Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,939
- 36,866
Ilikuwa miaka kama 6 hivi iliyopita, watumishi wa kada yetu tulikuwa wachache, muda wa kazi au masaa ya kazi kwa wiki au mwezi yalikuwa mengi zaidi ya yale masaa ya shirika la kazi duniani.
Hatukulipwa posho ya muda wa ziada (extra duty allowance).
Tulikuwa tunafanya kazi mpaka unahisi homa. Kila tukimwambia boss anajibu simple tu. Majibu yake yalikuwa mithili ya haya; "Ukikubali kufunga ndoa na serikali kubali kila kitu....mbona kazi sio ngumu," n.k.
Siku moja nikajilipua nikaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara kulalamikia kufanyishwa kazi kinyume na Sheria na Haki za binadamu. Kwamba nafanyishwa kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku bila kulipwa posho. Ikumbukwe masaa ya kazi yanapaswa yasizidi 8 na yakizidi yatahesabika kama muda wa ziada na mtumishi atapaswa kulipwa, nayo yasizidi masaa 4.
Nikaandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu nakala kwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yetu, nakala kwa meneja wa kituo. Hizi mbili nikazituma kwa EMS na nakala ya boss msimamizi meneja nikampelekea kwa mkono.
Hali ya hewa ilitulia. Waliajiriwa watu kwa dharura siku ya Jumamosi na Jumapili zoezi zima lilikamilika Jumatatu walianza kazi, Mimi nikapewa cheo cha Supervisor.
Sikushauri utumie njia hii, maana ina risk kubwa kwako na kwa Boss wako. Unaweza kupoteza kazi au hata kupata madhara mengine. Boss wako asipotaka kutimiza haki zako kwa njia ya amani umafia unahitajika.