmmm
 
Katika post za nyuma au comments nilisikia habar za moto wa jahannam,,huu moto wetu wa duniani uwe mara saba zaidi ndio ukali wa huo moto wa jahannam

Na huo moto unaambiwa unasaza na hauchi kitu,sifa yake nyingine kutokana na ukali wake ni mweusi kwa mwonekano
Yani Mungu akuumbe halafu akuchome moto? Wewe unaweza kumchoma moto mtoto wako? Siamini hili.
 
Ile kuchukua dizeli na kutaka kumpaka ni nia tosha kabisa, hakuna cha kunuia wala kusema. Kama unajua Qur'an unasema dua hii "Bismillahil-ladhi la yadurru ma'as-mihi shai'un fil-ardhi wa la fis-sama'i, wa Huwas-Sami'ul-'Alim".

Itafute maana yake kwenye mtandao.
Simba.
GOOGLE Translate: Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mgawanyi wake hageuki katika mambo, wala hachagui, wala hashughulikii Jina la Mwenyezi Mungu.”
 
Tukashuka, swahiba mtoto wa Sheikh. Mtoto wa Sheikh aliikua ni kijana wa mjini kabisa Unguja, hakua amezubaa na mambo ya mjini anayafahamu kweli kweli kwa mtazamo wangu, ni kama kijana yeyote wa mjini Dar. Mfano kijana aliezaliwa na kukulia Ilala Dar huwezi mfananisha na kijana alie zaliwa na kukulia Kimara au Gongo la mbpoto Dar.Wana tofauti za muono na mpaka za maongezi.

Huyu alikua kijana wa katikati ya jiji la Unguja. Alikua amesoma vizuri kwa viwango vyetu, na alikua amesomea fani yangu ya umeme wa magari. Alienda chuo cha ufundi cha serikali Unguja kafaulu vizuri akaenda DIT Dar akafanikiwa kupata shahada yake ya mwanzo. Hivi alipo Unguja ana 'duka lake" mwenyewe, karakana yake ya umeme anaiita duka. Kwa kua licha ya kua fundi umeme wote kuanzia magari pikipiki mpaka majumbani, pia alikua anauza na kutengeza laptops na PCS aina zote. Alikua maarufu sana Unguja, hilo utalijua kwa simu zake ambazo, mara nyingi nimeona akiwa na mimi anaiweka simu silence na hapokei akiendesha.

Kufika to hoteli nikachukua kadi yangu ya mlango rresepshen nikamwabia karibu uvione vyumba vya hii hoteli, hujaviona wewe. Akanambia poa. Tukingia ndani. Akasema ni vizuri nimependa hii art ya Kizanzibari ya vigtanda na makochi humu ndani. Hata dirisha naona ni asrgt ya Kizanzibari iliowekwa kissa zaidi. Wamepatia sana.

Nikamwabia si hata Menejea umemuona ni Mzanzibari? Nimemuona, namjua yule Unguja, toka mimi bado mdogo sema ndio alipotea miaka kuibuka kaibukia huku
Mimi: ndio maisha.

Tukatoka nikamwabia twende pale beach saa hizi pazuri sana. Tukaenda kiukaa tunatazama beach, nikaagiza kahawa tukaletewa. Huku tunakunywa kahawa...
Swahiba: Simba hebu nielezze, juzi nimekupeleka kwa yule Bi S. lakini nimeona toka umekuja kwa Sheikh maongei yenu yamelenda sana vibuki, saa zingine mpaka mnaenda kuongea siri. Mna siri gani na vibuki wewe naSheikh? Au swahiba umepata jiko la pili huko?
Mimi; hapana, labda Sheikh anataka kukupatia wewe mke huko? Tukacheka wote.
Swahiba: Unajua leo ndio mlikua wazi kuonhgea mbele yangu mkaongelea Dokta, unajua mimi namjua huyo Dokta mnaemuongelea, yule kwao ni karoibu kabisa na pale kwetu sema siku hizi wamehamia Mombasa lakini mjomba yao bado yuko pale, ni maarifu sana na mkewe ni maarufu sana kupita kiasi.

