Kuna vitu unapaswa kufanya ila hufanyi na vilevile kuna vitu hupaswi kuvifanya ila wewe unafanya! Ndoa inataka uelewa mpana sana na sio mambo 6X6 tu baada ya hapo basi kila mtu anaangalia ustaarabu wake ujue hapo kuna utata na haichukui muda mrefu utasikia ndoa iko matatani.
Kupendana, kuheshimiana, kuvumiliana na kuamininana ndio nguzo pekee katika ndoa! Vingine matokeo tu!!
Ngumi kwenye ndoa zetu zisingekuwepo kama hayo niliyoyataja yangezingatiwa na wanandoa wote, fujo kwenye ndoa zinasababishwa na mmoja au wanandoa wote kujiamini kuwa anajua/wanajua kupita kiasi na kusahau kuwa ndoa ni somo lisilo na ukomo na halina graduate! Siku una-graduate kwenye ndoa yako ni siku unaingia kaburini tu...
Mtaumizana bure! kupigana ni dalili za kukosa uvumilivu au uvumilivu kufika ukomo, na hii ni hatari! Mkishaanza kupigana kwenye ndoa hata vile vionjo vya mapenzi ya dhati vinaanza kupungua hata kama mlizoea kuwasiliana kwa siku zaidi ya mara tatu itapotea! Kama mlikuwa mna mtindo wa kwenda family vacation kila mwaka utaona inatoweka na mambo mengine ndo yatakuwa priority. Hata ule moto wa "baby I miss you , Honey I love you, Darlin etc vyote hivyo vitabaki kuwa hekaya tu!!
Kaa chini na mumeo kama mnapendana, mwambie Mungu hapendi ugomvi kati ya wanandoa na kuwa unatambua kosa lako,unalijutia na hutalirudia tena. Mwambie ingawa ulikosea lakini kukupiga si kitu chema kinakuumiza kama mtoto wa kike na inapunguza upendo.
Mkumbushe the bygone days mlikuwa mkiishi vipi, the good times mlipokuwa pamoja na mipango yenu ya kimaisha ya kujenga familia bora yenye amani na upendo!
Mpendane upya na hiyo itoke mioyoni mwenu na Mungu atasimamia ndoa yenu.
Ubarikiwe!