Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Kwakweli niffa ni mrembo we dada na unafaa kuwekwa ndani na kuhudumia ila mm siwezi hata kukuapproach maana kila nikiona comments zako nakumbuka jangid plaza, Ontario na team yako mlijua kutunyoosha mbwa nyie...!
 
Kwakweli niffa ni mrembo we dada na unafaa kuwekwa ndani na kuhudumia ila mm siwezi hata kukuapproach maana kila nikiona comments zako nakumbuka jangid plaza, Ontario na team yako mlijua kutunyoosha mbwa nyie...!
Mlikuwa wajinga wajinga tu, mlijua mtapewa pesa za bure, poor Tanzanians..kwa kirengesa.

Hata hivyo mlijinyoosha wenyewe Ontario hana hatia mlilipia ujinga wenu
 
Uislamu hauruhusu Muislamu kuolewa na asiekua Muislamu, unaolewa na mtu asiekua muislamu kutakua na kheri hapo! Kwanini usifanye subra mpaka upate Mwanamme wa kiislamu mwenye kheri nawe, unaingia kwenye mapenzi na mtu usiemjua na isitoshe sio wa imani yako!

Allah akuongoze dada yangu Nifah , akujaalie upate mume mwenye kheri nawe, nakupenda kwa ajili ya Allah
Mapenzi yaacheni tu Kama yalivyo....who knows huyo asiye muislam anaweza badili dini Kwa sababu yake?
Halafu mtume alisema akija mtu mkamridhia tabia yake muozesheni, hakusema dini yake....muhimu tabia, anaweza kuwa MUISLAMU akawa na tabia mbovu, na aside MUISLAMU akawa na tabia njema.
 
Back
Top Bottom