Nifanyeje kumbembeleza mme Huyu?

Nifanyeje kumbembeleza mme Huyu?

Poa basi nimeelewa mkuu

dah pole shost kwa kipigo!ila ingekua mie ndo nimechapka hvo lazima ningerudisha mashambulizi,uvumilivu mie zero,afu sababu yenyewe hata haina nguvu,sema wanaume wanajua kukuza mambo! Haya pole sana mke mwema,ungetupia picha kabsa tuone hzo nundu,huhuhu
 
Mwambie akukung'ute tena.
hahahahahaha....noma sana
teh.PNG
 
Rafiki si nimekumbia usiniite jaman

Siwez kuona au kusikia hii kitu huyu Dada kapitiliza ujasiri na hata mshipa wa aibu ndo mana alikataa kusema tatizo
Amshukuru hyo mumewe ambaye kajaliwa busara na hekima mwingine angemtegeua nyonga .....michepuko sio dili jaman aache uhuni

Sielewi tatizo ni nini..inatia hasira tamaa za kishenzi hizi....
Unatema bigijii kwa karanga ya kuonjeshwa

Haimaanishi kila aliyekosea ivunjwe ndoa ,, tushauri jamani amegundua kosa, anahitaji kujenga na mumewe, tukishindwa mshauri tutajenga au
 
siku nyingne usirudie utoto kama huo hyo inakuwa kama dhara. Ina maana urafki huo mlianza hyo siku?? Urafiki gan wa mwanamke na mwanaume tena mke wa mtu?? Ipo siku utakuja kuumia kwa kukosa maarifa.... Kwann asijulikane sku zote kama rafiki na ajulikane sku ya birthday??

chezea frends with benefits wewe
 
Adhabu alokupa ndogo sana....huna haya na wala hujui vibaya!lol
 
Haijalishi kosa, Mwanaume anaekupiga hana haya.
Na kama amekupiga mara ya kwanza his more likely to repeat again.......

Nadhani huwa hawakusudii kumpiga mke ni hasira inayoletwa na majibu ya muhusika. Unaweza ahidi kutompiga mkeo lakini IPO siku unajikuta umerusha kibao.
 
Jamani nimekosana na kipenzi changu na akanipiga sana Jana Usiku na hakukuwa na Amani kabisa,staki tununiane tena Usiku Huu, nahisi Mimi ndo mwenye makosa nifanyeje kumbembeleza na nifanyeje agundue that I am truly sorry,msaada wana MMU
Be blessed
daah, mama unakaribisha domestic violence

Haya omba kibano kingine hadi hasira zake ziishe
 
Kuna vitu unapaswa kufanya ila hufanyi na vilevile kuna vitu hupaswi kuvifanya ila wewe unafanya! Ndoa inataka uelewa mpana sana na sio mambo 6X6 tu baada ya hapo basi kila mtu anaangalia ustaarabu wake ujue hapo kuna utata na haichukui muda mrefu utasikia ndoa iko matatani.

Kupendana, kuheshimiana, kuvumiliana na kuamininana ndio nguzo pekee katika ndoa! Vingine matokeo tu!!
Ngumi kwenye ndoa zetu zisingekuwepo kama hayo niliyoyataja yangezingatiwa na wanandoa wote, fujo kwenye ndoa zinasababishwa na mmoja au wanandoa wote kujiamini kuwa anajua/wanajua kupita kiasi na kusahau kuwa ndoa ni somo lisilo na ukomo na halina graduate! Siku una-graduate kwenye ndoa yako ni siku unaingia kaburini tu...

Mtaumizana bure! kupigana ni dalili za kukosa uvumilivu au uvumilivu kufika ukomo, na hii ni hatari! Mkishaanza kupigana kwenye ndoa hata vile vionjo vya mapenzi ya dhati vinaanza kupungua hata kama mlizoea kuwasiliana kwa siku zaidi ya mara tatu itapotea! Kama mlikuwa mna mtindo wa kwenda family vacation kila mwaka utaona inatoweka na mambo mengine ndo yatakuwa priority. Hata ule moto wa "baby I miss you , Honey I love you, Darlin etc vyote hivyo vitabaki kuwa hekaya tu!!

Kaa chini na mumeo kama mnapendana, mwambie Mungu hapendi ugomvi kati ya wanandoa na kuwa unatambua kosa lako,unalijutia na hutalirudia tena. Mwambie ingawa ulikosea lakini kukupiga si kitu chema kinakuumiza kama mtoto wa kike na inapunguza upendo.
Mkumbushe the bygone days mlikuwa mkiishi vipi, the good times mlipokuwa pamoja na mipango yenu ya kimaisha ya kujenga familia bora yenye amani na upendo!

Mpendane upya na hiyo itoke mioyoni mwenu na Mungu atasimamia ndoa yenu.

Ubarikiwe!

Nimejifunza kitu kupitia ww japo ili walenga walio kwenye ndoa ila ata sisi tunaojiandaa tumepata kitu
 
Back
Top Bottom