Nilichomfanyia Bosi wangu hatakuja kusahau mpaka kifo chake

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,709
36,166
Ilikuwa miaka kama 6 hivi iliyopita, watumishi wa kada yetu tulikuwa wachache, muda wa kazi au masaa ya kazi kwa wiki au mwezi yalikuwa mengi zaidi ya yale masaa ya shirika la kazi duniani.

Hatukulipwa posho ya muda wa ziada (extra duty allowance).
Tulikuwa tunafanya kazi mpaka unahisi homa. Kila tukimwambia boss anajibu simple tu. Majibu yake yalikuwa mithili ya haya; "Ukikubali kufunga ndoa na serikali kubali kila kitu....mbona kazi sio ngumu," n.k.

Siku moja nikajilipua nikaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara kulalamikia kufanyishwa kazi kinyume na Sheria na Haki za binadamu. Kwamba nafanyishwa kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku bila kulipwa posho. Ikumbukwe masaa ya kazi yanapaswa yasizidi 8 na yakizidi yatahesabika kama muda wa ziada na mtumishi atapaswa kulipwa, nayo yasizidi masaa 4.

Nikaandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu nakala kwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yetu, nakala kwa meneja wa kituo. Hizi mbili nikazituma kwa EMS na nakala ya boss msimamizi meneja nikampelekea kwa mkono.

Hali ya hewa ilitulia. Waliajiriwa watu kwa dharura siku ya Jumamosi na Jumapili zoezi zima lilikamilika Jumatatu walianza kazi, Mimi nikapewa cheo cha Supervisor.

Sikushauri utumie njia hii, maana ina risk kubwa kwako na kwa Boss wako. Unaweza kupoteza kazi au hata kupata madhara mengine. Boss wako asipotaka kutimiza haki zako kwa njia ya amani umafia unahitajika.
 
Usishangilie. Tunza hii comment yangu. Kwa kifupi ulichokifanya ni cha hovyo sana. Ulikosea Ulikopeleka hizo barua ni mbali sana. Hata baada ya kuzipokea barua yako wanajua hakuna mfanyakazi hapa. Wakubwa huwa wanachukia wafanyakazi wa hivyo. Kupewa huo usupervisor nakwambia ni mtego tu. Ni swala la Muda.
 
🤣🤣🤣ulimuweza mpuuz mmoja huyo

Nami nina boss kimeo Kama huyo,ana miaka zaidi ya miaka 15 kituo kimoja,afu anajisifia uzawa na kaigeuza ofisi ya Umma Kama ofisi yake binafsi,kiasi Cha kuleta vijana wake waliomaliza chuo,ndo anaowakabidhi kazi za kufanywa na Maafisa,Tena Maafisa waandamizi.

Nilipohamia kituo hiki nilikuwa na morale ya kazi kishenzi,mweh bada ya wiki nikagundua huku Halmashauri uvivu,uzembe,oyaoya na kutowalipa watumishi stahiki zao Kama extra duty,ni Jambo la kawaida Sana

Mfano Kifaa kikiharibika unaripot kwake,anakujibu kwa kejeli yani afisa (huku akitaja cheo Cha mhusika)unakosa elfu 30 kununua hicho kifaa?afu anacheka kwa kejeli na kuondoka

Nimejifunza,saivi nafika mapema naandaa ratiba yangu ya siku,nashungulikia majalada yanayonihusu siku hiyo,then 9.30net naamsha popo.kukiwa kuna shortage ya lolote sisemi,napiga mluzi,nalog in Jf,naperuz kupass time,then 9.30net naamsha popo.Nafikiria kuomba leave nikaongeze elimu nabkupumzika na karaha za ofisi kwa muda.

Hii ndo tized,ofisi za Umma nyingi Zina mabos vichomi na uozo mwingi
Usijichoshe,next time,fanya yako usigombane na watu,wengine wachawi utajalogwa au ukawekewa mtego uje ufukuzwe kazi.

Serikali sio kampuni ya baba yako kusema uwe na uchungu nayo Sanaa,watu wanajipigia na hawaproduce chochote and nobody gives a f.uck.
 
Usishangilie. Tunza hii comment yangu. Kwa kifupi ulichokifanya ni cha hovyo sana. Ulikosea Ulikopeleka hizo barua ni mbali sana. Hata baada ya kuzipokea barua yako wanajua hakuna mfanyakazi hapa. Wakubwa huwa wanachukia wafanyakazi wa hivyo. Kupewa huo usupervisor nakwambia ni mtego tu. Ni swala la Muda.
Miaka 6 imepita maisha yanaendelea.
Ulitaka niteseke nife na kazi kwa sababu ya mpuuzi mmoja?
Mimi sio mjinga. Sasa nafanya kazi kwa kuzingatia muda na likizidi hata lisaa nalipwa.
Ulofa wa makondoo sina.
Unajua mabosi wangu ni 3 tu.
1. Meneja wa kituo, 2.Mkurugenzi mkuu na 3. katibu mkuu wa wizara.
Sasa kwa boss nimeripoti zaidi ya mara 3, kwa Mkurugenzi ni best yake . Kama ningeenda kwa Mkurugenzi ningehatarisha kazi yangu (najua mazingira ya kazini kwetu) , unatuma barua au email next week boss wako anaisoma mbele yako. Yaani imeenda na karudishiwa kama ilivyotumwa.
 
