Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Jamani msisahau kwamba wanaume ni viumbe dhaifu sana kwenye mambo hayo, inawezekana kabisa huyo binti alimtega na mumeo akategeka...wewe kama mwanamke unatakiwa kukaa kitako na mumeo muweke sawa jambo hilo, inawezekana akitaka tendo la ndoa na wewe huwa unamjibu umechoka au hutaki tuu sasa unategemea yeye afanye nn?hizi ishu zikitokeaga mara nyingi wanaume ndo wanaonekana wabaya lakini je wewe mwanamke umejiuliza kwamba wewe sio chanzo cha hilo tatizo? Ukishajua hilo basi muombe Mungu akusaidie na ailinde ndoa yenu.... Na nikwambie tu kwamba hiyo kesi ukiipeleka kwa wazee mwisho wa siku ni wewe mwanamke ndo unaonekana mkorofi na unaambiwa uombe msamaha uondoke na mumeo.... Upo?
 
Ndo ukweli...na friction ni kubwa ukijifanya mjuzi wa 'hardcore sex'...lakini still, utelezi haupunguzi risk..kwani kama mwanamke ndo mgonjwa, vijidudu vyenyewendio vipo kwenye huo utelezi! All in all...safer sex is the condomized one, na hii ni challenge kwa wanaume ambao umri umeenda..kitu chenyewe tia-maji tia-maji, hata ukirescuscitate na Viagra...utavisha condom!?
hahahahha! ngoja nicheke si kwa mazuri bali kwa jinsi ambavyo hili gonja limeumiza familia zetu Mungu atunusuru.

kuna kitu ambacho nimekidiscover most of women ambao wako under ARV'S wako kwenye lesser chance ya kutransmitt HIV kuliko wale ambao hawatumii kabisa. For a man he is more safe kama akimake love na mwanamke ambaye yuko kwenye mashudu chances za kuambukizwa ni ndogo ukikompea na wale ambao wanayakimbia mashudu.

lakini sasa ukija kwa mwanamke kama akimake love na mwanaume awe anatumia mashudu huyu mwanaume ama hatumii bado chances za kuambukizwa ni ileile. what makes this??

of course hii imetokana na samples ambazo nilikuwa ninazifanyia study na ambazo kwenye interview na hata kwenye vipimo vilionyesha hivyo. i failed to know the reason.( anyways siwez kuprempty kila kitu hapa as bado haijakuwa published but naomba clinical explanation)
 
Davina

Sikushauri uondoke ,ila pia unanishangaa unaposema siwezi kuondokan eti kwetu mbali. Hii ni pschological jail. Kwani ulizaliwa ili milele uishi na mume? SO what ? huwezi kuwa independent if worse comes to worse? Acha kuwashusha wanawake bwana --mtu hadi anatembea na mwanae bado unalia lia ooh naogopa? mlizaliwa naye?

Kwanza mkalishe mumeo -tena umueleze kinagaubaga kuwa hupendi na umedhalilishwa na tabia hiyo. maana kumezea utaja jiletea kansa bure. Kuna tabia nyingi sana majumbani- wanaume kusex na ndugu wa mke, houegirl ila hii na binamu yake? loh kali

Imagine mwanao ndio kaenda kutembea kwa binamu na amefanyiwa hivi? ungejisikiaje? , huyo binti ni victim of circumstance na kumfukuza sio suluhu. Ungekaa nae akakueleza vizuri what else conspired.
 
davina anza kwanza kuyanyoosha humo humo ndani kabla ya kuyapeleka kwa wazazi au ndugu wengine.Mie naamini mkikaa mkayamaliza humo humo ndani mtapata ufumbuzi wa kudumu kuliko mkianza vikao na ndugu.Kama jamaa hajawahi kuwa na tabia hiyo, na ameteleza kutokana na mazingira yaliyomkuta, amini lazima suluhu itapatikana na maisha yatarudi kama zamani.
Tena hili la kukutwa na ndugu wa damu, anatamani ardhi ipasuke aingie kuliko ndugu walijue hili.Na huyo binti akifika huko kijijini hawezi kusema amefukuzwa.atasema amerudi kusalimia, na atakuwa anaombea hili suala lisifike huko.Kama ni wa Iringa asije akawa amejitundika muda huu kabla haujapeleka taarifa.mumeo Akianzisha mazungumzo uwe tayari kushiriki mazungumzo haya na mlimalize wenyewe bila kushirikisha ndugu wala viongozi wa dini.
naamini kwa uwezo wa mungu mko wazima!

napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm n mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia,

kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine
nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo,
, kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa, tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu)

jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wang akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gar akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake,niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri bint akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule bint akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokina, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala,

leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.
wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima, nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani
 
Last edited by a moderator:
nilikosea tangu mwanzo na sitaki kukumbuka, lakini jua alinirubuni nikiwa binti mdogo sana!


Daaaa.. Pole sana davina. watu8 wewe sasa unachokoa vidonda vilivyopona ndo nini banaaa!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Davina, pole sana.
1. Hili suala limekuuma kwa sababu unampenda mume wako.
2. Hili linakuuma kwa sababu unaamini kwenye usafi na utakatifu wa ndoa, pia Nguvu ya kiapo cha wanandoa cha kuaminiana na kuheshimiana.

3. Mume wako kuzini/kuvunja kiapo/kukosa uaminifu ni kielelezo tu cha mmomonyoko wa misimamo katika maisha yake. Anapaswa kurudi nyuma, na kuanza upya kujifunza kutii kiapo cha ndoa na kuwa mwaminifu sio kwako tu bali hata kwa watu wengine.

4. Kurudi kwenu kunaweza kumfanya akuone haupo nyumbani, lakini mara nyingi kumewafanya wanaume wengi kujenga usugu na kiburi kama njia ya kuhalalisha matendo yao. Kuondoka nyumbani kwako ni Ishara ya kushindwa vita.

*Ninasema kushindwa vita kwa sababu ndoa sio biashara bali ni vita. Ni vita unayopigana dhidi ya watu wa nje, ndugu zako, majirani, marafiki, pesa, kazi.
*Kuingia kwenye ndoa ukitegemea kila kitu kitakuwa tambarare ni kujidanganya.
*Vita vinakuja vingine sio hivi tu. Suala ni je, wewe unajua namna ya kuwapiga maadui zako???

NJIA NZURI NI KUMTANDIKA KWA MSAMAHA - Lazima uliongelee hili jambo na mwonyeshe kuwa ametenda kosa la Usaliti wa Uaminifu wako kwake. Kumnyamazia mtu unaeishi nae ni kosa kubwa (maana ataitafuta furaha anayokosa kwingine. Hivyo ni muhimu wewe ukawa ndie unaetoa suluhisho la moto unaowaka ndani yake.

5. Ni vizuri ukamfundisha mume wako (ukawa mwalimu wake)katika wakati wa raha.
*Muw ena misimamo kama watu, kama familia,kama marafiki na muwajibike kuitetea misimamo hiyo wote pamoja.

6. Ongeza mawasiliano katika mahusiano yenu : ninahizi nyie mna mid life Crisis/ ambayo isipothibitiwa mtaachana. Msifuate mwili wenu unavyowatuma, bali fuateni roho zenu.
 
Daaaaahhh pole sana davina,mtangulize Mungu katika hilo.
 
Last edited by a moderator:
hahahahha! ngoja nicheke si kwa mazuri bali kwa jinsi ambavyo hili gonja limeumiza familia zetu Mungu atunusuru.

kuna kitu ambacho nimekidiscover most of women ambao wako under ARV'S wako kwenye lesser chance ya kutransmitt HIV kuliko wale ambao hawatumii kabisa. For a man he is more safe kama akimake love na mwanamke ambaye yuko kwenye mashudu chances za kuambukizwa ni ndogo ukikompea na wale ambao wanayakimbia mashudu.

lakini sasa ukija kwa mwanamke kama akimake love na mwanaume awe anatumia mashudu huyu mwanaume ama hatumii bado chances za kuambukizwa ni ileile. what makes this??

of course hii imetokana na samples ambazo nilikuwa ninazifanyia study na ambazo kwenye interview na hata kwenye vipimo vilionyesha hivyo. i failed to know the reason.( anyways siwez kuprempty kila kitu hapa as bado haijakuwa published but naomba clinical explanation)

Nakubaliana nawe..na reason ni kwamba mtu mwenye HIV akiwa anatumia ARVs, viral load (kiasi cha virus mwilini mwake) kinapungua sana hata sometimes ukipima viral load inakuwa 'negligible'..huyu sasa kama ni mwanamke chances za kuambukiza mwanaume ni ndogo. Na hii ni kwa sababu mwanaume uambukizwa wakati uume unapokuwa ukeni hasa kama umechubuka kidogo kutokana na jigy-jigy...na kwa kuwa ngozi ya uume ni ngumu kuliko ngozi ya uke...ni vigumu kidogo kuchubuka.

Ila kama mwanaume ndio ana HIV...ni rahisi kumuambukiza mwanamke hata akiwa kwenye ARVs...na hii is more of 'logic'..uume uma ngozi ngumu na una nguvu, hivyo ni rahisi kuchubua ngozi laini ya uke..pili manii/shahawa ambazo ndio zinabeba hao virus zinamwagwa ukeni na zinaachwa huko baada ya tendo. So virus wana muda wa kutosha kutafuta sehemu dhahifu ya ngozi ya uke na kupenya na kuinfect mwanamke.
 
lazima utakua single wewe? Mimi pamoja na ukichaa wangu wote, ndoa yangu bado nimeishika tena sitaki hata initoke dear! Kama kuondoka ndo suluhu hapa basi, i can assure u that, she will go back to her husband. Na mume pia atachanganyikiwa mkewe kuondoka lakini pia davina atachanganyikiwa pia.

Sijui mungu aliweka nini kwenye kiapo cha ndoa, watu wengi waliodivorce au kutengana akiri zao haziko fresh pia huwa wanapoteza focus fulani kwenye maisha na wengine huamua tu kuoa/kuolewa tena ila ni shughuli jamani.
Cha msingi, kue na strong factor ya kuvunja ndoa ambayo hapa sijaiona bado.

Nawakilisha
huu ni uongo,maybe unaowafahamu wewe.wapo ambao walivumilia,na wakaambulia ukimwi.na inachosikitisha.mara nyingi mke hufa mwanzo.uamuzi ni wake,ila sometimes kuna ndoa nyengine,kuachana ni best solution.nimeshangaa kweli na comment yako.
 
yaani Mtoboasiri wewe una roho yangu khaaa!
sasa nimekuumiza kwa lipi jamani siunaona nimejisemea ukweli tu??

BTW karibu nyumban kwangu swtlo wangu Kaizer ananichinjia mbuzi this week end.

Ngoja niwe mpole, maana nikisema hadharani nitarushiwa mawe! Sie wengine tuna damu ya kunguni ati.

Kaizer, nimekaribishwa. Upoooo??? Mbuzi awe mkubwa!
 
Kuna mambo huwa siwazi kukaa kikao na mtu kudiscuss!! Yaani hapo ni mwisho wa ndoa, hakuna ndoa hapo!!! Afanye kwa heshima, wetu wanacheat ndio lakini sio kwa uwazi hivyo!! Tena na mwanae???? Laanakhum! Dada mpendwa kacheck afya yako, then sepa, hakuna ndoa hapo!!
 
Daaaa.. Pole sana davina. watu8 wewe sasa unachokoa vidonda vilivyopona ndo nini banaaa!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ili utoe ushauri mzuri inapaswa umhoji muhusika kwanza, nami nilikua najaribu kumfanya afunguke zaidi nijue mwanzo wa mahusiano ulikuwa vipi.
Msingi mzuri ndio uimara wa nyumba, na jinsi uendavyo chini ndivyo nyumba iendavyo juu zaidi.
Hata mapenzi yapo hivyo hivyo, yale yanayodumu ujue watu wamewekeza MIOYO na AKILI zao hapo.
 
Vipi; nawe yamekukuta nini mwenzetu?

Btw: Yaani Kongosho hayumo humu???!!!! Maajabu!

wewe mi siwezi kulea ujinga kama huo halafu watu wnamshauriii akae nayeye anadai kwetu mbaliii davina hii kauli yako imeniboaaa sana am sorry to say this wewe mwenyewe unajikandamiza u dont know ur value hujitambui upo upo upo tu
 
Last edited by a moderator:
Dah..Miaka 47 ni umri tosha kabisa huyo binti kumuita huyo uncle yake babu licha ya kumuita mjomba, huo mchezo haukubaliki na sio jambo la kunyamaza kimya. haraka sana wajulishe washenga ili apewe onyo, kuondoka ni kwamba unampa nafasi ya kutafuta kabinti kingine na kuendeleza huo mchezo. huo si ni sawa na mtoto wake jamani.

Nachoweza kusema ni kwamba kama alithubutu kufanya hayon yote getini je huko njiani au huko kwenye biashara unajua walifanya mangapi makubwa zaidi ya hilo uliloshuhudia kwa macho yako

Kwanini mahesabu yafanyike kwenye gari wakati tayari amefika nyumbani?
Hii inaonyesha ni kamchezo kao kalishaanza siku nyingi na pia ni wazi kwamba yeye ndo alimwambia aje aishi hapo kwenu ili iwe rahisi kwao kuendeleza hako ka mchezo. usiondoke komaa nae ukomeshe hiyo tabia yake kama sio kuipunguza kasi.
 
maybe huyo mwanamume anakujua uko weak.hata aki cheat,hufanyi lolote.kama angekuwa na heshima zake,angeyafanya mbali tu.na kama unavyosema sio mara yake ya kwanza.be strong jitahidi uwe na msimamo wako,ambapo huyo bwana asikuone legelege
 
Back
Top Bottom