Mimi; Huyo Dokta ndie alifanya nije kuwatemmbelea Unguja. Babu yangu ni swahiba sana na Sheikh, nadhani nia yao yule binti nimuoe, wameona njia ya kumsaidia ni kuolewa yule, kwani ana mambi ya kwao huko ya vibuki.
Swahiba: Yule usimwache wala usikatae, yule mtaani hapa wote wanamjua wanamsigfu ile mnbaya, yule unaa,biwa toka shule ya msingi mpaka anaenda chuo hajawahi kuchukua namba mbili. Yule mpaka serikali inamtambua uwezo wake. Yule kishapewa ofa na serikali hapa mara kibao lakini sijui chuo kikuu gani huko cha Marekani ndio kimemzuia, kimefungulia ofisi Dar na hapa anakuja sana yule kiazi, akija lazima aende kwa mjombake pale jirani yetu, kwao sasa yule ndio mwembe ladu orijino. Yote ni Kikwjuni lakini kwao pale ndio mwembe ladu.

Mimi; Sasa mwamaba umenitisha na watu wa kibuki hawa, mimi siyawezi, kua mume mwenza na wanaume wenzangu mwamba?
Swahiba; Yule msomi hayuko hivo labda wamemrpga ndio anakwend kutafutaytiba, maana kasomewa dua na Sheikh nyumbani, kila akija Unguja anakiuja japo siku mpoja kusomewa rokia.
Mimi: Mwamba kwanini humuoi wewe, ukimwambiaSheikh ni kama kusukuma mlevi.
Swahiba; Mimi mkubwa sana kwangu yule usimuone vile, simpati hata kwa dawa, yule kaolewa mimi niko primary.
Mimi: Kwani umei ni nini bwana Mbina mtume mke wa kwanza alikua mkubwa sana kwake?
Swahiba; Yule nipo tayari kumuoa hata sasa hivi, mwabie Sheikh na wewe nakupoa kazi mnipelekee posa kwao. Usiondoke kesho mnipelekee posa.
Mimi; Ongea na Sheikh hata kwa simu akikubali tupeleke posa mimi navunja safari.
Swahiba: Ongea na wewe Sheikh, mimi nikimwambia yule mzee atanitolea njiani, wenyewe washaniwekea kinbinti hicho hivi wanangoja kimalize chuo tu, wanisukumie.
Mimi; Wakusukumie tena?
Swahiba: Si unajuamke wa kupewa hujaongea nae hata siku moja, wazee wanasema tu, si ndio kusukumiwa huko?

Mimi; Ngoija swahiba, naona wewe una hamu wya kuoa, lakini huyo mtoto anakuchelewesha mpaka amalize chuo.


Nikachukua simu yangu nikapoga namba ya hoteli nikwaambi mimi fulani nataka kuongea na Meneja. wakaniunganisha nae.
Meneja: Nimerudi nipo hapa na swahiba yangu tunapiga kahawa beach hapa.
Menje; Njooni, njooni haraka, watanibaka huku.

Alivoonge mapaka mimi nkacheka.

Mimi; Mwaba twende nikakupe mke sasa hivi, huyo hurushi kabisa, umei wako, msomi. toto, toto kweli, sema ndio hao vibuki, usiseme sijakwambia, Huku tunaenda kwa meneja.
Swahiba; Tukatie macho Nuru, hawa vibuki bila kuwajua wana mambo makubwa, hao Sheikh sijui?

ulipogika kwa Meneja walikua kwa ndani, lakini Meneja naona katuona kwa dirishani tunavofika, akafungua mlango wa nje.

Meneja; Karibuni karobuni, mwamba hujaonekana tena? Hujaipenda hoteli yetu?
Swahiba: Nimeipenda sana sema mashughuli mengi na Simba hataki kuniita nije kumchukua.
Meneja: Jamani, mijimama ilikua inacheza nyimbo za mduara, maana kuna mziki mnene kwa Meneja, sio kawaida. H2 na T walikua wamejifunga kanga kinoni walipotiuona, wakazifungua.
H1; Simba, na usingetrudi leo, kesho usingeaondoka Unguja hii, umeleta ji handsome lingine?
Sh; Usijidai biutre mwache mtoto wa Sheikh... huyu fundi wangu huyu wa laptop yangu.
Meneja; Bwana wewe fundi wa computers?
Swahiba: ndio kazangu, si unamsikia bi Sh hapo, mimi electrical na electronidcs zpte kasoro mambo hya simu tu siyapendi, maana simu raha yake uwe na duka la simu, sio kutengeza tu.
Meneja: Unajua kuzitengeza?
Swahiba; Naijua lakini sijabobea huko kwa hio sina uazoefu nazo lakini ni simple, basics ni zile zile, hazina ugumu wowote kutengeza kwa kwake.
Meneja: Tukimaliza hapa tutaongea kazi.

Nikaona swahiba kamkodlea macho kila dakika anamytazama T. Meneja yiko sharp sana.
Meneja: Huyu boi Sh mnajiana, huyu hapa boi H na huyu Bi H, hawa wametokea Dar. Na huyu hapa Malkia T. huyu wa hapa haa Unguja mjini.
Swahiba; Mimi nafahamu sana mpka kwao, labda yeye hanifahamu.
T; Sura zako sio ngeni kabisa. Kwama wa Unguja nitakukumbuka tu si unajua saa hizi kukumbiuka shida huku anaonesha chupa za vinywaji.
Swahiba: Ukipenda nitakukumbusha.
Meneja; Twendeni nje, hapa mziki huu una kelele umenizbua masikio, halafu Simba anapenda kahawa yake bila kelele. Tukatoka nje, mimi meneja na mwamba, Meneja akarudoi ndani kidogo, kumbe kulikua kuna mhudumu wamemleta mdio anahudumia. Meneja akaja kukaa na sisi.

Mhudumu: Niwaletee nini wageni?
Meneja: mgeni mimi gtu hapoa, hawa wote wenyeji.
Mimi; Niletee juisi ypohyote ile fresh, hyakiwepo machiungwa nitafurahi sana.
Swahiba; Na mimi kama Simba hapo.
Meneja: Waletee na kahawa, hawa watu kahawa.

Ile tunaletewa vinywaji na mhudumu na miijimama ikatoka yote, wote wamebeba vnywaji vyuao wakkaa juu ya meza.

H1: Simba tueleze kuhusu mwenzio, usiwasikilize hawa Waunguja kama wao wanamjua sisi hatumjui.
Sh; Mkomenii kijana wa watu, hii mali yetu Unguja, hamumuoni alivyo spicey?
H1: hebu koma wewe, wacha dada zako tukiongea wewe sikiliza tunataka kusema nini. Sikiliza kijana, mimi ulivyotaja wewe fundi computers ndio nimekua interested, mimi nazileta sana laptop used kutoka Marekani na Uingereza, ndio biashara yangu kubwa Dar. Kuna soko hapa Unguja?
Sewahiba: Soko la hapa gumu sana la la[ptops, hutowez bei za hapa, watu wa bara wankuja kuchukua hapa tena kwa bei ya rehareha ya hapa wanakuja kuziuza Dar. Kuna kijana mmoja yupo Mgomeni, nampelekea sana laptos, yeye ana mtu wake hapa anamuuzi, mimi zinaletwa kwangu niweke software zile za awali na nihakikishe zinafanya kazi vizuri ndio namtumia, bei gani ananunua kwa huyo mtu sijui, mimi nazifanyia mamboi technical tu.
H1: Ndio wapo wengi wanaleta laptops kutoka huku, lakini hilo lisikutie wasiwasi, kma kunasoko huku, naweza kuzishusha mpoja kwa moja huku bila kuzilegta Dar. Kule napeleka mzigoi wao na hapa nashusha mzigo wa hapa. Umeongea la maana sana, fundi ni muhimu kua nae maanake karibu zote zinakuja hazina siftware kabisa, lazima ziwekewe na zifanyiwe marekebisho madogo madogo, mimi ndio hapo ninapoumizwa faida.
Swahiba; Kwanini?
H 1; Nawauzia watu wa jumla tu kwa sababu sina mtu reliable wakuzitia software na kuzifanyia marekebisho, watu wa jumla wanachukua hivyo wanazifanyia wenyewe halafu wanaziua.
Swahiba: Wewe ndio uko pale Kariakoo lile jengo chini wanauza matairi?
H1 ; Haswaa ndio mimi.
Swahiba: Vijana wa chuo nilichosoma dar ndio wanunuzi wako wakubwa wa jumla, hata mimi nishanunu amara mbilki kwako.
H1; Wewe umesoma DIT? Swahiba akajibu ndio.
H1; Bila nyinyi naifunga biashara. Na ukare wenu nimewawekea totpo linalowauzia lina tako hilo hata T kasingiziwa, hampindui wala hampatani.

Wote tukacheka. Njoo dar ufungue biashara ya rejareja ya laptops tufungue na duka la simu tuwe partners, inalipa sana.
Swahiba: Mie jiji lile haswa siliwezi, nimepata ofa nyingi.
Sh; Bora ubaki Mwamba, sasa wote mkihamia Dar, sisi nani atatungeneza kompyuta zetu zikiharibika?
H 1: Si mtazileta Dar?
Sh; Wewe ongea na T pale anatafuta biashra za kufanya, fungua nae duka la simu. pesa zimelala hapo hazina kazi za kufanya.
Meneja; na mimi nitawekeza.
Sh. Unaona mambo hayo? halafu wanataka kutuchukulia talents zetu zote wazihamishie bara.
Mimi: Tena mwamba ndio mke huyo, mashaallah, mabo yote yanjipa hapa hapa.
Sh: hawa Masheikh hawatutaki sisi, naogopa kusema yasiwe mengine hapa.
H 2: Mradi T ,wenyewe na Mwamba hapa wakikubaliana sisi tutasherehekea tu. Simba si tutakuja harusini?
Mimi; Tena mimi ndio bestman wake.
Sh; Unaona Meneja toto linakutoka hivi hivi unaliona.
H 1: Meneja kasema ana mchumbake na kila kitu tayari, mwache ajae huyo mzungu awe groupo letu. hatuna mzungu hivyo?
H2; Kweli hatuna labda aje kama mgeni tu, walishawahi kuja wageni wananihii hukumbiuki, wale wazungu wawili walikua wizara gani sijiu akawaleta kuwaonas(ehsa shughuli yetu kama utamaduni wa Kizanzibari.
SH; Wale wangekua wanakaa hapa wangekua members walipenda sana, maana lilikua ttamasha lile sio sherehe, watu kugtoa Dunia nzima ilikua July mwisho mwisho ile.
T; Si namimi ndio niikua siku ya kwanzaa yangu?
H1; Hswaaaa nimekumbuka sasa.

Meneja; Tuoingee ya maana sasa kabla sijasahau. Mwamba wewe ukipata nafasi njoo tuongee unafanya elecyrical works na electtronics zote? Swahiba akajibu, ndio.
Meneja; Njoo tuongee tuna kazi nyingi, sasa hivi tuna mkataba na kampuni ya Kenya ndio inafanya maintanace zote za umeme wa AC na DC, ia kitu. Wnapiga pesa nyingi sana. Bira hizo pesa zibaki kwetu hapa.
H1; Hii ndio faida ya vijana wetu kusoma. Usiiachie chance hio, Nyota ya jaa shida kuonekana, leo umeiona mapemaaaa. Umesoma dua gani ulipotoka kwenu, nifundishe na mimi peke yangu, hawa wengine shauri lao.
H2; kwanini na sisi tusiijue?
H2; Si unaona hapa, kila mmoja anagtaka kua partners na wewe na T pale kakaa kimya kama inaletwa posa tayari, ujuba wote umemuondoka, anatamani useme utamuoa. Meneja kisha mtolea nje live, bika chenga.
Meneja; Jamani sijakataa, nani atakikataa kiumbe kizuri namna hii, sema nimeshajicommigt na nimecommit mtoto watu anasoma Uislam sasa hivi. Kishaan kuujua kuliko mimi.
H1 anausome wapi huo Uislam?
Meneja; Hukohuko kwao Ulaya.
H1: Wazungu wanatushinda wite kwa Uislam siku hizi.
Sh; Unguja watalii kibao wa kizungu huwajui kumbe ni Waislam, utajuwa time za kusali, wanaingia misikitini. Na ukimuona mwanamke wa kizungu katitanda Kiunguja hata awe mtalii ujue huyo Muislam.

Meneja; Jamani kie nimefurahi mlivokuja Simba, naomba kaeni na wageni, mie napiuga raundi za kazi kidogo kama lisaa limoja nitakua nimeshatudi. Mnisamahe sana wageni.
Mimi; Poa, lakini wageni tumalizane nao habari ya ndoa ya T na mwamba hapa.


Meneja akaenda zake tukabaki na mijimama ya kibuki.

...

Hapa ndio vitimbi ambavyo na ujanja wangu wote wa Usimba sikuvitegemea. Yaani H1 akaanza...
H1; Bora Meneja alivyoondoka maana nilikua nahamu ya bangi, nyie Waunguja kama mnaogopana shauri lenu.

akatoa ganja kwenye handbag lake akawasha atakatoa zingine mbili akaweka juu ya mezo.
H1: Haya jiripueni wenyewe, mlikua mnamuogopa Meneja. Na wewe Simba hebu ongea na huyu nduguyo Meneja, saa zote yupo tense tu. Naona ukiwepo wewe ndio kidogo ana relax.

Mimi; Labda mumemtisha?

Sh; kwani vituko vidogo wamemfanyia, hii mijimama ya Dar haifai kabisa. Wanamtia ushawishi na T.

H 2: Atiwe ushawishi na nani huyu T? Huyu anayajua mambo kuliko sisi, huyu dijitali, sisi analogi, unaona vile hajaolewa tu ndio unamuona mtoto sana asieyajua mambo?

Sh; Mwacheni T wangu jamani, juzi mmemsukumia Meneja, si bahati ,mngemsukumia jitu la hovyo hovyo si angefanywa kachumbari huyu?
H1; Unajuaje walichofanyana?

T; jamani mimi nimelala sijijui, na kama amenifanya kitu si ningejua nilipoamka? Huyo gentleman. msimtie dosari mwana wa watu jamani. Yeye kazi tu, utafikiri wote sisi hatuna kazi, mpaka anakera.

H1; Angekupagaza nao usingeona anakera, shwaini. Lala na simba au mwamba hapa uone kama hujafanywa samaki.

Mimi: Mimi ndio hata kulala nae nymba moja nisingelala nae, wanasema baina ya mwanamke na mwanamme ni shetani. Nigelala hata beach.

H1; Mnhhh, huyu anaejidai sie kumbe ndie. Simba mwenda kimya huyu. Wachezeeni na hawa basi kama hawajawa firimba hapahapa.
H2; Alieanzisha kumchezea Meneja si wewe, sisi tumeunganisha tu.

Wakati tunaongea, tukasikia hodi hodi kwa mbaili, kutazama chini kidogo ni yule Dada wa Kikenya anaekaa kaa resepshen kwa nje.

Mimi; Karibu dada Martha.

H1: hata majina ushawajua halafu unajidai ungelala beach, mtazame macho yake. Kama wewe mwema sana kingekushinda nini kujizuia hata ulale beach?

Mimi:; Si majina yao yapo kifuani wote, wanabeji za kushona zina nembo ya hoteli na majina yao.

Martha;Mr. Simba, nimetumwa hii note na Meneja. Martha akanipa kikaratasi.

H1: Si unaoana wanaongea kwa vi note.

Nikampa ki note yeye H1, kisome hiki, meneja kafanya heshima sio kumtangazia kila mtu.

H1; Sh Kisome mwenyewe chako hiki akampa kile kinote bi Sh.
SH; Ningeshangaa.
T; Nini tena Sh?
Sh; Mume wangu kaja ndio nimeitwa niende.
H1; Haya katoe upwiru mwanetu, ukihitaji msaada tuko hapa.

Sh; msaada wa nini? Wewe nakuachia mwamba na simba hapo, ushindwe mwenyewe. We binti ningoje twende wote.

Sh akaingia ndani kuchukua handbag lake naona kaingia na msalani maana kachelewa kama dakika kumi au zaidi ndio katoka.
H1: Nyoo, umeenda kuiosha, unajua kaja na .... mkononi.
Sh; T Nipeleke basi.
T; Ngoja na mimi nniingie ndani kidogo.

