Kuwalazimisha waalimu kufundisha 'english course' bila posho mpaka saa kumi na nusu kinyume na muda wa kazi ambao ni saa tisa na nusu ni uonevu

Somaiyo

Member
Jul 1, 2022
92
176
Kuna tamko limetolewa na katibu mkuu MSONDE kuwalazimisha waalimu nchi nzima kuwafundisha wanafunzi waliomaliza darasa la Saba kuanzia saa nane na nusu mpaka saa kumi na nusu.

Muda wa kazi kwa mtumishi ni kuanzia saa mbili asubui mpaka saa TISA na NUSU. Baada ya MUDA huo unakuwa MUDA wa ziada na mwalimu au mtumishi anastahili kulipwa posho ya MUDA wa ziada.

Sasa hii kulazimisha waalimu kwa kutumia kauli ya MAELEKEZO kutoka juu kwamba waalimu woote wa sekondari nchi nzima wabaki kufanya kazi hiyo ni UOnevu kwa kundi hili la watumishi. Serikali tunaomba mlitolee ufafanuzi
 
Wazo ni zuri Sana, tena limechelewa mno,huu mpango ulinisaidia miaka 30 iliyopita,

Tuliingia form one, waalimu kila wakifundisha, matoto kutoka snt kayumba, tunatoa macho tu, vitu haviendi, likatolewa tamko,kusitisha masomo yote, ipigwe kozi ya kizungu jtatu mpaka ijumaa, kwa miezi Sita! Hii kitu ilitusaidia sana, baada ya kozi kuisha,form one tulikuwa tunapiga kizungu vzr Sana, kuongea, nk, debate ilikuwa uwanja wetu,

Cha msingi kozi iliendeshwa kwenye muda wa serikali, hii ya kuwalazimisha, ni kuwatia kisirani waalimu, ni kuongeza ndimu na chumvi kwenye kidonda Chao cha maslahi duni cha muda mrefu,

Waalimu ni wahanga Sana wa mfumo CCM, pesa ya mwenge, inakatwa kwao, kupokea wageni wao ndio flour girls,,
Kazi ya ualimu imefsnywa ya laana kama boda boda
 
Watoto ni maroboti ambayo yako busy na vitabu tangu la kwanza mpaka std 7 hayana muda wa kipumzika.

Miezi 3 hii ni ya mtoto kutafakari, kutembea, kusafiri, kujifunza biashara za baba zao, kucheza, kujitafuta nk. Wale wanaopenda ndoo waende pre form one, ila dio kuwalazimisha ni kuvunja haki za watoto.
Nchi inawaza kingereza ndio mafanikio. Wangapi wanajua kingereza na gawana maisha.
Badala Musonda kusisitiza ufundushaji bora wa somo la kingereza shule ya msingi analazimisha vitu visivyowezekana.
Wanaenda kusoma hizo shuke jwa sherua gani,usajili gani, gharana za vifaa jama chaki, manila, marker pen, vitabu analipa nani?
Kwa sababu hii nchi ina MAZOMBIE wengi wataunga mkono hoja.
MTOTO WAKO KASHINDWA KUELEWA KINGEREZA MIAKA 7 ATAELEWA MIEZI 2.
 
Mnawapenda CCM ,na kutumika kama dodoki ondoeni hicho chama maana kila mwalimu unayemwona Hana furaha ,Sasa mtu anaanza kazi hadi anastaafu mikopo,mikopo,hata hela ya kuhonga Hana ondoeni huyu ujinga unaoitwa CCM ndio mtakuwa na mwanga wa maisha.
 
Wazo ni zuri Sana, tena limechelewa mno,huu mpango ulinisaidia miaka 30 iliyopita,
Tuliingia form one, waalimu kila wakifundisha, matoto kutoka snt kayumba, tunatoa macho tu, vitu haviendi, likatolewa tamko,kusitisha masomo yote, ipigwe kozi ya kizungu jtatu mpaka ijumaa, kwa miezi Sita! Hii kitu ilitusaidia sana, baada ya kozi kuisha,form one tulikuwa tunapiga kizungu vzr Sana, kuongea, nk, debate ilikuwa uwanja wetu,
Cha msingi kozi iliendeshwa kwenye muda wa serikali, hii ya kuwalazimisha, ni kuwatia kisirani waalimu, ni kuongeza ndimu na chumvi kwenye kidonda Chao cha maslahi duni cha muda mrefu,
Waalimu ni wahanga Sana wa mfumo CCM, pesa ya mwenge, inakatwa kwao, kupokea wageni wao ndio flour girls,,
Kazi ya ualimu imefsnywa ya laana kama boda boda
Yes wawalipe waalimu na sio kuwalazimisha
 
