The Republican
Senior Member
- Dec 5, 2021
- 174
- 308
Hehehe unachekesha sana Sasa unataka kubishana hata hati ya kiarabu huandiki, utaelewa mafhum ya HADITHI?
Inaposemwa Imepokewa kutoka kwa Fulani (rawi wa hadithi), ikapokewa kwa Fulani Amesema Abuu Hurairah Amesema Mtume S.A.W maana yake Unaelewa?
Mtiririko huu kitaalamu unaitwa Isnad, yote kuondoa UCHAFU wa kuzushwa kwa HADITHI mpya.
Muhdditheen (wataalamu wa elimu hii wako wengi) wanaogawa hadithi katika madaraja manne. HADITHI ziko katika madaraja manne
1. Sahihi- isnad yake ni ya nguvu sana na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W
2. Hasan, 3. Dhaifu 4. Maudhui.
Hebu niambie ni profesa Gani kakufundisha uongo huyo nipate kumraddi katika publishings zake na awe Discredited?
Kwenye hili Huna ujualo PhD. Tulia.
Kama hii ni PhD tumekwisha, hebu chutama.Wewe ndio hujui ulichokiandika na kama hujui omba kuelimishwa kuliko kujifanya mjuwaji.
Hadithi si maneno yote ya mtume, hadithi ni kitabu kilichofanyiwa research kwa sababu kwenye Quran hakuna biography ya mtume ndio sababu ya kuandikwa vitabu vya sunna vya hadithi na Sila na waandishi wake waliviandika mtume akiwa ameshafariki.
Labda ili uelewe vizuri ni kama unavyoona injili ya Luka kwenye biblia aliandika maisha ya Yesu kwa kuwahoji watu waliokuwepo wakati wa Yesu, au kama unavyoona Absalom Kibanda anaandika kitabu cha maisha ya Lowasa atawahoji watu wote wa karibu akiwemo JK, sasa simple logic huwezi kudanganya umma eti kuandika kitabu cha mtu aliyekufa eti yote ni maneno yake si kweli acha kudanganya watu.
Hivi vitu tunafundishwa na maprofesa waliobobea na tunasoma vitabu sasa wacha mbambamba.
Halafu twende kwa hoja Mimi nakuwekea HADITHI na ayats,
Matola, Mambo matatu ndio governing engine ya Uislamu.
1. Qur'an
2. Hadithi An nabawi
3. Ijmai ya Maulamaa katika Ijtihaad zao.