Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Huyo mbwa anayezungumziwa hapa niliwaona kwa Wazungu fulani wenye orphanage Center huko Kigamboni.

Siku moja nikawauliza kama wanauza, wakaniambia wanaye mdogo wa miezi 6 na wanamuuza Euro 1,000/- yaani zaidi ya milioni mbili, nilikaa kimya kama sikuuliza.

Vv

Life is not fair
 
Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe

Hakuna aina ya mbwa anaitwa rock teller, labda mlinzi alimaanisha Rottweiler huyu hapa chini.
images.jpeg
 
bora mimi ninayefuga mbwa koko wangu, wote tushazoea ndefu, tena hua ananipa sapot mana mamb yakizd anazunguka tu hapo kwa asha kibajaji ananiletea sufuria namkwangulia ukoko wake na sufuria naenda uza, siku nikimpa tu vichwa vya dagaa atalipa fadhila week nzima, mana atanijazia vyomb kabati nzima, na yeye hatak mpak uwe mwiz, yan ukiwaza tu kuja kuiba yeye ndo anakufuata huko huko kwako mmalizane, sema ana shida tatu, kwanza n mzinzi, pili kukiwa na sherehe mtaani jiandae kupga usafi wa kutosha asubuh mana atajaza kila kitu hasa zile sahan nyeupe za makaratas na tatu akishba anadharau ukimwita anakuja huku anatambaa(wafugaji wanaelewa) na akikuona unakula dagaa anakuja kukujazia mifupa ya nyama alizokula hapo nje halaf analala huku katanua miguu juu na mdomo waz
Duh! Mzee umetisha, nimecheka mpaka watu wameshtuka.
 
Kuliko kuweka masai bora mbwa maana hadanganyiki.
Kuna siku mwizi aliingia hiyo nyumba ina hao german shephard jamaa kaingia vizuri kwa kuruka ukuta kaiba vitu akawa anarushia nje wale mbwa wamejibanza tu kimya wanamsubir aanze kupanda ukuta!jamaa ile anaanza kujiandaa kukwea ukuta wakamvuta wakampa nako za kutosha afu za kimya kimya hakuna kubweka wala nini??jamaa akaanza kuita mwenye nyumba aje kumsaidia
 
Kuliko kuweka masai bora mbwa maana hadanganyiki.
Kuna siku mwizi aliingia hiyo nyumba ina hao german shephard jamaa kaingia vizuri kwa kuruka ukuta kaiba vitu akawa anarushia nje wale mbwa wamejibanza tu kimya wanamsubir aanze kupanda ukuta!jamaa ile anaanza kujiandaa kukwea ukuta wakamvuta wakampa nako za kutosha afu za kimya kimya hakuna kubweka wala nini??jamaa akaanza kuita mwenye nyumba aje kumsaidia
Yap ukiwafunza huwa wanafanya kazi tamu sana
 
Ninao kumi ninawatunza kwa gharama kubwa kwa mwezi wanakula chakula cha 4m
Halafu ndugu zako hauwapi mahitaji ya kutosha..
Unathamini mbwa kuliko binadamu,
Mnaiga utamaduni wa kijinga...siku Mungu akiamua ufe utakufa tu hakuna mbwa wa kukuongezea maisha!
 
Asa walijuaje kama alikuwa anawapa kg 7 badala ya kg 10?
 
Halafu ndugu zako hauwapi mahitaji ya kutosha..
Unathamini mbwa kuliko binadamu,
Mnaiga utamaduni wa kijinga...siku Mungu akiamua ufe utakufa tu hakuna mbwa wa kukuongezea maisha!
Unakosea sana mkuu, huwezi kutajirisha ndg wavivu hata siku moja, pia ikiwa ana uwezo kutumia 4ml ujue anapesa za kutosha na kusaidia wengine.
Msilolijua ni kuwa, hawa mbwa hufugwa kibiashara na wanalipa sana kushinda kufuga ng'ombe.
Angalia hapa;
1. Mbegu nzuri ya mbwa na akazaa watoto 7 ukauza kila mmoja kwa 1.2ml sawa na 8.4m
2. Mbwa hubeba mimbax2 kwa mwaka=8.4x2=16.8m
3. Chakula cha mbwa mfano nyama utauziwa 2,000 kwa kg, zidisha kwa mwaka halafu linganisha na atakachoingiza
 
Unakosea sana mkuu, huwezi kutajirisha ndg wavivu hata siku moja, pia ikiwa ana uwezo kutumia 4ml ujue anapesa za kutosha na kusaidia wengine.
Msilolijua ni kuwa, hawa mbwa hufugwa kibiashara na wanalipa sana kushinda kufuga ng'ombe.
Angalia hapa;
1. Mbegu nzuri ya mbwa na akazaa watoto 7 ukauza kila mmoja kwa 1.2ml sawa na 8.4m
2. Mbwa hubeba mimbax2 kwa mwaka=8.4x2=16.8m
3. Chakula cha mbwa mfano nyama utauziwa 2,000 kwa kg, zidisha kwa mwaka halafu linganisha na atakachoingiza
mkuu bado me kiupande wangu kununua mbwa kwa bei hyo ni bonge la anasa
 
Afu Mzee huyu sio mbwa bali mashetani yako,hawezi kuwa mbwa huyu,,,af pia kilo 50 zitoke wap hapo
Dah..!
Nilitegemea kukutana na koment kama hii..ukiangalia na hizo picha za passport size za hivo vijibwa yaani nimecheka mpaka bar nzima wananitazama
 
Haka kathread kana uongo flani
Mimi naifahamu Moro japo kwasasa naishi arusha maeneo ya uongo ni haya

1.msamvu kuna sheli tano
2.sheli moja haina makazi ya watu karibu ile ya opozit na tanesko
3.sheli ya pili pale njia ya iringa karibu na noa za turiani hakuna kabisa makazi
4.sheli ya tatu hapa karibu na ATM ya NBC hakuna makazi ya aina hiyo na nyuma wanafyatua matofali kutoka hapo ni maendeleo wa uswazi mpk mtawala
5.sheli ya NNE IPO ilipokuwa makuti bar kabla haujavunjwa hakuna makazi binafsi ya namna hiyo kule nyuma ni gest na hotel I
6.sheli ya tano ni hapa pemebeni ya itigi zamani kwenye Malaya wengi itigi imevunjwa haipo na nyuma ya ile sheli ni uswazi wa mafisa
7.watu matajiri wenye makazi ya aina hiyo utawakuta forest Kule juu karibu na kwa mkuu wa mkoa na ofisi za toss

NB hakuna stori ya hivi Morogoro tungejua tu hii ni habari kubwa ipuuzeni hii thread imeandika uongo jambo kubwa kama hilo litokee msamvu tusijue eti mbwa kamla binadam kambakiza kichwa UONGO HUU HAUPO MOROGORO NA HAKUNA MAKAI BINAFSI YA AINA HII ILIYOELEZWA HAPA

SHIGONGO STORIES

Na wewe ni muongo, si morogoro bali Tanzania nzima hakuna sheli sehemu yoyote ile.
 
mkuu bado me kiupande wangu kununua mbwa kwa bei hyo ni bonge la anasa
Kwasababu hufahamu faida zake.
Kwa upande wangu wangu napenda sana mbwa wa kisasa, ukitaka tukosane mpige mbwa wangu.
Mbwa waliwahi kunisaidia sana, nilikuwa nimehamia nyumba mpya na nikiwa mgeni wa mazingira, nilikuwa sijaimarisha ukuta, vibaka walikuja usiku wako zaidi ya 4, kilichowapata hawatasahau na walisababisha watu kuogopa kuja kwangu hata mchana japo huwa nawafunga.

Mimi nafuga kibiashara na hata polisi walikuwa wateja wangu.
Hawa viumbe wanalipa sana hasa ukiwa na mbegu bora na orginal.

Tahadhari, kama sio mzoefu usiingie kwenye biashara hii kichwakichwa utapoteza pesa. Upate washauri wakushauri mbegu bora.

Kulikoni kufuga koko wala mavi, fuga hawa mbwa wa kisasa ili wakizaa warudishe gharama na waendelee kujitunza
 
Back
Top Bottom