Mnawapenda CCM ,na kutumika kama dodoki ondoeni hicho chama maana kila mwalimu unayemwona Hana furaha ,Sasa mtu anaanza kazi hadi anastaafu mikopo,mikopo,hata hela ya kuhonga Hana ondoeni huyu ujinga unaoitwa CCM ndio mtakuwa na mwanga wa maisha.
Ni wazo pia, lakini kwa sasa wawalipe waalimu
 
Swali la msingi la kujiuliza ni hao walimu wanaimudu hiyo lugha ya kiingereza kwa ufasaha!?
 
Kuna tamko limetolewa na katibu mkuu MSONDE kuwalazimisha waalimu nchi nzima kuwafundisha wanafunzi waliomaliza darasa la Saba kuanzia saa name na NUSU mpaka saa KUMI na NUSU

MUDA wa kazi kwa mtumishi ni kuanzia saa mbili asubui mpaka saa TISA na NUSU. Baada ya MUDA huo unakuwa MUDA wa ziada na mwalimu au mtumishi anastahili kulipwa posho ya MUDA wa ziada.

Sasa hii kulazimisha waalimu kwa kutumia kauli ya MAELEKEZO kutoka juu kwamba waalimu woote wa sekondari nchi nzima wabaki kufanya kazi hiyo ni UOnevu kwa kundi hili la watumishi. Serikali tunaomba mlitolee ufafanuzi
Maelekezo kutoka juu?!! Hivi Hawa viongozi wanampenda kuropoka bila kufikiria kwa nini lakini? Kama mmnajua kingereza ni somo muhimu kwa wanaenda sekondary, kwanini shule zote nchini isiwe English medium... Juzi tu mmetoa rasimu mpya na ktk utafiti wenu hili la Lugha lililalamikiwa ila kwa kuwa mnalinda biashara za private schools., mmeligomea saa hizi mnasema wafanye tuition... Acheni ubinafsi... Nyie mnaweza fanya kazi bure... Kweli
 
Kuna waathirika wawili:
Walimu huchoka ni haki yao wapewe motisha kwa kufundisha muda huo. Kumbuka huwa hawana allowances kama walio na kazi nyingine. Tudiwachukulie poa.
Wanafunzi nao vichwa hugonga inabidi walimu wawe wabunifu kuwafanya wanafunzi wapende somo bila kuchoka.
 
Kuna tamko limetolewa na katibu mkuu MSONDE kuwalazimisha waalimu nchi nzima kuwafundisha wanafunzi waliomaliza darasa la Saba kuanzia saa nane na nusu mpaka saa kumi na nusu.

Muda wa kazi kwa mtumishi ni kuanzia saa mbili asubui mpaka saa TISA na NUSU. Baada ya MUDA huo unakuwa MUDA wa ziada na mwalimu au mtumishi anastahili kulipwa posho ya MUDA wa ziada.

Sasa hii kulazimisha waalimu kwa kutumia kauli ya MAELEKEZO kutoka juu kwamba waalimu woote wa sekondari nchi nzima wabaki kufanya kazi hiyo ni UOnevu kwa kundi hili la watumishi. Serikali tunaomba mlitolee ufafanuzi
Hili tamko kalitolea hewani?? Sina hakika kama hii taarifa inaiukweli wowote maana hakuna kiongozi mwenye akili timamu atajiamulia tu kusema
kitu kama hiki
 
Kwani walimu wenyewe wanasemaje? Kuna ile jamaa usiyemkubali ndiyo anagonga dada yako tena dadayako anaipeleka mwenyewe hata kwa kutoroka kwa kuruka ukuta.

Juzi kwe graduation ya la saba shule x moja ya waalikwa ni head master wa shule ya sec y sasa huyu jamaa alipopewa fursa ya kuongea alipigia sana promo swala hilo la English course yaani inaonekana yeye shuleni kwake limekubalika mno. Wewe na mimi tukae kimya walimu wenyewe wamekubali na kama kishingo upande basi wapambane na hali yao ya sitaki nataka.

Kinachoniuma mdogo wangu nilitaka aje huku bush anisahidie kutafuta chambo wa kuvulia samaki ili tupate pesa ya mahitaji ya shule mwakani.
 
Back
Top Bottom