Arsis; Swali zuri sana.
Wanatumia bila kujijua, wamekua "brain washed" na hawaelewi tofauti, kwa sababu wanafata tafsiri. Hivi visa na mafundisho ya biblia yaliingizwa miaka mingi sana kwenye tafsiri za Wur'an sio Qur'an yenyewe. Ilianza baada ya kufa Mtume Muhammad.
Mtume, hakuitafsiri Qur'an, wanamzushia eti katafsiri. Mtume hakuna aya zaidi ya 10 au ishirini ndizo alielezea maana yake. Tafsiri zingine zote ni za kutunga au kugtokea biblia au fantasy za waandishi wa tafsiri, kama alfu lela u lela tu.
Mkiependa kujua zaidi kuhusu historia ya hadithi na kuna majina makubwa ya watu wa hadithi kwenye vitabu vyao wanakiri kuna visa wamevielezea kutokana na biblia, hii ni kwa kutokujua ubora na umuhimu wa Qur'an au kwa kudhani watu wataelewa zaidi wakifanya hivyo. Na wengine ni kwa makusudi kabisa ili wapotoshe ubora wa Qur'an.
Pia mkipenda kujua zaidi elimu ya Qur'an bila kutumia hadithi za kujitungia, ulizeni maswali kama hili, yenye nguvu. Kuna njia nyepesi za kila mmoja wetu kuweza kutambua hii hadithi ya kwe;i au sio hya kweli.
Kama mnakumbuka kuna mtu kaleya mstari juu huko, kaupamba kwa Kiarabu nikamuuliza aya ipi hii? Akajibu hadithi, nikamwabia hadithi ipi hio? Hajajibu tena, sasa ananisoma kwa kunusa nusa tu. Namwambia usofanye hivyo, sio elimu hio. Kama yalikua ni maneno ya mshairi sema tu ni mshairi, kama hujui yametoka wapi na uliyasikia tu, sema hayo nilisikia tu lakini sina elimu nayo yametoka wapi.
Tuytumie hili jukwa kujua mengi sana. Ya dini, ya sayansi, ya ulimwengu. Ya dhahiri na siri za kidunia. Tusowe na jazba kama hatujui kitu au tunas shaka nacho, sisi hatuwezi kujua kila kitu, isipokua tunasema umri huongeza maarifa na busra, nadio elimu yenyewe hio.
Hakuna zaidi ya Allah na mafundisho yake.
Arsis.