Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

sijui kwa nini nimetaka kutokuchangia huu uzi ila naona niseme japo kidogo tu na wewe dada davina.

kwanza nikupe pole kwa matatizo haya, ila nikutie moyo kwamba wewe sio wa kwanza kupitia haya mamii. ushauri wangu kwako ni huu hapa, kwanza jiulize unataka nini kwenye maisha yako, ukisha jua basi amua kulingana na unachokita wewe.

pima kwa akili yako uone kama hii ndoa unaiweza ama huiwezi kama unaiweza utahimili vipi hii mikiki?? na kama huiwez utahimili vipi changamoto za kutoka kuanza maisha mapya.

Kwangu mimi kosa alilofanya mumeo ni kosa ambalo linamdhalilisha yeye lkin pia linakujengea chuki na ugomvi kwako na kwa jamaa zako(wakwe). pia ukumbuke kwamba impact ya kosa hili inaweza ika extend hata kwenye visasi si tu kwako bali hata kwa wanao.

kosa hili linaweza kukusababishia wewe matatizo makubwa sana usipolihandle kwa akili sana, kwani undugu wa mumeo umeguswa kwa kiasi kikubwa sana. usikurupuke hata kidogo, tulia wala usihamaki kuanza kusema haya kwa ndugu na marafiki hapana tulia acha uwezo wa akili yako ifikiri kwa akili zaid.

kitendo cha kumfukuza huyu binti ni sawa kabisa, wala usiseme kwann umemtimua wewe tulia, na akitaka yeye ndo aseme kwann umemtimua ila wewe uwe kimya kukata mzizi wa fitina.

ukisha kaa umetulia, ongea na mumeo ukweli kwamba amekuaibisha na kwamba kwa vitendo vyake vyte vya ufuska umevumilia but kwenye hili huwez tena kuvumilia inakubidi uamue maamuzi magumu. mwambie wazi kwamba skendo yake imevuka mipaka na hata watu wana msema vibaya tena mwambie kwamba hata huyu binti kasema kwa watu kwamba sukari yake haikozi na wewe ulijifunza kuyanyamazia ila sasa mtaani ndio stori( hapa mtishe kwa maneno ya uongo lkn yatakayo mfanya aone uanaume wake unadhalilika). baada ya kumwambia then mwambie anasemaje juu ya haya maisha.

usiondoke ndani mwako ila mwambie kwa alipofikia inabidi kurevive upya ndoa yenu kwa kwenda kutubu kanisani kisha kuweka kiapo upya, kisha kupima juu ya magonjwa. sali sana juu ya ndoa yako na amani ya familia yako. wapende sana wanao timiza wajibu wako, pendeza sana hadi sasa yeye aanze kukuonea wivu. mfanye mumeo aanze kukulilia wivu kwa kupendeza, kujitoa out wenyewe kula good time nk.

mm huwa siangalii nikitaka kujipa raha ZANZI ningeifuata hata km 30 toka nyumban kwangu, tena ningekuwa namuaga kabisaa kwamba nakwenda kupata raha na friends sehem fulan sasa akili imkae sawa. nenda kazini mwako, fanya kazi, pendeza sana kila siku na pamba mpya, wape wanao raha za kufa mtu halafu yy muignore hadi point ya mwisho.
 
Last edited by a moderator:
"pedophilia is the psychiatric disorder characterized by act or fantasy where an adult engage in sexual activity with a child or children."

your husband is 'pedophilic'...huu ni ugonjwa wa akili kabisaa na kuna jinsi ya kuutibu kwa psychiatrist, he needs professional help. Ongea naye, au shirikisha rafiki zake, ndugu zake (shangazi mwenye binti)..ili apate msaada wa kisaikolijia...au jela inamuita! Inaaminika r.kelly naye ana tatizo hili, possibly na marehemu michael jackson (he was more of a fantasy though).

Nb: Stop that circle...other wise mwanao (kama ni wa kike) could one day become a victim. Au hata mtu mwingine anayekuhusu sana atakuwa victim. Kwa wenzetu ulaya pedophilics huwa wanakuwa anounced kabisa public ijue na anafuatiliwa maisha yake yote...because it tends to reccur even after treatment.
kitabibu inasemekana pia mwanaume kama alikuwa malaya akishfika umri wa 35yrs hajaiacha tabia hiyo .hatakaa aiache tena mpaka kufa na hiyo inaweza kuwa ndio tiketi yake it has been proved scientificaly na mimi namjua mtu wangu wa karibu wa hivyo .so inawezekana pia ndio ugonjwa wa huyo mumewe
 
Pole sana davina, kuna mambo mengine maishani hayana majibu ya haraka na suluhu zake sio kama hesabu za kawaida 2+2=4

Kama unamahusiano mazuri na ndugu wa mmeo, na ikiwa mila zenu hazikukatazi kwenda kwao, nenda kapumzike kwa ndugu wa mmeo, yeye usimwambi lolote ila tu mjulishe kwamba unaenda kwa ndugu zake na ukifika huko tafuta sababu yeyote usiwaambie kwanza yaliyotokea, kama bado ana chembe za ubinaadamu atakufuata na huenda hiyo ikawa ni nafasi ya wewe na yeye kuliangalia tatizo hilo kwa upya.

Mwisho, maombi ya mwenye haki yafaa sana, hasa akiomba kwa bidii.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa majaribu, nafikiri inaweza ikatokea katika mazingiza fulani lakini suala la kujihusisha na ndugu hilo hapana, binafsi naamini mumeo ana matatizo ya kiakili! Kwa mtazamo wangu alichokifanya ni miongoni mwa makosa ambayo hatakiwi kusamehewa hawa kidogo, kumsamehe ni kumhalalishia na kuzalisha ma-pedophile wengine wengi kwenye familia nyingine za kote atakapopita ... kwa nchi zilizoendelea huyo anatakiwa afungwe kwenye jela/hospitali maalumu za wendawazimu na kuzuiwa kupita baadhi ya maeneo especially yenye watoto kama vile shule na makanisa!

Ok, to the point, kwanza kemea hiyo tabia kwa 'sauti kubwa na kali sana', usisamehe haraka na mwisho hakikisha kikao cha watu anaowaheshimu sana kama vile wazazi, mshenga, mchungaji ama ndugu kinafanyika kwa kungu zote mwisho, usimuache apoe kwani now anajiandaa ni jinsi gani atatoka katika huo mtego ... niamini, ukichelewa atakugeuka na kukubishia huku akiapa kwa majina ya miungu yote duniani na mbinguni na mwisho wa siku utaonekana muongo na atakufunza adabu!
 
pole sana sikushauri uondoke lazima uipiganie ndoa yako! lara1 huwa anaushauri ila tabu mkali sana
ngoja ni pm ili niwe huru zaidi kukushauri kwa vizuri.

nakusubiri!
 
Ondoka kwa amani ukapumzike nyumbani kwanza.
Hapo utakuwa umepata jibu uamue nini
Kwa mtu kama huyo, ukiondoka si utakuwa umemsaidia sasa kuimport hata machangudoa ndani? Kama ameshindwa kumheshimu ndugu yake. Yaani mjomba wake, hivi kweli atamheshimu nani? Lakini mke pia ajiangalie labda hampi vema mmewe. Au kuna mapungufu fulani yapo ndani ya ndoa yenu. Si vizuri kuhukumu upande mmoja. Inawezekana kuna kitu huyo mme anakosa kwako. But hii ni extreme, ameshindwa hata kuchukua madada poa huko arudi kuchukua mwanae?
 
kitabibu inasemekana pia mwanaume kama alikuwa malaya akishfika umri wa 35yrs hajaiacha tabia hiyo .hatakaa aiache tena mpaka kufa na hiyo inaweza kuwa ndio tiketi yake it has been proved scientificaly na mimi namjua mtu wangu wa karibu wa hivyo .so inawezekana pia ndio ugonjwa wa huyo mumewe

Nivea...huyo sio malaya...mwanaume malaya anafanya sex for fun, huyu is not for fun...what fun can a man in 40s get from a 17 yrs old child, or even younger!? Simviki cheo cha umalaya huyo..ni fataki ka alivyosema mkewe!
 
sijui kwa nini nimetaka kutokuchangia huu uzi ila naona niseme japo kidogo tu na wewe dada davina.

kwanza nikupe pole kwa matatizo haya, ila nikutie moyo kwamba wewe sio wa kwanza kupitia haya mamii. ushauri wangu kwako ni huu hapa, kwanza jiulize unataka nini kwenye maisha yako, ukisha jua basi amua kulingana na unachokita wewe.

pima kwa akili yako uone kama hii ndoa unaiweza ama huiwezi kama unaiweza utahimili vipi hii mikiki?? na kama huiwez utahimili vipi changamoto za kutoka kuanza maisha mapya.

Kwangu mimi kosa alilofanya mumeo ni kosa ambalo linamdhalilisha yeye lkin pia linakujengea chuki na ugomvi kwako na kwa jamaa zako(wakwe). pia ukumbuke kwamba impact ya kosa hili inaweza ika extend hata kwenye visasi si tu kwako bali hata kwa wanao.

kosa hili linaweza kukusababishia wewe matatizo makubwa sana usipolihandle kwa akili sana, kwani undugu wa mumeo umeguswa kwa kiasi kikubwa sana. usikurupuke hata kidogo, tulia wala usihamaki kuanza kusema haya kwa ndugu na marafiki hapana tulia acha uwezo wa akili yako ifikiri kwa akili zaid.

kitendo cha kumfukuza huyu binti ni sawa kabisa, wala usiseme kwann umemtimua wewe tulia, na akitaka yeye ndo aseme kwann umemtimua ila wewe uwe kimya kukata mzizi wa fitina.

ukisha kaa umetulia, ongea na mumeo ukweli kwamba amekuaibisha na kwamba kwa vitendo vyake vyte vya ufuska umevumilia but kwenye hili huwez tena kuvumilia inakubidi uamue maamuzi magumu. mwambie wazi kwamba skendo yake imevuka mipaka na hata watu wana msema vibaya tena mwambie kwamba hata huyu binti kasema kwa watu kwamba sukari yake haikozi na wewe ulijifunza kuyanyamazia ila sasa mtaani ndio stori( hapa mtishe kwa maneno ya uongo lkn yatakayo mfanya aone uanaume wake unadhalilika). baada ya kumwambia then mwambie anasemaje juu ya haya maisha.

usiondoke ndani mwako ila mwambie kwa alipofikia inabidi kurevive upya ndoa yenu kwa kwenda kutubu kanisani kisha kuweka kiapo upya, kisha kupima juu ya magonjwa. sali sana juu ya ndoa yako na amani ya familia yako. wapende sana wanao timiza wajibu wako, pendeza sana hadi sasa yeye aanze kukuonea wivu. mfanye mumeo aanze kukulilia wivu kwa kupendeza, kujitoa out wenyewe kula good time nk.

mm huwa siangalii nikitaka kujipa raha ZANZI ningeifuata hata km 30 toka nyumban kwangu, tena ningekuwa namuaga kabisaa kwamba nakwenda kupata raha na friends sehem fulan sasa akili imkae sawa. nenda kazini mwako, fanya kazi, pendeza sana kila siku na pamba mpya, wape wanao raha za kufa mtu halafu yy muignore hadi point ya mwisho.

usiniulize tena kwanini nakupenda!sawa?
 
naamini kwa uwezo wa mungu mko wazima!

napenda kuwashukuru sana kwao michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm n mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia,

kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine
nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo,
, kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa, tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu)

jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wang akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gar akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake,niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri bint akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule bint akamwambia leta daftari
2akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokina, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala,

leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.
wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima, nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyua0app mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani
Kumkimbia kwa muda kwa madai ya kupumzika ni sawa na kumwachia nyani shamba la mahindi mabichi.
Dawa ni kubanana hapo hapo. Kingine cha muhimu dada ni kumuombea, matatizo mengine huwa ni roho inayotawala familia kuanzua kwa mababu hivyo ni kuzivunja kwa Jina la Yesu!
Unapomfulia nguo hakikisha unaziombea pia.
 
Kwa kumpenda mumeo, mtoto wako na wewe mwenyewe nakushauri yafuatayo;

Achana nae na uendelee na maisha yako! Usipofanya hivyo yafuatayo yanaweza kukutokea;

1. Kuambukizwa magonjwa ya zinaa
2. Kuambukizwa UKIMWI na kufa kifo cha huzuni
3. Kama mtoto wako mdogo ni wa kike ipo siku mumeo atambaka
4. Kama mtoto wako mdogo ni wa kiume ipo siku mumeo atamlawiti
5. Atakuletea watoto wa nje wengi hivyo kuleta kero na bughudha kwenye familia.
6. Kuishi maisha ya huzuni na kukosa amani, hivyo utapungua, mng'ao na uzuri wako utapotea, roho ya ukatili na chuki itakuingia, pressure itakuwa juu, Stroke itakunyemelea

Huyo zinaa imemzidi. Kama ni mtu wa dini piga goti chini msamehe KISHA endelea na maisha yako!!!! Jitahidi mtoto asiwe affected na upuzi wake.

Pole sana
 
Pole sana davina, kuna mambo mengine maishani hayana majibu ya haraka na suluhu zake sio kama hesabu za kawaida 2+2=4

Kama unamahusiano mazuri na ndugu wa mmeo, na ikiwa mila zenu hazikukatazi kwenda kwao, nenda kapumzike kwa ndugu wa mmeo, yeye usimwambi lolote ila tu mjulishe kwamba unaenda kwa ndugu zake na ukifika huko tafuta sababu yeyote usiwaambie kwanza yaliyotokea, kama bado ana chembe za ubinaadamu atakufuata na huenda hiyo ikawa ni nafasi ya wewe na yeye kuliangalia tatizo hilo kwa upya.

Mwisho, maombi ya mwenye haki yafaa sana, hasa akiomba kwa bidii.

itanipa wakati mgumu sana kukaa kwa ndugu, ndugu zake wengi wanaishi mbali alafu kijijini na kama nilivyosema hakuna ndugu wa kumkanya akamuelewa coz kwanza wanamuogopa ,
 
Back
Top Bottom