Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

ASILI YA MAJINI --2
Baada ya kuona kuwa majini wameubwa kwa moto kwa mujibu wa quran nije katika hadithi za bwana mtume muhammad swalalah alaiy wasalam.
Aisha (RA) alieleza kwamba Mtume Muhammad (SAW) alisema: "Malaika waliumbwa kutokana na nuru, majini waliumbwa kutokana na moto na Adamu aliumbwa kutokana na kile kilichoelezwa kwenu."
عن عائشة رضي الله عنه قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «خُلقت الملائكة من نور، وخُلق الجَانُّ من مَارِجٍ من نار، وخُلق آدم مما وُصِفَ لكم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
Hadthi hii ni sahihi na imepokewa na muslim, Katika hadithi hii tumeona kuwa Malaika wameumbwa kutokana na nuru , majini kutokana na moto na wanadamu kutokana na kile tulichoelezwa kwa maana hapa mtume alisha waeleza kuwa mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo.
Hivyo hakuna shaka kuwa asili ya majini ni mwale wa moto. Tuje katika melengo yao kwanini majini wameumbwa?

LENGO LA KUUMBWA MAJINI.
Imetajwa katika Quran kuwa lengo la wanadamu na majini kuumbwa ni kumuabudu Allah. Kama ilivyokuja katika quran (Adh-Dhariyat 51:56)
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ -- sikuumba majini na watu ila waniabudu.

Hapa tunaona kuwa lengo kuu la kuumbwa majini na sisi wanadamu ni kumuadu Allah, swali linakuja ikiwa ilo ndio lengo la kuumba mbona majini na wanadamu tunafanya mambo ya kumkufuru mungu nadhani umesoma katika kisa cha bwana simba mabalaa ya majini jinsi wanavyokata majii(kunywa pombe), wanavyofanya uchawi na mabalaa mengine, Kuhusu wanadamu apo bwana Battor unajua mabalaa ya mwanadamu uzinzi, wizi, rushwa, chuki, uongo, dhulma, zinaa, mauaji, kukata undugu, kusengenya, ushoga, utapeli n.k kwanini yote haya na Allah anasema lengo ni kumuabudu yeye?
Quran inajibu kwa kusema katika surah Al-Insan (76:3) ''Hakika Sisi tumemwongoza katika njia. Ikiwa atashukuru au akufuru."
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Hapo wamezungumzwa wanadamu kuwa muongozo upo na njia ni mbili tu ushukuru au kukufuru na majini pia imeelezwa katika surat jinn kuwa kuna kundi la majini lilisikia quran nalikakiri kuwaa ni ya ajabu na inaongoza katika haki na hawatamshikisha mola wao.
"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا"
Lakini pia katika aya ya 11 ya surat jiinn inasema

''وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا'' -- Na hakika miongoni mwetu wapo walio wema, na miongoni mwetu wapo kinyume na hivyo; tulikuwa njia mbalimbali.
Hapa utaona kuwa majini wenyewe wanasema kuna wema na wabaya hivyo suala linabaki kwa mwanadamu au jinn kuchagua njia ya kufuata na watakao mtwii Allah malipo yao ni pepo na watakao kufuru na kumuasi ALLAH ni motoni kama ilivyo katika quran
"قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ"
(Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam”. [Al-A’araaf: 38]

Toka nimeanza kuelezea mpaka hapa kuna mambo utagundua kuwa kwa mujibu wa uislamu:-
  • Malaika wameumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na wanadamu kwa udongo
  • Lengo la majini na wanadamu ni kumuabudu Allah.
  • Watako fanya kinyume na kumuabudu Allah malipo yao ni Moto.
Hivyo basi, Ushirikiano wowote wa mwanadamu na majini katika kumuasi Allah ni makosa na imekatazwa katika uislamu hilo halina mjadala, ni KUFRU.
Mjadala unabaki Je ni sahihi mwanadamu na majini kushirikiana katika wema mfano bwana Arsis alivyoshirikiana na Simba katika kumuokoa msukule huko unguja na mifano kama hiyo Je yafaa?
Inshaalah, Nitalieleza pia kwa kadri ninavyoelewa, Hapa hapataki muhemko maana pana mambo mtu anaweza ona yafaa kumbe haifai na mengine kuona hayafai kumbe yafaa.
Nitarudi kuelezea maisha ya majini, kuzaana kwao, tabia zao, na kubwa zaidi kwanii wanasumbua wanadamu.
Yani jini kaumbwa kwa moto alafu adhabu yake iwe Moto ...itakuwa adhabu kweli ?
 
