Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Bado unajiona uko sawa? unawezaje kuhudumia mbwa gharama ya mil 4 ilihali wapo binadamu wenzako hawana uhakika hata wa mlo mmoja kwa siku?

Jitathmini, njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba mno@
Dunia ya sasa binadamu ndio hatari zaidi kuliko mbwa,pia huwezi kugharamia kitu kisicho na faida
 
Halafu kuna hawa mbwa wanaitwa dobeman. ..moto wa kuotea mbali
 
Haka kathread kana uongo flani
Mimi naifahamu Moro japo kwasasa naishi arusha maeneo ya uongo ni haya

1.msamvu kuna sheli tano
2.sheli moja haina makazi ya watu karibu ile ya opozit na tanesko
3.sheli ya pili pale njia ya iringa karibu na noa za turiani hakuna kabisa makazi
4.sheli ya tatu hapa karibu na ATM ya NBC hakuna makazi ya aina hiyo na nyuma wanafyatua matofali kutoka hapo ni maendeleo wa uswazi mpk mtawala
5.sheli ya NNE IPO ilipokuwa makuti bar kabla haujavunjwa hakuna makazi binafsi ya namna hiyo kule nyuma ni gest na hotel I
6.sheli ya tano ni hapa pemebeni ya itigi zamani kwenye Malaya wengi itigi imevunjwa haipo na nyuma ya ile sheli ni uswazi wa mafisa
7.watu matajiri wenye makazi ya aina hiyo utawakuta forest Kule juu karibu na kwa mkuu wa mkoa na ofisi za toss

NB hakuna stori ya hivi Morogoro tungejua tu hii ni habari kubwa ipuuzeni hii thread imeandika uongo jambo kubwa kama hilo litokee msamvu tusijue eti mbwa kamla binadam kambakiza kichwa UONGO HUU HAUPO MOROGORO NA HAKUNA MAKAI BINAFSI YA AINA HII ILIYOELEZWA HAPA

SHIGONGO STORIES
 
Dunia ya sasa binadamu ndio hatari zaidi kuliko mbwa,pia huwezi kugharamia kitu kisicho na faida
Ni kweli mkuu, mbwa ni afadhali kuliko mlinzi binadamu mara milioni. Ukiweka mlinzi binadamu utakuta majaribio ya kukuibia yanaongezeka. Pili uaminifu wa mbwa ni 100%.
 
Haka kathread kana uongo flani
Mimi naifahamu Moro japo kwasasa naishi arusha maeneo ya uongo ni haya

1.msamvu kuna sheli tano
2.sheli moja haina makazi ya watu karibu ile ya opozit na tanesko
3.sheli ya pili pale njia ya iringa karibu na noa za turiani hakuna kabisa makazi
4.sheli ya tatu hapa karibu na ATM ya NBC hakuna makazi ya aina hiyo na nyuma wanafyatua matofali kutoka hapo ni maendeleo wa uswazi mpk mtawala
5.sheli ya NNE IPO ilipokuwa makuti bar kabla haujavunjwa hakuna makazi binafsi ya namna hiyo kule nyuma ni gest na hotel I
6.sheli ya tano ni hapa pemebeni ya itigi zamani kwenye Malaya wengi itigi imevunjwa haipo na nyuma ya ile sheli ni uswazi wa mafisa
7.watu matajiri wenye makazi ya aina hiyo utawakuta forest Kule juu karibu na kwa mkuu wa mkoa na ofisi za toss

NB hakuna stori ya hivi Morogoro tungejua tu hii ni habari kubwa ipuuzeni hii thread imeandika uongo jambo kubwa kama hilo litokee msamvu tusijue eti mbwa kamla binadam kambakiza kichwa UONGO HUU HAUPO MOROGORO NA HAKUNA MAKAI BINAFSI YA AINA HII ILIYOELEZWA HAPA

SHIGONGO STORIES
kweli we bumbuwazi mkoa gani tanzania wenye sheli 6?kwaiyo unataka kunambia sheli zote za morogoro unazijua au ulisha shiba futari
 
Specifically umesema sheli hiyo iko msamvu na huyo tajiri anaishi 5th house kutoka sheli ndio nimedadavua mazingira yote ya sheli za msamvu kuku prove wrong na uongo
 
Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe

Hao mbwa wanaitwa rottweiller ni wakali na pia ni watiifu mno. Kama hawakujuwi LAZIMA watakughulikia tu no matter what, sie hapa nyumbani tunao wanne (4) Mze alileta toka South Afrika. Mbwa yeyote akiwa abused LAZIMA atakugeuka tu, sie wetu wanakula chakula cha kipimo kuhofia wasipatwe na obese na kuwa useless/lazy....mmoja akimaliza kabla ya wenzake hapati chakula mpaka kesho yake. Wenyewe wanajuwa vipimo vyao na wakimaliza hawasumbui kwani wenyewe kwa wenyewe wanaogopana, wengine wakibakiza ndipo wale wasioshiba wanakwenda kumalizia.
 
Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe
Hili mbona kama ni kisa cha kutunga mkuu?
 
Back
Top Bottom