Ishushwe vipi wakati kwenye kitabu cha Quran kuna Torati, zaburi na injili?
Doktori doktori dah sijui nisemeje
Qur'an kama ilivyo vitabu vingine vya Mungu huwa vinadhibitisha ujumbe wa kabla yake
Mfano taurati ilidhibitisha zaburi,na injili ilidhibitisha taurati na qur'an kwakuwa ni kitabu cha mwisho kinadhitisha hayo yote kwa uchache,usitarajie au kuelewa kwamba kuna vifungu vyote hivyo,,,ntakumpa mfano
Kuna aya katika qur'an inazungumzia juu ya kufunga swaumu ya ramadhani,hapo Allaha anasema mmelazimishwa kufunga swaumu kama ambavyo walilazimishwa umati za nyuma huko
2:183
"Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu."
Kwahiyo hapo quran imekumbusha kwamba hata huko nyuma katika umati zilizo pita katika vitabu vya mwanzo watu waliambiwa wafunge swaumu
Tuje kwenye swala lingine,kwa nyakati tofauti wakristo na wayahudi kila mmoja alikuwa anwaona wenzake wamepotea na kuhangamia,sasa quran inaelezea hizo habar kudhibitisha hayo yaliyo tokea huko nyuma
2:113
"Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauli yao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitilafiana."
Kwahiyo mifano iko mingi sana,kuna aya mpaka ambazo zinaeleza namna ambavyo ibada za zamani zilikuwa zinafanyika,,kwenye taurat watu walikuwa wanasujudu kama waislamu,Yesu mwenyewe kuna kipindi alionekana amesujudu
Sijui nyinyi ibada ya kupiga magoti mmeitoa wapi?