Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Jana kuna mchina nilikutanishwa nae ni CEO wa kiwanda cha uzalishaji wa marine boards, melamain boards, pliewoods na MDF ambacho wamekijenga pale Mafinga.
Nilimuuliza ABCs za maisha yake hapa Tanzania na akanambia yafuatayo.
1. Yeye alikuja Tanzania kipindi cha ujenzi wa uwanja wa mpira wa Benjamini Mkapa na alikuja kama kibarua wa kulipwa posho kwa siku.
2. Uwanja ulipoisha kwasababu alipokuwa kibarua alikua akijituma sana boss wake alimwamini na kumpa kazi ya kusimamia Makarasha Chalinze kama Foremen.
3. Walipomaliza mradi wa Chalinze yeye aliona kurudi china haiwezekani kwani kwa muda aliokaa TZ kaona fursa nyingi na utajiri mwingi.
4. Aliamua kumshawishi boss wake kwamba kama wao wanarudi china yeye anaomba abaki TZ aone fursa na ndipo alipoenda mafinga na kuona fursa iliyopo kwenye miti. Na akamwambia boss wake wafungue kiwanda yeye atakisimamia na atahakikisha mtaji unarudi na faida wanapata.
5. Boss Alikubali na sasa kile kiwanda ni kikubwa yeye ndo msimamizi na anamiliki billions of money .
NILIMUULIZA KWA MUDA ALIOKAA AMENIFUNZA NINI NDANI YA TANZANIA.
1. Alinambia nyie Watanzania ni watu wajinga sana kwasababu mnaamini kwenye miujiza kwakutumia muda mwingi kusali na kulala.
2. Fedha mlizotafuta kwa jasho mnachezea kamali/gulugulu alilotengeneza mchina mkiamini mtapata utajiri, akamalizia hakuna utajiri wa namna hiyo.
3. Hamjui matumizi ya simu, muda mwingi mnatumia simu kwa vitu vya kijinga akishangaa mtanzania anaweza kukupigia cm mara 20 mfululizo kama hupokei simu yake. Yeye Ana muda maalum wa kupiga cm na kupokea simu.
4. Mnaabudu na kuamini wanasiasa wanaweza tatua shida zenu kumbe wao ndo wanawategemea ninyi mtatue shida zao.
5. Mfumo wenu wa Elimu ni wa kijinga kwasababu haumuandai mtoto kuwa mbunifu na kutumia maarifa yake kubuni/ama kuzalisha bidhaa ili ziingie sokoni.