stata mzuka
JF-Expert Member
- Nov 25, 2012
- 4,834
- 1,765
Nilikutana na mdada wa chuo cha biashara CBE. Kipindi hicho nami nilikuwa nafanya degree yangu ya pili pale Mzumbe. Tulipendana sana, nilisafri mkoani kikazi.
Tuliwasiliana kila siku ila kuna siku moja nilipata sms toka kwa mwanaume ikidai nimuache mpenzi wake akimaanisha yule mpenzi wangu. Juzi nimerudi safari mpenzi wangu alinipokea vyema na kwa furaha.
Cha ajabu chini ya kapeti chumbani nimekuta kondomu 3 zilizotumika takribani siku kama 2 nyuma. nimemuuliza mpenzi wangu amesema nae hajui zimefikaje chumbani kwetu.
Nifanye nini ndugu zangu ila binafsi nimeamua nimuache huenda nitapata mwingine.
Piga chini mkuu kama kaweza kukufanyia hivyo ndani ya Uchumba hashindwi ndani ya ndoa.
Ukiona MANYOYA ujue kaliwa!