Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

England%252C%2BUK%252C%2BUFO%252C%2BUFOs%252C%2Bsighting%252C%2Bsightings%252C%2Balien%252C%2Baliens%252C%2BET%252C%2Brainbow%252C%2Bdouble%252C%2BMay%252C%2B2015%252C%2Bnews%252C%2Bmarvin%252C%2Bgaye%252C%2Bimpersonator%252C%2BBirmingham%252C%2Bstrange%252C%2Bodd%252C%2Bdutch%252C%2Btop%2Bsecret%252C%2Bnasa%252C%2Blife%252C%2Bmars3.jpg
 
Niaje wadau?

Hili tukio nililishuhudia kwa macho yangu wala sio stori..

Ilikuwa ni jijini mwanza mwaka 2006 tukiwa kwenye gari tunatoka kwenye harusi usiku kama saa nane hivi ama saa tisa usiku.

Tulitoka harusini salama salimini safari ilikuwa ndefu kidogo lkn tulipokaribia kufika gari tuliokuwa tumepanda iliishiwa mafuta!

Dereva akaipaki gari pembeni mtu mmoja akashuka kukimbilia petroli ilikuwa ni maeneo ya ghana kwa wakazi wa mwanza nadhani mnapapata.

Wakati tukisubiri petroli huku wengine wakiwa wameshuka wakibalizi ghafla tuliona mwanga wa kijani umetanda pote!

Kucheki juu niliona kitu hicho kikitoa mwanga huo huku kikienda juu kwa kasi na mwanga huo ulidumu kwa sekunde kama sita hivi na kile kilichotoa mwanga huo kilipotelea angani!

Kusema kweli mapigo ya moyo yalinienda mbiombio..Watu walisema ni satelite lkn hawakuwa na uhakika.

Kutokana na utoto nliokuwa nao sikuhoji sana lkn sasa nimelifikiria tukio lile nimekosa majibu pia nimejaribu ku google ni satelite gani ilirushwa mwaka huo but no..

Kama ni satelite ni lini Afrika ama tanzania tumeirusha huko angani mwaka 2006...? but nothing!

Wadau kama kuna alieshuhudia tukio lile na anajua ni nini kile kilichotokea anijuze maana kichwa kinanikeleketa kutaka kujua ni nini kile..?

Hata leo nimekuwa nikiwauliza na kuwakumbusha tuliokuwa nao siku ile lkn jibu walitoa ni satelite! Hivi satelite ikiwa inarushwa ndo hutokea vile..?

Na tatizo jengine nililoliona hapa ni kuwa sisi waafrika sio wafuatiliaji wa mambo kiundani.. (But not all).

Wadau ni hivyo tu kama kuna anaejua anijuze and that is all...!

Karibuni

Tatizo mkuu tayari una jibu lako si umeambiwa satellite sasa hutaki kuamini Kama satellite tuambie jibu lako
 
Watanzania wengi wako kama hao ndugu zako
yaani kitu hawakijui lakini wanakipasisha kuwa ni kitu fulani baasi
hawataki hata kujisumbua tena kujiuliza

ndo maana Africa iko hivi ya mwisho duniani

Haiwezi kuwa Satelite labda ni UFO na UFO maana yake ni 'unidentified flying objects'


labda wadau wengine watakusaidia Kiranga Nyani Ngabu
UFO naomba ufafanuz brother
 
Tatizo mkuu tayari una jibu lako si umeambiwa satellite sasa hutaki kuamini Kama satellite tuambie jibu lako
Ningekuwa najua nisingeuliza!
lini tanzania imerusha satelite ama nchi yoyote ya afrika ktk mwaka huo..?
satelite ikoje na wkt wa kurushwa inakuaje..?
nifanye nijue kama nilichokiona kilikuwa ni satelite kwa kuyajibu hayo maswali
 
Mkuu The Boss nami nahisi itakuwa ni UFO. Palikuwa na mjadala mzito sana kuhusu mambo ya UFOs miaka ya nyuma kidogo, japo wajuvi wa maswala ya aviation wanasema haya mambo yalikuwa ni mwiko kuyazungumza kipindi hicho. Lakini baadaye imekuja kupata nafasi kidogo na watu wengi wakiwemo pilots wa commercial liners na military aircraft wamesema wanewahi kutana na jambo hilo.

Japo wataalam nao husema pia muda mwingine kuna watu waliona nyota ambazo zina miale mikali na ziko mbali na uso wa dunia na kutengeneza illusion kuwa ziko karibu na ni UFOs. Ila wapo ma pilots wa kijapani ambao walisema walishuhudia kabisa hiyo object na hadi kwenye rada ya ndege yao waliione lakini bado swala hili limekuwa ni utata.

Kwa wapenzi wa discovery channel kuna kipindi walikuwa wanaonyesha sana the hidden truth/conspiricay behind the UFOs. Wengi wakikataa kuhusu hizo objects na wengine wakitoa shuhuda kuwahi ziona na pia yuko pilot aliyeshuhudia kuwahi kuifuata hiyo object na kujaribu kuipiga risasi akiwa na fighter jet miaka hiyo.

Wengine wataongezea.
Naona hobby zetu zinafanana, hivyo vitu vipo kabisaaa, ukitaka kujua vizuri, nenda Youtube tafuta Section 51 utavipata mambo yote yanayozungumza kuhusu UFO na features zake, kuna mmoja aliifuma UFO kwenye eneo karibu na nyumbani kwake akaipiga video ile UFO ilikuwa kama inaelea usawa wa futi tatu toka ardhini baadae likasepa bila kishindo cha sauti wala nini, hivi vitu vipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom