Nilivyogeuza imani hii ya kishirikina kuwa fursa ya biashara na kutengeneza mamilioni

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Mtu mmoja mwenye hekima na busara aliwahi kusema there is a positive thing in every negative thing.

Mwaka 2011 nilienda kijijini kwao na mama yangu mzazi (Homboza karibu na Chanika)

Nilipanga kukaa kwa mwezi mzima.

Nikiwa huko mishe zangu nyingi nilikuwa nazifanyia Chanika center.

Nikiwa Chanika nilibahatika kula chakula kwenye kibanda cha mama lishe. Kilikuwa ni chakula kizuri kupita kiasi. Nilivyokula kwa mara ya kwanza nikajiapiza kuwa nakula kila siku mahali hapo.

Siku moja ya Jumanne nilienda kupata chakula kwenye kibanda hicho ila cha kushangaza palikuwa pamefungwa. Nauliza watu wanasema Jumanne huwa hafunguagi. Kwa kuwa mimi pia nimetoka kwenye familia ya kiswahili na nimekulia uswahilini nikajua huyu dada na yeye ana mambo ya kiswahili. Waswahili huwa wanaamini Jumanne ni siku ya shari. Wengi wao huwa hawafungui biashara siku ya Jumanne wakiamini hawawezi uza chochote ( ingawa si wote/ wasioamini shirki hufungua Jumanne kama kawaida)

Nikafanya uchunguzi wangu Chanika yote siku hiyo nikagundua mabanda mengi ya chakula yamefungwa hiyo. Sikuishia chanika, nikaendelea pia kufanya uchunguzi kwenye maeneo mengine ambayo idadi kubwa ya wakazi ni waswahili kama vile Mbagala, Temeke, Buza n.k kote huko nika notice the same..

Nikasema nitaigeuza hii kuwa fursa. Nilichokufanya nilienda kuongea na hao wenye mabanda kuwaomba wanipe nafasi ya kuwa nauza siku ya Jumanne tu ambayo wao wwnakuwa wamefunga na nitakuwa nawalipa hela.

Wengi walikubali kwa sababu walijua sintouza hiyo Jumanne plus hela kidogo niliyokuwa nawalipa ilifidia gharama za wao kukaa nyumbani bila kufanya kazi.

Nilianza na mabanda matatu baada ya mwaka nikawa na mabanda ya kutosha ambayo nilikuwa nauza chakula Jumanne tu.

Biashara ilikuwa nzuri sana coz wakati waswahili wenzangu wapo nyumbani, mimi vijana wangu wanakuwa ofisini wanapiga kazi.

Nilivyoona biashara imekuwa nzuri nikafungua branches Zanzibar na Tanga.

Few years later nikawa nimetengeneza mamilioni ya shilingi ambayo nilitumia ku invest kwenye biashara nyingine.

Leo nimekuja Chanika nimetafuta breakfast kwenye migahawa kama mitatu yote nimekuta imefungwa nikakumbuka how I made millions off this belief.

Haya SASA iliyekuwa unatafuta wazo la biashara, wazo hilo hapo tayari.

Lifanyie kazi, utakuja kunishukuru.

# kila.kitu ni fursa
 
Branch where and where?

Ok apo nimechukua nyama mifupa nimekuachia ,
nipo apa videte lakin hii ni aina flan ya chai,
Nimejifunza kuwa katikat ya baya Kuna zuri pia
 
Mkuu Likud hongera sana kwa kutupa wazo zuri bila kukulipa chochote .
 
Back
Top Bottom