DOKEZO Shida ya maji mkoani Morogoro

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Blender

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
3,441
5,309
Nilikuwa kikazi mkoani MOROGORO, nikapita kwa ndungu yangu mafiga iasee, wananchi wa Morogoro municipal wana shida ya maji balaa.

Hasa kipindi hiki cha kuelekea maonyesho ya 88 Hali inakuwa mbaya zaidi, kwani maji mengi wanayapeleka kunyeshea kwenye bustani za mazao mbalimbali kwenye eneo hilo la 88.

Yani week nzima maji yametoka mara tu yani 😤, tena mwenyeji wangu ananiambia hata masaa 2 hayakufika yakakatika.

Viongozi wa mkoa wa Morogoro acheni propaganda wananchi wenu wanaumia, maonesho ya 88, kila mwaka vitu ni vilele tu, watu wameshawazoea hakuna jipya, na hata wakulima wenyewe hawanufaikii kivile, kwasababu kilimo sio maonyesho bali ni shambani.

Pia usumbufu mwingine niliouona ni moshi utokao kwenye kiwanda cha ku-process tubacco, aisee harufu ya moshi wa tobacco ikifika mida ya jioni ni kali sana, mpaka maeno ya SUA huku inafika embu imangini apo means ni karibia mjini mzima, ikifika mida ya jioni wananchi wakiwemo watoto wadogo wamama wajawazito wanavuta moshi mzito wa tumbaku (tobacco).

Viongozi wa mkoa wa Morogoro kuweni na weledi kwenye majukumu yenu ya kazi.

Pia nasikia mbunge abood ametoa basi la maziko, ina maana watu wa Morogoro maitaji yao ni kufa na kuzikwa tu yani 😂.

Wananchi wa Morogoro municipal na viongozi kuweni serious.
 
Moro shida ya maji mbona haijaanza jana wala leo. Shida ya viongozi wetu hawajui kufanya matazamio miaka 200 baadae wao wanawaza hapo hapo. Saiv mji umekua na watu wengi ila miundo mbinu ya tangu tanganyika haijapata uhuru.
Duu noma sana aisee
 
Alafu uwezi amini mkuu, MOROGORO ndio chanzo kikuu Cha maji, safi na salama Kwa jiji la dar


Poleni sana hata huku Zanzibar, maji ni kipusa na unaambiwa ulipie pipe za maji ambayo hayajapatapo kutoka na umejichimbia kisima chako ndani ukilipie .

CCM ni janga
 
Sijui kuna ugumu gani ku solve shida ya maji Morogoro, hii inafanya magonjwa kama typhoid kuwa juu sana hapo Morogoro mjini.
 
Huku MOROGORO Kuna mashirika mengi ya kiislamu sijui ni kwanini, ni kama wanataka kuanzisha Islamic State vile,


Uislamu ni vitendo si mashirika , hao wote watakuwa ni walafi , wangalianza kujipanga kuliondowa Tatizo la maji,

Huku ZnZ, hali ndio hiyo , Raisi haondoki misikitini ni unafiki mtupu , yeye ndiye mwizi mkubwa
 
Jamani Morogoro morogoro yeeee maji yatirirka milimani yooo! Inasikitisha Sana.
Inahuzunisha sana , nasikia wenyeji wanasema mpaka mvua inyeshe ndio utaona maji tiririka mlimani,
Serikali ya CCM Ili waachia watu wafanye wanavyotaka wakidhani ndio maendeleo (propaganda)kumbe wanaharibu,mlima uruguru una vipara vingi sana SS ivi , na mpaka Kuna mmomonyoko wa udongo unaonekana HAta ukiwa stendi ya msavu unaina hicho kipande kilicho meguka.

Nasikia kipindi Cha mkoloni aliruhusu watu kwenda mlimani kuokota kuni TU , na sio kukata miti ovyo, ila tulivyo pata Uhuru, ukawa ni uhuru wa manyani,
Wakoloni walikuwa ni watu wa maendeleo ya kweli,
Serikali ya CCM imefeli bakubwa sana
 
Uislamu ni vitendo si mashirika , hao wote watakuwa ni walafi , wangalianza kujipanga kuliondowa Tatizo la maji,

Huku ZnZ, hali ndio hiyo , Raisi haondoki misikitini ni unafiki mtupu , yeye ndiye mwizi mkubwa
Mashirika ya kiislamu yanazidi kuwa mengi nchini, siu HAta yanazalisha Nini ili kujiingiizia kipato
 
Poleni sana hata huku Zanzibar, maji ni kipusa na unaambiwa ulipie pipe za maji ambayo hayajapatapo kutoka na umejichimbia kisima chako ndani ukilipie .

CCM ni janga
Yani kisima umekichimba Kwa pesa Yako, alafu wanataka Kodi, kweli Serikali ya CCM ni wezi TU Yan 😂
 
Back
Top Bottom