Yani jini kaumbwa kwa moto alafu adhabu yake iwe Moto ...itakuwa adhabu kweli ?
Mbona binadamu kaumbwa kutokana na udongo, Je ukipigwa na dongo utaumia au?
Anyway, kuna maelezo zaidi kuhusu hili, kwanza unatakiwa ujue majini wameumbwa kutokana na mwale wa moto ila wao sio moto, kama vile ambavyo mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo ila sisi sio udongo.
Jambo la pili ni kuwa sifa za huo moto ambao wataadhibiwa nao majini waovu na binadamu waovu unazijua? kwakuwa quran ndio imesema majini wameumbwa kutokana na moto basi nenda katafute sifa za moto ambao majini wataadhibiwa nao kwa mujibu wa quran.
 
USHAURI UMEFIKIRIWA

Sasa, ni vema kufahamu, panapojukwaa la watu ama wanajamii wenye seti tofauti tofauti za uwezo wa 'kushughulika/kujishughulisha', kuna mambo ambayo 'huendelea' kwa minajili ya 'Ujenzi wa Ujuzi wa Mambo'.

Kwa mintarafu ya hivi, siyo kila mtu 'yupo macho' na jambo hili huchukua vipi sura yake (!)

Wakati mwingine, 'Mwenye Macho' ndiye mwenye ujuzi wa kufaragua mambo, kwa jinsi ya kawaida ama ile isiyoyakawaida.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa tabia ya upole, unyenyekevu na uvumilivu/ustahimilivu pale inapotokea nasibu ya kutano/makutano ya 'Wanaojua ilivyobora' na 'Wale wanaochechemea kiujuzi na maarifa'...

Uzi huu ni 'Jaribio la Kijamii'--Jaribio kwa ajili ya 'Utayari' wa wanajamii kukutanika na watu wenye uwezo wa kawaida na kupitiliza kawaida iliyozoeleka.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa wanajamii kutambua 'tabia zao' ambazo ni mikingamo ya kiufahamu; kuwafanya wao wasinasibike kujijengea uwezo wa ku-JUA ilivyobora.

Watu wenye uwezo wa kawaida na kupilitiza kawaida hawafikirii kwa namna za 'porojo' ama/na 'kuhorojoka'; kwa kuwa hawa wana namna ya ufikirifu uliokatika sifa na hadhi ya mbegu za u-JUA-ji.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa wanajamii kubadili tabia na mazoea ya kutumia akili zao; wafanyebidii kwa ajili ya 'namna mpya ya kuyaona mambo na kuyabayanisha'.

Wanajamii wenye kuchechemea kiutambuzi na fahamu, ni waja wenye nasibu ya 'kuhitaji kufundwa kiakili'; hili ndilo maana ya neno 'Rizayati', neno lenye asili ya kiarabu na tena lenye asili ya 'kumfunza farasi mdogo nidhamu/adabu/mazoea'--istilahi ya masufii.

Rizayati ya Elimu 3.0 ndiyo 'haja ya Maudhui' ya uzi huu; hili linahitaji nidhamu/adabu/mazoea 'Mapya'...

Si 'busara' mtu asiye na rizayati 'kumpangia' mtu mwenye 'Rizayati'; hili ndilo namna moja ya kutafsiri kwa nini 'Mtu wa Daraja/Watu wa Daraja' wanaweza kusita 'kujumuika humu'...

Hmmm
Kuna elimu unayo mkuu endelea tufaidike.
 
Kitu cha kwanza cha kuondoa, nuksi, hasda, uchawi, kijicho au chochote kile kibaya ni sala na kuacha maasi.

Kuna mdau juu hapo Mwami Atale kaelezea kidogo kuhusu mtu na muumba wake kua "connected", mimi nasema hakuna zaidi ya sala. Kuna nguvu ipi nyingine kubwa zaidi ya kua na mawasiliano ya moja kwa moja na Muumba wako?
Simba.
Nakubaliana na wewe, kuwa connected na Muumba, Kupitia experience yangu binafsi, hii nathihitisha 💯.
 
Ha ha hahichi kisa chako kimenichekesha
Ila wengi wanaweza kudhami ni utani
Majinni Wana vitimbi haswa
Ila mm nililetewa ZOGO kubwa nimemtoa bikra Binti Yao halafu sijamuoa
Nikapata misukosuko mno mpk rasmi nilipoamua kuachana na mambo ya MAJINI ila nilijifunza ELIMU kubwa mno kwao hasa kutoka kwa huyo BINTI Yao walieniambia nimemtoa BIKRA halafu sijamuo

Kwa uchache tu hii DUNIA ama ulimwengu Una layer 7 Kila JINI ana uwezo wake kwa Kila eneo lake but kama alivyoeleza mkuu Kuna Kuna layer zingine hawawezi kufika na Wala hazina umiliki wao ni layer ambazo ukifika hatuwezi kufika mpk QIYAMA
Sielezi mengi 7bu mengi yashaelezwa
Ila mambo ya MAJINNI yanavuruga haswa ukiwa against nayo na wao wamekuchagua wewe
Zaidi ukiyafuatilia sana watu wanaweza kukuona CHIZI

Nimefurahi kusoma huu Uzi una ELIMU kubwa
Sana Tena sana mno
Longer sana Arsis
Mkuu una ujuzi wowote juu ya mtu kukabidhiwa mali na mizimu ya ukoo! Yaani imekupenda na wanataka kukupa mali...nifungue kidogo
 
Mbona binadamu kaumbwa kutokana na udongo, Je ukipigwa na dongo utaumia au?
Anyway, kuna maelezo zaidi kuhusu hili, kwanza unatakiwa ujue majini wameumbwa kutokana na mwale wa moto ila wao sio moto, kama vile ambavyo mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo ila sisi sio udongo.
Jambo la pili ni kuwa sifa za huo moto ambao wataadhibiwa nao majini waovu na binadamu waovu unazijua? kwakuwa quran ndio imesema majini wameumbwa kutokana na moto basi nenda katafute sifa za moto ambao majini wataadhibiwa nao kwa mujibu wa quran.
Sasa huyo alieandika kuran huo moto waliutest vipi ?
Nataka kujua hizo sifa za huo moto na aliutest vipi ?
 
Mbona binadamu kaumbwa kutokana na udongo, Je ukipigwa na dongo utaumia au?
Anyway, kuna maelezo zaidi kuhusu hili, kwanza unatakiwa ujue majini wameumbwa kutokana na mwale wa moto ila wao sio moto, kama vile ambavyo mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo ila sisi sio udongo.
Jambo la pili ni kuwa sifa za huo moto ambao wataadhibiwa nao majini waovu na binadamu waovu unazijua? kwakuwa quran ndio imesema majini wameumbwa kutokana na moto basi nenda katafute sifa za moto ambao majini wataadhibiwa nao kwa mujibu wa quran.
Nikiona mjadala kama huu wako ndio natamani tuendelee na kisa cha Adam tuje cha majini tuje cha Isa ili tuzielewe lisan au locution zilizotumika kwenye Qur'an kwa kina.

Kuna kitu kinaitwa tashbiha au metaphor kwa Kingereza. hata katika maongezi yetu ya kila siku.

Qur'an nayo ni mama wa hilo, ukichukulia kwanza ilishushwa wakati Waarabu wanashindana kwa ufasaha (eloquence) wao wa lugha kwa ndimi (lisan) tofauti tofauti. Muujiza mmojawapo wa Qur'an ninlugha ya juu sana iliotumika.

Namaanisha kusema sio kila tunapoona binadam kaumbwa kwa udongo basi inamaanisha hivyo, wengine mpaka wanafikia kufuru sijui akauchukua udongo wa kila sehemu akaufinyanga akaumba mtu! yaani wamefikia kumfanya Mwenyezi Mungu ni mtengeza vinyago vya iudongo, Astaghafirullah, wakati mwenyewe anasema yeye husema kuwa inakuwa (kiun fa yakun). Na kuzaana kwetu kakuelezea kwa kina kwenye Qur'an, ni muingilano wa mke na mume. hakuna zaidi.

Hali kadhalika tukisoma kaumbwa kwa moto, tuelewe maana yake nini?

Hilo Natanabahisha tu ni somo kamili. Nipo tayari kuulizwa chochote kuhusu hilo.
Simba.
 
USHAURI UMEFIKIRIWA

Sasa, ni vema kufahamu, panapojukwaa la watu ama wanajamii wenye seti tofauti tofauti za uwezo wa 'kushughulika/kujishughulisha', kuna mambo ambayo 'huendelea' kwa minajili ya 'Ujenzi wa Ujuzi wa Mambo'.

Kwa mintarafu ya hivi, siyo kila mtu 'yupo macho' na jambo hili huchukua vipi sura yake (!)

Wakati mwingine, 'Mwenye Macho' ndiye mwenye ujuzi wa kufaragua mambo, kwa jinsi ya kawaida ama ile isiyoyakawaida.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa tabia ya upole, unyenyekevu na uvumilivu/ustahimilivu pale inapotokea nasibu ya kutano/makutano ya 'Wanaojua ilivyobora' na 'Wale wanaochechemea kiujuzi na maarifa'...

Uzi huu ni 'Jaribio la Kijamii'--Jaribio kwa ajili ya 'Utayari' wa wanajamii kukutanika na watu wenye uwezo wa kawaida na kupitiliza kawaida iliyozoeleka.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa wanajamii kutambua 'tabia zao' ambazo ni mikingamo ya kiufahamu; kuwafanya wao wasinasibike kujijengea uwezo wa ku-JUA ilivyobora.

Watu wenye uwezo wa kawaida na kupilitiza kawaida hawafikirii kwa namna za 'porojo' ama/na 'kuhorojoka'; kwa kuwa hawa wana namna ya ufikirifu uliokatika sifa na hadhi ya mbegu za u-JUA-ji.

Hili ndilo linalolingania umuhimu wa wanajamii kubadili tabia na mazoea ya kutumia akili zao; wafanyebidii kwa ajili ya 'namna mpya ya kuyaona mambo na kuyabayanisha'.

Wanajamii wenye kuchechemea kiutambuzi na fahamu, ni waja wenye nasibu ya 'kuhitaji kufundwa kiakili'; hili ndilo maana ya neno 'Rizayati', neno lenye asili ya kiarabu na tena lenye asili ya 'kumfunza farasi mdogo nidhamu/adabu/mazoea'--istilahi ya masufii.

Rizayati ya Elimu 3.0 ndiyo 'haja ya Maudhui' ya uzi huu; hili linahitaji nidhamu/adabu/mazoea 'Mapya'...

Si 'busara' mtu asiye na rizayati 'kumpangia' mtu mwenye 'Rizayati'; hili ndilo namna moja ya kutafsiri kwa nini 'Mtu wa Daraja/Watu wa Daraja' wanaweza kusita 'kujumuika humu'...

Hmmm
Hakuna ubaya, ndio maana nikakwambia weka jibu au swali au comments yako kidogo weka na link ya mada yako, tutakuja kukusoma.

Maana nimeona mada zaidi ya moja, labda yote imelenga mada moja, tutajua huko utapotuwekea link.

Sidhani hapo kama kuna tatizo. Tunatakiwa tushindane kwenye mema. Elimu kwa mtazamo wangu ni kitu chema sana, sijali inatokea wapi, lakini ni muhimu tukajiwea nidhamu. Hata mashule kuna nidhamu ya vipindi, vyuo vikuu kila lecturer na wakati au na darasa alake.
Simba.
 
Nikiona mjadala kama huu wako ndio natamani tuendelee na kisa cha Adam tuje cha majinni tuje cha Isa ili tuzielewe lisan au locution zilizotumika kwenye Qur'an kwa kina.

Kuna kitu kinaitwa tashbiha au metaphor kwa Kingereza. hata katika maongezi yetu ya kila siku.

Qur'an nayo ni mama wa hilo, ukichukulia kwanza ilishushwa wakati Waarabu wanashindana kwa ufasaha (eloquence) wao wa lugha kwa ndimi (lisan) tofauti tofauti. Muujiza mmojawapo wa Qur'an ninlugha ya juu sana iliotumika.

Namaanisha kusema sio kila tunapoona binadam kaumbwa kwa udongo basi inamaanisha hivyo, wengine mpaka wanafikia kufuru sijui akauchukua udongo wa kila sehemu akaufinyanga akaumba mtu! yaani wamefikia kumfanya Mwenyezi Mungu ni mtengeza vinyago vya iudongo, Astaghafirullah, wakati mwenyewe anasema yeye husema kuwa inakuwa (kiun fa yakun). Na kuzaana kwetu kakuelezea kwa kina kwenye Qur'an, ni muingilano wa mke na mume. hakuna zaidi.

Hali kadhalika tukisoma kaumbwa kwa moto, tuelewe maana yake nini?

Hilo Natanabahisha tu ni somo kamili. Nipo tayari kuulizwa chochote kuhusu hilo.
Simba.
Somo la Adamu ungeendelea nalo inaonekana limebeba mambo mengi.
kuhusu hili la sasa la majini kuumbwa kwa moto umesema quran imetumia tashbiha katika hili tupe ufafanuzi, Inaposema majini wameumbwa kwa moto ina maana gani?
 
I ngekuwa ni hivyo basi jini bakora asingeenda kule hotelini kwa meneja kumsafishia hoteli nzima kwa mitishamba na madawa. Arsis jipange uje na majawabu
wakati mwingine Arsis anazingua yeye akiulizwa shida zinazohitaji tiba amekariri jibu moja tu "fanya ibada,sali sana acha maasi" ndo imeisha hivo inaweza jambo hana ufahamu nalo basi amwite Arsis au bakora amshirikishe hao watajua tu kwa njia zao kisha yeye simba ndo atoe majibu hapa atakayopewa na hao watu wa kazi sio kukimbilia fanya ibada,acha maasi kwani ni nani ambae hana dhambi maana wafanya ibada na sala ni wengi sana ila wachamungu ni wachache.!
 
Asante sana, nashukuru kwa Ushauri na tutafanyia kazi pia tunajitahdi kutokufanya maasi lkn kwasbabu sisi ni binadamu kuteleza kupo.

Ombi langu km Kuna tiba unaweza kuelekeza akafanya mwenyewe msaidie. Hapa namuongelea Baba wa familia watoto wanasoma haingizi hata mia anaweza kukaa zaidi ya mwaka kama mwanaume anaumia sana.....na pia iko wazi inajulikana ni uchawi wa mtu wake wa karibu. Kwa wachungaji, mashekhe kufunga nk yote anafanya

wakati mwingine Arsis anazingua yeye akiulizwa shida zinazohitaji tiba amekariri jibu moja tu "fanya ibada,sali sana acha maasi" ndo imeisha hivo inaweza jambo hana ufahamu nalo basi amwite Arsis au bakora amshirikishe hao watajua tu kwa njia zao kisha yeye simba ndo atoe majibu hapa atakayopewa na hao watu wa kazi sio kukimbilia fanya ibada,acha maasi kwani ni nani ambae hana dhambi maana wafanya ibada na sala ni wengi sana ila wachamungu ni wachache.!
au sio .mfano uende hospital unaumwa dr asikupe dawa. akwambie we kubywa maj meng .lala mapema kula matunda.
 
Kwanza wewe tu kumsomea haitoshi. Yeye mwenyewe inatakiwa awe na mwili msafi, afanye ibada, halafu ugonjwa ya kuanguka inaweza kua mambo mengi, damu nyingi, damu kidogo, tatizo la ubongo, tatizo la mishipa, tatizo la uchawi na kurogwa, tatizo la mgongo.

Kwanza anza na tiba ya kusafisha mishipa yake ya mwili mzima, Anywe mdalasini ya maji vuguvugu kila siku kabla hajala kitu alfajir na usiku kitu cha mwisho. Ale mbadala sini ya kuroweka kwenye maji ya vuguvugu na asali safi vijiko viwili kabla hajala kitu. Kikombe au glass moja tu asubuhi na moja usiku kwa siku saba tu.

Asiwache ibada. Halafu tupe majibu.
Nini nifanye kusafisha tumbo langu la uzaz ili kubeba mimba? Maana sipati mzunguko wangu vizur (nilishaenda hospital lkn tiba hazijasaisia sana)
 
Hakuna ubaya, ndio maana nikakwambia weka jibu au swali au commenta yako kidogo weka na kink ya mada yako, tutakuja kukusoma.

Maana nimeona mada zaidi ya moja, labda yote imelenda mada moja gtutajua huko utapotiuwekea link.

Sidhani hapo kama kuna tatizo. Tunatakiwa tushindane kwenye mema. Elimu kwa mtazamo wangu ni kitu chema sana, sijali inatokea wapi, lakini ni muhimu tukajiwea nidhamu. Hata mashule kuna nidhamu ya vipindi, vyuo vikuu kila lecturer na wakati au na darasa alake.
Simba.
MASAHIHISHO

Watu wa 'Maarifa' na 'Maarifu' hawana kitu kama 'Mada'...

Watu wa maarifa ni watu wenye mawazo yenyekuririka kama vile damu kwenye mishipa na vijimishipa...

Ni kitu ambacho tunaweza kukitaja kama Uono na Ufikirifu Mifumo wenye nasibu isiyo na ukomo wa kubayanisha ukweli wa mambo na mahusiano/mashahibiano ya 'Maua' ya 'Maarifa'...

Ukiona mtu wa 'Maarifa na Maarifu' anaweka mashahuri yaliyojisheheni ni kwa kuwa 'ana kusudi linaloweza lisiwe wazi kwa mtu-asiye-na- njia/mbinu' ...

Watu wa Mwangaza, kwa mfano, 'usomeshaji wao wa visomo' ni mambo ya 'mazungumzo ya Mkuu na ukaaji kitakowa Wanafunzi wa mambo ya kiroho'... Ni mambo ya mawaidha na kutega sikio, UPANISHAD--siyo kwa kuwa kwamba hadhira inalolote la 'kushindana' na 'Mtoa Mawaidha'...

Miongoni mwa jamii ya watu wa mwangaza kuna 'Masikilizano ama/na Maarifu'--Maarifu ni mambo yajayo na hisia zaidi ya tano... Hayo mambo kama kumsikia mtu lakini haumuoni, kujua fulani 'yupo' hapa lakini 'haonekani kwa macho'...

Watu wa Mwangaza huwa na u-JUA-ji mbegu ulio na asili ya 'ualama na ishara'--telepathia inawezekana kutokana na ufundi wa ufungashiaji wa nia kwenye 'ualama'... Mambo ya kuweka 'Nia' kwenye kitu -- kitu cha kusudi la kimawasiliano ya namna ya mafikara...

Halafu, ni vema ifahamike fika--binadamu kwa mazoea, bado hana uwezo wa kunufaika na 'mawasiliano' ya kimafikara kwa kheri ya daraja la juu. Hili ni kwa kuwa 'viumbe watu wa kigeni' wengi wana namna ya uakili unaochakata mambo mengi mno kwa 'fungu dogo' la 'kifungasho cha telepathia'...

Ndiyo, hili shauri la kuomba mafungu ya maarifa yaje kidogo kidogo lina namna yake ya kuchukuliwa kwa mtu wa upeo wa ujuzi wa mawazo, tabia na mwenendo wa 'mpokeaji maudhui'...

Vipi ikiwa uwezo wa wanaokusudiwa kuyasikia haya yote, kwa upande mwingine ndiyo unatengenezewa nasibu ya tanuliwa?

Anayelihisi hili kuwa ni hi hivi khasa ni bora angalikomaa kupokea chochote kile kijavyo humu--ikiwa kinakutaka sana ujibadilishe matizamo na mazoezi, basi na iwe hivyo (!) Kuna 'baraka yake iliyojificha'...

Mtu anaweza kutundika humu matundiko hata 'Alfu kumi' lakini yakipitiwa hayo na mtu wa Mwangaza ni labda 'upotezi wa nafasi wa ile nasibu ya kuwezekana kuweka yale yaliyomema/fasaha na ufanisi wa hali ya juu wa kusafirisha U-JUA-ji'--na labda hakuna ujuaji wowote hasa ila ubatili na kujilisha upepo--ashkum si matusi...

Kuwe na ustahimilifu kwa namna sizizo za kawaida za mtu kudhihiri mawaidha--siyo kwamba kwa mtu upeo na mwangaza hatambui 'cognitive dissonance--disonia ya kiutambuzi' ya hadhira--haya yote 'yapo ndani ya hesabu'

Hmmm
 
Nini nifanye kusafisha tumbo langu la uzaz ili kubeba mimba? Maana sipati mzunguko wangu vizur (nilishaenda hospital lkn tiba hazijasaisia sana)
tusubiri jibu la Arsis maana shida kama hizi hatoagi majibu ya maana yeye amekariri jibu lake la "fanya ibada,sali sana acha maasi" ndo kamaliza hivo hakupi suluhisho ya kipi ufanye ujitibu shida yako..ngoja aje
 
Sisi sio katika hao wasiokua na mada . Sisi tuna mada.
Simba.
 
Nini nifanye kusafisha tumbo langu la uzaz ili kubeba mimba? Maana sipati mzunguko wangu vizur (nilishaenda hospital lkn tiba hazijasaisia sana)
Magome ya mdalasini roweka kwenye maji ya moto, siku ya pili kiwe ndio kinywaji chako cha kwanza algfajiri na cha mwisho usiku. Iwe kawaida yako mwanzo mpaka mwisho wa mzunguko.
Sisi tujitahidi, Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua zaidi.
Usiache kusali na jiepushe na maasi.
Simba.
 
Kuna kitu kinachoweza kufahamika kama 'kufungika/kufungiwa ya kunasibika kuyajua kwa wakati'; kwa kiingereza ni mambo ya 'compartmentalization'...

Katika majukwaa kama haya, 'mada' ni jambo lenye asili ya kujiwekea mpaka wa kuyasikia na kuyajua kwa wakati; lakini vipi ikiwa 'asili ya mipaka katika kutaka/kupenda kuyafahamu kuyajua mambo' husigana na nasibu ya Ujumuifu wa 'Maarifa na Maarifu'(?)

Kwa mfano, huu uzi unajina: "niliyoyashuhudia-nilipofunguliwa macho"

Je, unatambua jambo la 'Kufunguliwa macho' lina asili ya 'Nuru ya Ufahamu, Maajabu na Mastaajabu' yake?

Ipi inaweza kuwa 'mada' katika 'Nuru ya Ufahamu, Maajabu na Mastaajabu yake' khasa?

Kiufundi, sisi sote ikiwa ni watu wa 'akili' na basi nasibu ya 'dini', adui mkubwa wa kupambana naye ni 'Kasumba' ya 'Mafungu Elimu'...

Labda iwe sisi watu hatuna mpango na 'Maarifa na Maarifu' ila 'kujifurahisha na hili ama lile kwa wakati'; haya ni mambo ya kujichagulia...

ALRIGHT, Simba, 'Ninachangamsha Jamvi'--Ukiona nazidisha sana kupilitiliza mipaka, sema!
 
au sio .mfano uende hospital unaumwa dr asikupe dawa. akwambie we kubywa maj meng .lala mapema kula matunda.
Tatizo lililoulizwa na ushauri aliopewa ni tiba kubwa sana kwa wenye uelewa

Lakini nawaelewa hilo la dawa. Matatibu wengi wenye uzoefu wa kazi zao, wanajua mgonjwa akiwa (hypochondriac), huyu ni mtu mwenye waasiwasi na afya yake kila mara. Akitokea mtu anasema anaumwa mbavu na yeye hujihisi hivyo na husema mimi mbavu siku hizi zinaniuma.

Mara nyingi hao hupewa "placebos", hio ni tiba feki tuseme, unaweza kupewa dawa lakini hazina dawa yoyote ni unga tu wa kawaida au wanakandamizwa na vitamins tu,

Vipo vidonge spesho kabisa kitaalam ni dawa za placebos.

Hufikia wengine mpaka wakafanyiwa upasuaji placebo. Kuna wengine haridhiki mpaka apigwe sindano, Madokta na manasi wanajua wanachokiandika, hawa huchomwa sindano za placebo. Mgonjwa anaingia anaoneshwa kabisa sindano inavonyonya dawa inavowekwa sawa, hata anavochomwa inakua tofauti na yule anaechomwa dawa ya kweli, huyu inatakiwa aihisi sindano mpaka agune au aoneshe ishara fulani kua imemuingia.

Watu kama huyo kisaikolojia ndio anapona hivo.

Sitaki tufikie huko, naamini watu wana shida za kweli wanaojitokeza hapa.
Simba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom