Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

Niaje wadau?

Hili tukio nililishuhudia kwa macho yangu wala sio stori..

Ilikuwa ni jijini mwanza mwaka 2006 tukiwa kwenye gari tunatoka kwenye harusi usiku kama saa nane hivi ama saa tisa usiku.

Tulitoka harusini salama salimini safari ilikuwa ndefu kidogo lkn tulipokaribia kufika gari tuliokuwa tumepanda iliishiwa mafuta!

Dereva akaipaki gari pembeni mtu mmoja akashuka kukimbilia petroli ilikuwa ni maeneo ya ghana kwa wakazi wa mwanza nadhani mnapapata.

Wakati tukisubiri petroli huku wengine wakiwa wameshuka wakibalizi ghafla tuliona mwanga wa kijani umetanda pote!

Kucheki juu niliona kitu hicho kikitoa mwanga huo huku kikienda juu kwa kasi na mwanga huo ulidumu kwa sekunde kama sita hivi na kile kilichotoa mwanga huo kilipotelea angani!

Kusema kweli mapigo ya moyo yalinienda mbiombio..Watu walisema ni satelite lkn hawakuwa na uhakika.

Kutokana na utoto nliokuwa nao sikuhoji sana lkn sasa nimelifikiria tukio lile nimekosa majibu pia nimejaribu ku google ni satelite gani ilirushwa mwaka huo but no..

Kama ni satelite ni lini Afrika ama tanzania tumeirusha huko angani mwaka 2006...? but nothing!

Wadau kama kuna alieshuhudia tukio lile na anajua ni nini kile kilichotokea anijuze maana kichwa kinanikeleketa kutaka kujua ni nini kile..?

Hata leo nimekuwa nikiwauliza na kuwakumbusha tuliokuwa nao siku ile lkn jibu walitoa ni satelite! Hivi satelite ikiwa inarushwa ndo hutokea vile..?

Na tatizo jengine nililoliona hapa ni kuwa sisi waafrika sio wafuatiliaji wa mambo kiundani.. (But not all).

Wadau ni hivyo tu kama kuna anaejua anijuze and that is all...!

Karibuni
Hicho kitu ulichokiona hata Mimi na wnzangu wanne tulikwisha wahi kukiona mwaka 1987 tulikuwa kwenye garden ya home baada ya kipindi cha marudio cha mama na mwana radio Tanzania, tulikuwa tunajiandaa kwa masomo ya usku kwa ajiri ya mtiani. Ni mwanga mkali wa bluu na ule mwanga ulipanda juu na kupotelea, ni mwanga mkubwa sana. Palepale tulikimbilia ndani tukamwuliza mzee. Akatuambia wao wanakijua kama "nyota ya jah" akasema muda ule tungeomba kitu chochote, kila mmoja wetu nasi tungefanikiwa, na kwamba ni bahati na uwezi kikiona tena maishani,,, kisayans nadhani ni U. F. O
 
Elewa Kuwa ni UFO...bado hata scientists wameshindwa kutambua...ndio maana wakaita unidentified flying object
 
Ndo nimepewa dakika chache zilizopita kilichobaki ni kupiga picha fulani niambatanishe-nitazipiga saa kumi na mbili wakati airbantu ikirushwa maana hurushwa mida hiyo tu.
i wait for it itaonekana sehemu gani..?
 
UFO.., as some may refer to it. Kuna hisia kwamba alietuumba/waliotuumba or alieu-programme huu ulimwengu ameshaandika the whole story, na hakuna utakachofanya au kutokea kitakachokuwa surprise. But surprises (bugs in a programme) may occur, UFO's could be such. Normally the programmer would rewind this simulation and correct the bug, or he may wipe out the circumstances leading to the error all together.., or to make it intresting he may just leave the simulatees with a blank. Tacheons are probably a suggestion of this pre-meditated existance, the double slit experiment hints at the rewinding and correction of errors when and as needed by the programmer. Being such, no wonder he is called all knowing, all powerful, being the simulator of our existance,nothing should be beyond the programmer, its simple logic.
 
Mwaka 2011 nilikuwa natoka Bujumbura kwa private car, nikielekea Nairobi (sikuwa pekeyangu) na ilikuwa ni Mara yangu ya kwanza kufika mwanza, tuliingia mwanza SAA sita usiku, nia na madhumuni tulale kisha asubuhi tuendelee na safari, siifahamu vizuri mitaa ya mwanza ila ilikuwa ni town maana kulikuwa na casino kama mbili hivi ktk huo mtaa. Tulitafuta hotel ya kula na kulala, nakumbuka Chumba changu kilikuwa kipo ktk ghorofa ya pili ktk hiyo hotel..sipendi kudanganya kipindi hicho nilikuwa natumia jani, basi wakati napuliza mambo yangu Kule, nilifungua dirisha ili harufu na moshi vitoke, Niliona likitu likubwa angani, Kubwa, kisha kwa mbali kama lina rangirangi za kumeta meta hivi, ila rangi nyeupe ilikuwa imetawala, nililiangalia kwa muda mrefu zaidi ya dakika 20, ckujua ni kitu gani, nikaenda kuoga kwa Mara ya pili nikiwmini labda ni stater za ganja, Hata nilipotoka kile kitu kiliendelea kuwepo pale, sikuwa na camera na cm niliacha ktk gari, ila still mpaka Leo huwa najiuliza sana kuhusu like dude, ni Kubwa mno.
 
Mkuu,
Tafuta Oxford English Readers book two kama hukusoma miaka ya 64 to 66
Abdul alitandika meza na kuweka viatu kama vile mtu amekaa.
Alianzisha hoja kuwa ameona malaika na amemkaribisha.
Kipimo cha kujua wewe ni mtu mzuri lazima umwone, usipomwona una dhambi.
Walipoingia mmoja mmoja ndani ya chumba kila alietoka alisema amemwona.hii ndio hadithi tunapewa
2006 na Leo mtu atakumbuka nini?

Nakioze;
Ningeliomba kutofautiana na weye kidogo kwa habari za kumbukumbu. Mara nyingi sana ukikumbana na kitu cha kukutisha au kukustua sana haswa ukiwa mtoto hicho kitu hakifutikagi kwenye seva ya memory yako. Hivyo, ka weye hukuwahigi kustuliwa ulipokuwa mdogo, kila kitu kwako kitakuwa ni hadithi tu. Mbona naikumbuka ndoto flani niliiota 1958 - 1960 niliokuwa naota mfulilizo kuwa naangukiwa na ndege ya kivita na mimi nilikuwa sijawahi ona ndege ya kivita mpaka nilivyokuja ziona ukubwani nazo zikifanana kabisa na nilichoota? Mambo mengine ka hayaja kutokea usiseme ati ni uzushi.
 
Kuna watu wanadhani mtu ukiwa mtoto basi ulikuwa unaota! duh! kuwa mtoto sio sababu wkt huo nilikuwa darasa la nne kwahiyo mnataka kuniambia mtu wa darasa la nne mwaka 2006 mpk leo hawezi kukumbuka kitu..?
nimekuwa hata nikimsimulia mama baadhi ya matukio kipindi nipo mdogo lkn hata yeye amekuwa akishangaa maana anadhani kwa umri ule(hata chekechea nilikuwa sijaanza) nisingeweza kukumbuka matukio mengine!

Nyie mnaosema umri kama kikwazo ndo mnaambiwa kitu na watoto wenu kisha mnapuuzia but inakuja kuwa tatizo mbeleni..
Kama ulikuwa darasa la nne 2006 ....utakuwa ulikuwa na miaka 10,11 au 12......mpaka sasa hujazidi 22 so ulikuwa Mdogo unaweza uliona kweli satellite kiongoz
 
Kama ulikuwa darasa la nne 2006 ....utakuwa ulikuwa na miaka 10,11 au 12......mpaka sasa hujazidi 22 so ulikuwa Mdogo unaweza uliona kweli satellite kiongoz
niambie sifa za satelite ikoje wkt ikiwa inarushwa..?
 
We baki ukijua kitu ulicho kiona ni kifaa kiendacho kasi na kutoa mwanga wa kijani unaotapakaa.
Kingine Mlale mapema bhana, privacy ni kitu cha muhimu sana kwenye ulimwengu wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom