Mike Tee

Feb 6, 2024
40
50
MIKE TEE
____________
Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu. Mike Tee alianza kuimba mwanzoni wa miaka 1990.

Mike Tee ni moja kati ya wasanii wa Bongo Fleva Hapa nchini Tanzania ambao walikuwa na ladha & style za kipekee kwenye upande wa uimbaji wa Nyimbo zao.

Album ya mike Tee ilikuwa inaitwa "SINTOBADILIKA" ilikuwa ina takribani nyimbo 8 ( side A & B ).

Side: A

1. Sintobadilika feat. Q chief

2. Acha kulia feat. Mr paul

3. Penzi nini

4. Siri kali feat. Tony nice

Side: B

1. Penzi ni nini feat bin Am

2. Sivainogela

3. Tuna Rap na kuimba feat. Stara

4. Nampenda Nani.

"GMC WASANII PROMOTERS L.T.D" Ndio walikuwa wasambazaji na wauzaji wakuu wa Album hiyo ya " mnyalu " kutoka kwa msanii mikee Tee Album hii ilikuwa ina mafanikio makubwa sana sokoni kutoka na kupendwa na wadau wengi wa Muziki na "cassette" nyingi ziliuzwa mtaani..

Mike tee nae alikuwa na machache ya kutueleza sisi wadau na mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva Nchini Tanzania juu ya Safari yake ya Muziki Angalau kwa ufupi tu..

"Enzi Hizo tulikuwa na kundi linaitwa the dangerous crewz (Mike Tee, Missie Annie[my sister] na Crazy Doggy)
1992 - 1998

Lakini baadae nilikuja Dar es Salaam.

Na Baada ya Adili Hisabati na Sey Fee na mimi tulipofanya ngoma inaitwa "Tamati" ndio p funk majani akasema ni vyema nirudi kama solo artist nisiwe chini ya crew kama ilivyokuwa Hapo awali..

Maneno haya aliyatoa p funk majani kwangu Baada tu yakupenda style yangu ya uimbaji.

Na kazi yangu ya Mwanzo kabisa kufanya ni ngoma inaitwa Nyaluland wengine wanaiiita Hali Halisi feat Lady Jay Dee

Mtu aliye ni inspire kufanya Muziki alikuwa Anaitwa Tony Nice Msanii kutoka kundi la Muziki wa Hip Hop lilofanya vizuri miaka hiyo ya nyuma linaitwa " WWA "(Wagumu Weusi Asilia)

huyu ndio pia alinifundisha kuandika mashairi na style
Kwa kifupi napenda kusema ndiye aliyenionyesha njia katika Ramani ya Muziki ..

Vip? wakati ukiishi upanga ulikuwa na gari aina ya Suzuki lakini kwa Bahati mbaya ukaibiwa Redio ambayo ilikuwa ndani ya gari ,hali hii uliichukuliaje muda huo ukiwa Bado upo chuoni Ifm ?. Dr Matala akiwa Mkuranga Pwani...

Pia ile nyimbo yako ya kimya changu je? Ilikuwa ni nyimbo ya Historia ya maisha yako halisi.

Mambo yaliokutokea ama ni nyimbo tu kama nyimbo zingine ambazo umekwisha wahi kutoa ..

"Kipindi nimeibiwa nilikuwa nakaa Mikocheni niliumia sana but nilikuwa nafanya biashara ya tours haikuniathiri sana niliendelea na mishe zangu kama kawaida. "

Naona kwako ilikuwa ni ni rahisi sana kwenda Bongo record na kukutana na p funk majani na kufanya nae kazi tofauti na wasanii wengine..

Lakini pia

Ebu nipe mtazamo wako maana taarifa zipo kibao mtaani kuhusu p funk majani kuwa ni producer mkorofi sanaa.

Ila wewe uliweza kufanya nae kazi na hata master jay pia tupe experience yako kutoka kwa hawa watayarishaji wakubwa Hapa Bongo ( p funk wa majani - Bongo record & master jay - mj record)

"Me nilikuwa nalipa cash tofauti na wengine walitaka kuwa chini ya label" ( Bongo Record label)

Ndio maana kwangu ikawa ni rahisi kuingia studio za Bongo record ..

Vipi kuhusu wimbo wako wa " kimya changu " ilikuwa ni true story au ilikuwa ni sehemu tu ya uandishi wa Nyimbo zako .

