Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe
Yale yale ya Marehemu Babu?
Kawafuga, wakamla
 
Nawawekea Picha Za Hao Mbwa Wanaoitwa Rotweiller Ambao Amedai Wanakula Kilo 10 kwa Mbwa Wawili na Pia Walimla Mtu Na Kubakisha Kichwa

Kwa Muonekano Tu Wa Mbwa Huyu Rotweiller Inaonyesha Kabisa Ni hadithi ya kutungwa kabisa

Moderator tunaomba upeleke uzi huu katika Thread Vichekesho na Vioja hapa sio mahala pake

View attachment 791980 View attachment 791981 View attachment 791982 View attachment 791983 View attachment 791984
Wewe huwezi kula kilo moja ya nyama? Kula ni uwezo au ukubwa wa mwili? Yule mchezaji mpira alipokuja Tz watu hawakushangaa kuku aliokata! Power Mabula alikuwa anakula kiasi gani, uliza waliokuwa wakimjua watakuambia.
 
Confermed hii habari ni ya uongo ipuuzeni nimeulizia msamvu na viunga vya jirani Hakuna tukio kama hili huyu aliota ndoto
 
Uongo sio jambo zuri hata kama hauna madhara. Yaani wamekula kilo 6 za nyama halafu wakamla na mlinzi mwenye kilo zaidi ya 50 wakabakiza kichwa tu!!!!!
 
Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe
Hao ni mbwa hatari sana sana sana... Na katika swala ulinzi wako njema sana ila UKIKOSEA KUWATUNZA WATAKUEZA WEWE UWE CHAKULA!!
 
Uongo sio jambo zuri hata kama hauna madhara. Yaani wamekula kilo 6 za nyama halafu wakamla na mlinzi mwenye kilo zaidi ya 50 wakabakiza kichwa tu!!!!!
hivi unawajua hao mbwa vizuri?
 
Nikinyume na taratibu za ofisi mkuu ila ukihitaji kuwaona naweza kukuelekeza ukihitaji kununu wa miezi mitatu unakaribishwa bei ni milioni 3 kwa huyo mdogo karibu
Mbwa milioni tatu? Hata mahari ya mkwe wangu sikulipa milioni tatu, sembuse mbwa anaeweza kunila!
 
Na wewe ni muongo, si morogoro bali Tanzania nzima hakuna sheli sehemu yoyote ile.
Ni kweli hakuna shell tanzania hii kwa sasa zilikuwako miaka mingi iliyopita, kwa sasa ni oil com, puma, lake oil na nyinginezo lakini si shell
 
Simba na ukubwa wake anapiga 20kg, itakuwaje mbwa kaka?
 
Ninao kumi ninawatunza kwa gharama kubwa kwa mwezi wanakula chakula cha 4m
4m inaweza kuwa ndogo pia kwa matunzo ya mbwa 10 kwa mwezi. Kiufupi mbwa ni luxury good kama magari n.k hivyoo wamilliki wake huwa watu wenye pesa na pia ni state of wealth kuweza kumilik mbwa wa kisasa,
 
Back
Top Bottom