A
Anonymous
Guest
Nadhani mnakumbuka Hospitali ya Amana ilishiriki kuhudumia Wagonjwa wa COVID-19 hiyo ilikuwa kuanzia Mwaka 2020, sasa katika ile kazi kulikuwa kuna posho ambayo Watumishi na Vibarua ilitakiwa tupewe.
Makubaliano ya awali yalikuwa kulipwa Shilingi 50,000 kwa siku japo baadaye walishusha hadi kuwa 40,000 kwa siku bila makubaliano y pande mbili, tukaona poa tu.
Tulikaa muda mrefu bila kupata malipo hayo, baada ya kakuanza kulalamika kwa uongozi kish taarifa kufika hadi Wizara ya Afya, ndipo Machi 2023 malipo yakatolewa kwa watu 37 tu huku wengine wengi tukibaki hatujui hatima yetu, idadi kamili siiikumbuki kwa kuwa tulikuwa wengi na vitengo tofautitofauti.
Wale Watumishi ambao hatukupata tukasikia tutapewa mwezi unao fuata yaani baada ya Machi 2023 lakini mpaka leo tunauanza Mwaka 2024 hatujapewa na hatujui kama hilo litatokea.
Upande wa vibarua waliingia hasara ya kukopa vitu na hela wakiamini hela itaingia na watarejesha mikopo yao lakini haijawa hivyo.
Ukiulizia au kufatilia malipo hayo unaonekana mkorofi, kwa sisi vibarua ukiulizia yanakukuta makubwa, unasimamishwa kazi kabisa au unaweza kutengenezewa mazingira ya kufukuzwa.
Naomba ujumbe huu uwafikie viongozi wa juu Serikalini akiwemo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aone namna ya kutusaidia ili tupate haki zetu kwani baadhi wameshaacha kazi au wameachishwa bila kupata stahiki zao.