Nilipanga kumuoa Januari, nimeahirisha

Nilipanga kumuoa Januari, nimeahirisha

Mh mkuu langu ni moja tu, kama kweli umesoma mpaka masters sioni why unaomba ushauti kwa issue kama hii! Unless otherwise! !

hata ukiwa hujasoma lakini una ufahamu wa kuyatawala mazingira huwezi omba ushauri kwa jambo hili...

elimu ni bora lakini hekima ni bora zaid
 
Nilikutana na mdada wa chuo cha biashara CBE.

Kipindi hicho nami nilikuwa nafanya degree yangu ya pili pale Mzumbe. Tulipendana sana, nilisafri mkoani kikazi.

Tuliwasiliana kila siku ila kuna siku moja nilipata SMS toka kwa mwanaume ikidai nimuache mpenzi wake akimaanisha yule mpenzi wangu.

Juzi nimerudi safari mpenzi wangu alinipokea vyema na kwa furaha.
Ajabu chini ya kapeti chumbani nimekuta kondomu 3 zilizotumika takribani siku kama 2 nyuma.

Nimemuuliza mpenzi wangu amesema nae hajui zimefikaje chumbani kwetu.

Nifanye nini ndugu zangu ila binafsi nimeamua nimuache huenda nitapata mwingine.
Tafuta Mwanamke Mwingine!
 
unataka tukupe moyo kwamba hajaliwa?p[iga chini sio mwaminifu huyo hiyo ndo adhabu pekee anastahili
 
Mungu amekuonesha mapema aina ya mwanamke uliye naye. Pengine hata hukuomba kwa hilo ila ameona inafaa ufahamu. Mengine kakuachia mwenyewe!
 
Sitisha kila kitu, hapo kinachofuata kuumizana roho
 
👌👌👌👊👊👎👎👙👙 akili nyingine heri kondoo
 
eeee jamani kuna vitu vingine ukivisema hata kichaa wa akili anajua unamdanganya...
 
Nilikutana na mdada wa chuo cha biashara CBE.

Kipindi hicho nami nilikuwa nafanya degree yangu ya pili pale Mzumbe. Tulipendana sana, nilisafri mkoani kikazi.

Tuliwasiliana kila siku ila kuna siku moja nilipata SMS toka kwa mwanaume ikidai nimuache mpenzi wake akimaanisha yule mpenzi wangu.

Juzi nimerudi safari mpenzi wangu alinipokea vyema na kwa furaha.
Ajabu chini ya kapeti chumbani nimekuta kondomu 3 zilizotumika takribani siku kama 2 nyuma.

Nimemuuliza mpenzi wangu amesema nae hajui zimefikaje chumbani kwetu.

Nifanye nini ndugu zangu ila binafsi nimeamua nimuache huenda nitapata mwingine.

Stori za kutunga ziko nyingi sana jf.
 
bora amekumbuka kinga ila mpnz wako mchafu. anaachaje condoms zishatumika chini ya kapeti!
 
usikurupuke kumuacha huyo binti jiulize kwanza alipataje ujasiri wa kuleta mwanaume humo ndani tena ni kwako, au kunamtu anawagombanisha tu kijanja. kama umeona ni wife material potezea hiyo kwa sasa. ila mchunguze kwa siri sana bila yeye kujielewa tena ongeza mapenzi asielewe. na muombe sana mungu akuonyeshe ukweli.

thanks kwa ushauri wako mzuri
 
Back
Top Bottom