T hajachelewa kama dakika tano katoka. Wakaondoka na Sh na Martha. Tukabaki mimi, Swahiba na mijimama ya Dar.

H1; sasa nyie jamaa zenu wa Kiunguja washaondoka, pigeni ganja, pigeni whiski tunyanduane. Tena mie wangu hyu Mwamba wa Kiunguja. Nimuwahi kabla hawajaoana na T.

Mimi: Duh na harusi tayari?

H1; Wewe ishara huzioni, humuoni T alivyotulizana, kuja mwamba hapa, hata glass ya wine hajainyanyua kupeleka mdomoni, amkose mtoto wa Sheikh? Swahiba ikamtoka...

Swahiba: T mzuri kweli, tena toka mdogo namwania kweli lakini...
H1; Lakini nini? Usimtie walakin mtoto wa watu.
Swahiba; Sio hivo, huyo ana mashetani ya kibuki, siyawezi mimi.

H1; Bora Sh alivokua hayupo, maana huyo yakitajwa tu yanapanda.
H2; Huyo sio yanapanda, tuko nayo hapa muda wote, saa zingine anaekunywa hapa wala sio yeye ni vibuki. Hamumuoni anakunywa kuliko sisi wote halafu halewi?
H1 kweli nilikua sijalitazama hilo.

Mimi; Kwani mashetani ya kibuki yanalewa?
H1: Muulize huyu swahiba yako alielianzisha.
Mimi;Swahiba lete habari zao.

Swahiba; Simba, mimi sina ujuzi nao zaidi ya kusikia tu. Tunasikia vibuki bila whisky hawapandi na ni watu wenye fedha ndio wanawaweza maana shughuli zao nasikia michango yake kwa mamilioni.
H1; Enhee, endelea na sisi tuyajue.
Swahiba; Msije mkapandisha vibuki hapa, si ndio nyinyi watu wa vibuki.

Mimi; Haya jamani, tuache hayo tuendelee mengine. Hakuna raha kama kuogelea baharini saa hizi, hakuna jua. Twendeni tukaogelee.

Swahiba: Simba, huku hapafai kabisa kuongelea si mchana si usiku.
Mimi; Kwanini?

Swahiba: Hii bahari ya huku sisi toka wadogo tunaambiwa tusije kuogelea wala picnic, kuna vibwengo kibao huku.
Mimi: Ndio ni hivo?
Swahiba: Simba wewe umesema tuyaache haya mambo, wewe unayajua zaidi yangu, mie na uhakika huo. Tuyaache tu.

Mimi; haya tuongee biashara sasa.

Swahiba; Unajua dunia ndogo sana, kweli milima haikutani binadam wanakutana. Hivi Bi H1, wewe ndio pale kwa Bin Sulum juu unaeuza laptops?
H1; Ndio mimi huamini?
Swahiba: Unajua mimi nishanunua sana laptop, tukikua hatukosi pesa za matumizi, tunanunua, yule dada dukani, antwambia chagueni hapo kwenye hilo boksi yupo snmart huyo hatoi boksi lingine mpaka lile liishe, mtachagua wee mwisho mtaria zilezile mlizoweka pembeni, lakini mali ya Ulaya ni ya Ulaya tu, zipo bomba sana zile. Tmeziuza sana baada ya kutoa software labda na mtu mwenyewe akitaka anaongeza memory kidogo au harddisk ndigo tunamwekea kubwa. dah Bi H; Uliyanya maisha yetu kua mepesi sana Dar. Nikupe siri?
H1; Mwaga tu siri leo tuzijue.

Swahiba: Unajua DIT nzima kila mwanafunziw akawa anatumia laptop zako, wanafunzi wengi, karibia wote wamekuja kusoma pale hawana laptop kabisa na masomo ya komputa utasomaje? Lab ya chuo ilikua na komputa desktop kumi sijui, hazitoshi kabisa, mpaka ilikua watu wanahonga kupata nafasi kwa msimamizi wa lab. Dah, wewe ukawa muokozi wetu.

Sema siku za mwanzo wale vijana walioanza kupajua kwako waliwagonga bei watu. Halafu kuna walimu wajinga wakataka kuzuia kila mwanafunzi kua na laptop yake, eti kwa kua wao hawana. Ujinga mtupu. Tukafanya mgomo baridi mpaka waziri mdogo wa elimu akaja pale, pale kuna watu wa usalama kibao, walipelka habari faster, alipokuja naibu waziri ndio ikawa ruksa mtu aje na laptop hata kumi, na walimu wote wakapewa laptops mpya mpya za kutoka maduka ya wahindi huko.

H2; Sasa wizarani kwani wajinga, si wameshaona wajipigie kamisheni zao.
Swahiba; Tena wameletewa mabomu afadhali ya zetu za used. Unajua komputa kila unavyoitumia ndio inakua bora zaidi.
Mimi; Hilo wife wangu kawahi kunambia, yeye alikua anakuja kufundisha part time mambo ya software pale DIT.
H1: Wewe isiwe mkeo ni Nisha?
Mimi; Ndio yeye huyo.
H1; Kumbe wewe ndio Risha?
Mimi; Ndio.

H1; kweli dunia ndogo, kile ndio kifaa kinachotegewa kwa software Tanzania nzima kama ulikua hujui. Mpaka kesho. Yule ikiwashinda wote hawa software au hawajui software gani kwa kazi ipi, pale ndipo mwisho wa matatizo. n-Namjua sana tena sana. Sasa kifaa cha Kitanga kile kwanini hukuja nacho huku?

Mimi: kakataa mwenyewe, ana kazi na kule sasa hivi ana hizo kazi za masoftware zimemshika shati.

H1; Mimi nawajua basi mpaka mamako na babako, kumbeeeee. halafu hautujui vibuki na mishetani yenu ya Kisimba ya kidigo huko? mamako mbona kila mtu anamjua, yule mwanamke wa shoka, si mchezo. Mlitufanyia vituko nyinyi harusi yenu, sijui mpoje wa Tanga, ukaenea uzushi Dar nzima.
Mimi; Upi tena huo?

H1; Si mlivumishwa mmeoana mtu na dadake.
H2; Kumbe ndio huyu? Eeeh ilikuaje.
H
1; Watanga hawa bwana, walilelewa pamoja tu kama ndugu lakini ni watoto wa mjomba na shangazi. Watu wazushi tu.

Mimi; Kweli lakini, sio watu tu, hata kwangu ilikua ngumu sana. Mimi miaka yote najua yule dadangu kabisa, nimeambiwa kabla ya harusi tu. Yule mke wangu ni mtoto wa Shangazi yangu.
H1: Unamjua mamake mzazi wewe H2.
H2; nani?
H1; Si yule Mwana... alikua katibu mkuu wizara ya ...
H2: ndio namjua sana, akiwepo Dar sherehe zetu hakosi, hata za kibuki anakuja lakini yeye hana kibuki yule.
H1: hawa si simba, wanajuana wenyewe mizimu yao na ya kibuki.

Sasa huyu ndio wa kumuoa T. T akiolewa na huyu kafika, hana ujanja kabisa hapa kwa Simba. Huyu mamake Simba, simba kweli sio mchezo. Tena Simba ukimwambia mamako umeonana na sisi atafurahi kweli, mpambe yule si mchezo. Mwana hayupo Tanzania ningempigia sasa hivi nimwabie tupo wote hapa.

Mimi; Huyu mwamba muozeni T halafu mumtulize T.
H1; Tumtulize kwani ana nini, wakisha oana mambo yao watajuana wenyewe. Mimi nakushauri we, Mwamba usimuache huyu mtoto, ni bahati imekudondokea, hii kunywa kwake vi waini sijui kuvuta kwake vibangi wala kusikusumbue, utavi kontroli tu.

H2; Au atavizoea.

Swahiba; sasa mimi mwenyewe situmii hivyo vitu, si noma hio?

Mara kidogo akaja tena Martha. Tukamkaribisha.
H1; haya tena nani anaitwa safari hii?
Martha: Meneja anasema Mume wake Sh amewaalika chakula cha usiku kule hoteli wote mjitayarishe, baada ya one hour muwe kule.

H1; hayo ndio mambo, waamie ahsante sana tunakuja on time.
...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom