Kuna mtu aliuliza juu ya maana ya haya maneno ninayoelezea kwa mujibu wa quran nadhani ni
FaizaFoxy naendelea nilipo ishia.
AFRIT au
IFRIT - ni aina ya majini.
Katika maelezo ya Qur'ani na Hadithi,
'Ifrit ni majini wenye nguvu Wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa na mara nyingi wanahusishwa na uovu na uasi. wametajwa katika quran surat Naml aya ya 39
قَالَ عِفْرِيتٌۭ مِّنَ ٱلْجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّى عَلَيْهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌۭ
Tafsir : Akasema Ifrit Mimi nitakuletea kiti chake kabla hujainuka kutoka mahali pako, na mimi nina nguvu juu yake na ni muaminifu.’"
Katika aya hii, Nabii suleyman (a.s) aliwauliza baraza lake na tunajua nabii sulyman alipewa utawala kwa wanadamu na majini na wanyama hivyo aliuliza nani anaweza kwenda kuniletea kiti cha malkia wa sheba aliyeitwa balqis ndiyo huyu ifrit akamjibu mimi naweza kuleta kabla hujanyuka kutoka kwenye kiti chako.
Pia katika kisa maarufu cha Isra na miraj Bwana mtume Muhammad (S.a.w) wakati wapo na jibril mtume aliona kiumbe kuna wafuata mtume akamuuliza jibril ni kiumbe gani hicho ndipo jibril akamwambie mtume huyo ni Ifrit minal jinn nikufundishe maneno ambayo ukiyasema ataacha kutufatilia, Jibril a.s akamwambia sema.
بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Bismillahi alladhi la yadurru ma'asmihi shay'un fil ardhi wa la fis-sama'i,Wahuwas-sami'ul-alim":
Tafsir: Kwa jina la Allah, ambaye hakuna kinachodhuru, iwe kwenye ardhi au angani, naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua."
Baada ya mtume kusema maneno haya jinn huyu akaacha kuwafatilia hii ni dua ya muhimu na inasisitizwa waislamu kuisoma katika adhkari za asubuh na jioni.
Kwa ujumla, Ifrit ni Majini wenye nguvu na waovu, lakini siyo wote wanakuwa na tabia mbaya. Kama majini wengine, wanaweza kuwa na tabia mbalimbali na uwezo wa kuchagua matendo yao.
MALAIKA - Kwa mujibu wa Qur'ani, malaika ni viumbe wa kiroho walioumbwa na Allah kwa nuru kwa ajili ya kutekeleza amri zake na kusimamia masuala mbalimbali ya ulimwengu. Malaika wana sifa maalum ambazo zinawafanya kuwa viumbe wa kiroho tofauti na wanadamu na majini.
Sifa za malaika
- Viumbe wa Kiroho : Malaika ni viumbe wa kiroho
- Wanawajibika kwa Amri za Allah : Malaika hutekeleza amri za Allah na wanapokea maagizo kutoka kwake. Hawana uhuru wa kuchagua kama wanadamu; wao huishi na kutekeleza amri ya Allah kwa utii kamili.Sura ya 16 aya 49-50.
- Wanaweza Kujidhihirisha : Malaika wanaweza kujidhihirisha kwa watu kwa umbo maalum au kwa njia ya kiroho.
Wapo wengi sana ila kubwa zaidi kwao hawamuasi Allah wanatekeleza wanaloamrishwa tu wametajwa sana katika quran na hadithi kuna Jibril, Mikael, Israfil, Munkar, Nakir n.k na wanamajukumu tofauti tofauti na wapo wengine wao wanafanya ibada tu na kumtukuza Allah.