Ilikuwa miaka kama 6 hivi iliyopita, watumishi wa kada yetu tulikuwa wachache, muda wa kazi au masaa ya kazi kwa wiki au mwezi yalikuwa mengi zaidi ya yale masaa ya shirika la kazi duniani.

Hatukulipwa posho ya muda wa ziada (extra duty allowance).
Tulikuwa tunafanya kazi mpaka unahisi homa. Kila tukimwambia boss anajibu simple tu. Majibu yake yalikuwa mithili ya haya; "Ukikubali kufunga ndoa na serikali kubali kila kitu....mbona kazi sio ngumu," n.k.

Siku moja nikajilipua nikaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara kulalamikia kufanyishwa kazi kinyume na Sheria na Haki za binadamu. Kwamba nafanyishwa kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku bila kulipwa posho. Ikumbukwe masaa ya kazi yanapaswa yasizidi 8 na yakizidi yatahesabika kama muda wa ziada na mtumishi atapaswa kulipwa, nayo yasizidi masaa 4.

Nikaandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu nakala kwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yetu, nakala kwa meneja wa kituo. Hizi mbili nikazituma kwa EMS na nakala ya boss msimamizi meneja nikampelekea kwa mkono.

Hali ya hewa ilitulia. Waliajiriwa watu kwa dharura siku ya Jumamosi na Jumapili zoezi zima lilikamilika Jumatatu walianza kazi, Mimi nikapewa cheo cha Supervisor.

Sikushauri utumie njia hii, maana ina risk kubwa kwako na kwa Boss wako. Unaweza kupoteza kazi au hata kupata madhara mengine. Boss wako asipotaka kutimiza haki zako kwa njia ya amani umafia unahitajika.
Sidhani kama ulitumia umafia bali ulitumia njia sahihi.
 
Usishangilie. Tunza hii comment yangu. Kwa kifupi ulichokifanya ni cha hovyo sana. Ulikosea Ulikopeleka hizo barua ni mbali sana. Hata baada ya kuzipokea barua yako wanajua hakuna mfanyakazi hapa. Wakubwa huwa wanachukia wafanyakazi wa hivyo. Kupewa huo usupervisor nakwambia ni mtego tu. Ni swala la Muda.
Afu hakutakiwa kuja kujinadi huku.....wanaume fanyeni mambo kimyakimya....mdomo mrefu wa nini eti?
 
Ilikuwa miaka kama 6 hivi iliyopita, watumishi wa kada yetu tulikuwa wachache, muda wa kazi au masaa ya kazi kwa wiki au mwezi yalikuwa mengi zaidi ya yale masaa ya shirika la kazi duniani.

Hatukulipwa posho ya muda wa ziada (extra duty allowance).
Tulikuwa tunafanya kazi mpaka unahisi homa. Kila tukimwambia boss anajibu simple tu. Majibu yake yalikuwa mithili ya haya; "Ukikubali kufunga ndoa na serikali kubali kila kitu....mbona kazi sio ngumu," n.k.

Siku moja nikajilipua nikaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara kulalamikia kufanyishwa kazi kinyume na Sheria na Haki za binadamu. Kwamba nafanyishwa kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku bila kulipwa posho. Ikumbukwe masaa ya kazi yanapaswa yasizidi 8 na yakizidi yatahesabika kama muda wa ziada na mtumishi atapaswa kulipwa, nayo yasizidi masaa 4.

Nikaandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu nakala kwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yetu, nakala kwa meneja wa kituo. Hizi mbili nikazituma kwa EMS na nakala ya boss msimamizi meneja nikampelekea kwa mkono.

Hali ya hewa ilitulia. Waliajiriwa watu kwa dharura siku ya Jumamosi na Jumapili zoezi zima lilikamilika Jumatatu walianza kazi, Mimi nikapewa cheo cha Supervisor.

Sikushauri utumie njia hii, maana ina risk kubwa kwako na kwa Boss wako. Unaweza kupoteza kazi au hata kupata madhara mengine. Boss wako asipotaka kutimiza haki zako kwa njia ya amani umafia unahitajika.
Nilikuwa natafuta UMAFIA WOWOTE HAPO. SIJAONA. ULICHOFANYA NI CHA KAWAIDA ANAFANYA MTU YEYOTE YULE
 
Back
Top Bottom