"Kimya changu niliandika baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu ila kuna moja Kati ya maandiko katika moja ya matoleo ya magazeti Enzi Hizo yaliokuwa yanayotoka kila wiki..

Waliandika hivi:

Mike Mwakatundu start of the ending .

Hiki kitu kiliniumiza sana ndio hasira zikaja Hapo hapo"

Na kupelekea nichukue uamuzi wa kuandika "wimbo huo"

WWA ni moja katika ya makundi/ crews za mwanzo kabisa Hapa Bongo kufanya Muziki wa Hip Hop je? unaweza kutueleza ulikutana nao vipi?

"Hao walikuwa wanasoma mkoani iringa.

mkwawa kipindi hicho ni high school na tulikuwa

tunakaa nae mtaa mmoja na tony nice one of the member
Mtaa wa wilolesi

niliposikiliza wimbo wako unaitwa " kama " kuna sehemu unasema vibanda vya mc katuni vyote napomoa "

Na Record label ya Bongo record nitaipeperusha kimataifa na watoto mic lazima wajue kushika na yote hii ni kamaa...

" Mimi target yangu ilikuwa ni kufanya investment kwenye elimu na assets tu sio kuonekana nafanya starehe na inshu za Muziki..

Pia zamani kulikuwa na ushindani mkubwa sana Kati ya wasanii wanaoimba bongo cartoon na hip hop na studio kubwa Enzi Hizo zilikuwa mbili tu bongo rec na mj rec

Vip kwa upande wa mdogo wako yupo wapi siku Hizi maana kimya kimetawala mimi katika kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba alikwisha wahi kutoa Ngoma moja tu inaitwa siwaelewi..

Kwa sasa Dada yangu Ni advocate ndio maana haimbi
Tena Muziki..

Wasanii wa zamani wengi wanadai kuwa mdosi aliwanyonya sanaaa..

Vip kwa upande wako ulipotoa Album yako ya mnyalu "ulipata kile ulichostahili" baada ya mauzo ya Album ilipofika sokoni..

Pia ni tukio Gani unalikumbuka katika historia yako ya maisha katika Muziki na huwezi kulisahau...

" Issue ya wadosi wengi iliwagusa ila nadhani baada ya kutoa album ya sintobadilika iliuza sana kuliko matatajio yangu nadhani kipindi hicho ilikuwa mm wagosi na Mr nice ndio tulifanya vizuri sokoni

Pia Kitu ambacho sitasahau ni kukataliwa kufanya show arusha coz sina hip hop song mpaka nilivyorekodi kama ndio niliruhusiwa kuimba mwanza and arusha

Hili jambo lilitokana na uhitaji wa mashabiki kwa kipindi kile maybe wanapenda sana Hip Hop ndio aliona akikuweka katika list ya watumbuizaji mashabiki watakao udhulia watakuwa wachache..

Au zilikuwa Sababu zingine nje ya Muziki kama njia ya kukwamisha kimuziki...

By that time culture ya watu wa Mwanza and Arusha walikuwa wanataka hip hop tu na ukiangalia muda huu kaskazini wana muziki wao...

________________________

Je? Wewe kama mdau wa Muziki wa Bongo Fleva Nchini Tanzania una lipi la kumshauri msanii mike Tee

Lakini ni ngoma Gani unaipenda Toka kwake.

#funguka.

UKWAJU WA KITAMBO
#tunakurudisha_kaleee!!
FB_IMG_1709973660035.jpg
 
Mshikaji yupo Wala hana mambo mengi mtu wakujichanganya na raia kiroho safi
 
Nakupendaaaaa na sifa nakupa nyakibataa(sijui kama ni sahihi) usiwaone wale wasiopenda maendeleo yaaako mpenzi waaangu. Daah ila Nature alikuwa mbaya wa chorus
 
Nature,SumaAy,Byser Blue,n mwingine Inspector Haroun toka Tmk walitisha sana enzi hizo.
Ndo wakaja kina Dully,King crazy GK Diplomatiz walitisha sana kwenye Hiphop.
Miamba ya Kwanza Unit usifanye mchezo
 
Huyo jamaa mzee wake alikuwa na pesa pale Iringa nakumbuka kipindi anasoma highland sec school alikuwa anamiliki toyota carina ED.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom